Mungu wa walokole ana nguvu sana 1997- 2019! Kumbukumbu zangu

Mungu wa walokole ana nguvu sana 1997- 2019! Kumbukumbu zangu

Alibarikiwa kuwa na maseyidi kumi na mawili. Ndio baba wa makabila ya kiarabu. Pia alifanywa kuwa taifa kuu. Lakini baraka ya agano ilobebwa kwenye tumbo la Sara na sio Hajiri.
 

Attachments

  • 248750_full-quotes-about-hidden-wisdom-in-the-bible-the-magical-keys-of-solomon.jpg
    248750_full-quotes-about-hidden-wisdom-in-the-bible-the-magical-keys-of-solomon.jpg
    74.2 KB · Views: 22
Kuanzia mwaka 1997 mpaka mwaka 2019 nilikua kwenye research binafsi ya mambo yasiyoonekana kwa macho ya kawaida. Nimefanya mahojiano na watu wa fani hii,kuanzia watu wa kawaida mpaka viongozi wa fani hii katika nyanja mbalimbali.

Mambo yasiyoonekana kwa macho,watu wanaita""UCHAWI""na ni fani yenye kuchanganya kidogo sababu inajumuisha imani za dini za wanadamu na imani za dini zisizo za wanadamu. Pia inajumuisha watu ambao wanaitwa bin-adamu na inajumuisha watu wale wengine ambao hawana undugu na hawa watu wanaoitwa bin-adam.Nielezee kidogo hao watu wengine,nimewaita watu sababu wana maumbo kama binadamu ila vimo vyao vipo tofauti na wapo katika jamii mbili tofauti.

Kuna ile jamii ya wanaokaa angani ambapo bila ruhusa yao huwezi kuwafikia,na kuna ile jamii ambayo hata bila ruhusa yao unaweza kuwafikia na wanakaa chini ya bahari au mito au maziwa makubwa(Lakes).Ngoja nifafanue kidogo jamii za hawa watu.

Jamii ya watu wa angani inashuka sana duniani na sijui waga wanakuja kufanya nini ila mara nyingi wanajishugulisha na wale binadamu mnaowaita walokole,na ili uzungumze nao inategemea umekutana nao katika hali gani kwenye ulimwengu usio wazi kwa macho ya kawaida,kiasili sio waongeaji sana ila sura zao zinaakisi mwanga kwa namna ya tofauti na unaweza kujiuliza wanavaa mavazi gani, kwa mavazi wanavaa hizi nguo mnaita kanzu ila ni bwanga afu ndefu mpaka miguuni na ni nyeupe.

Jamii ile nyingine ya watu wasio na asili na binadamu ila wamefanana na binadamu kimuonekano lakini wana vimo vikubwa ni ile inayokaa chini ya bahari,maziwa(Lakes) na mito.Hii jamii wao ni wazungumzaji sana afu miili yao haiakisi mwanga na wanakuja sana duniani na unaweza kuwaona bila ridhaa yao kwa kufuata utaratibu wanaokupa wafuasi wao au wanajimu wa nyota mbao ni binadamu wa kawaida,na mavazi yao ni kanzu pia ila za rangi mbalimbali zaidi ya nyeupe.Na watu wanaojishugulisha nao sana ni wale watu ambao nyinyi binadamu mnawaita wanajimu na washirikina au wachawi ila inategemea ushirikina na uchawi wa wapi maana dunia ni kubwa kutoka bara moja mpaka lingine na ushirikina au uchawi unatofautiana.

Binadamu kuna vitu huwezi kuviona mpaka either uwe mshirika wa jamii mojawapo kati ya jamii hizo mbili nilizokutajia hapo juu.Lengo langu leo ni kuzungumzia mkuu wa jamii ile ya wale watu wa angani ambao wanapenda kushirikiana na walokole au watu wa kulia lia,maana huyo mkuu ana vitu vya tofauti kidogo ndio maana nikasema pale juu kua "Mungu wa walokole ana nguvu sana".

Katika utafiti wangu ndani ya ulimwengu usio,onekana inaonyesha kua walokole wanapendelewa sana na huyo mkuu wao,maana kuna vitu anawapa vya ziada wao hawavitumii sijui kwanini niligundua hilo huko mbele katika utafiti wangu.Nimemuita Mkuu au Mungu wa walokole sababu kila walokole wanapoanza kulialia""Kusali""wale watu wa jamii ya kuakisi mwanga wengine wana mabawa na wengine hawana wakitokea kwa mkuu wa walokole ama nilivyokuja kujua baadae huko huko angani wanawajia na wanawazunguka hawaondoki na lile eneo husika linakua na mwanga unaweza kupofusha macho (Ni kama mwanga wa jua au radi au shoti za umeme zile cheche) ila walokole waga hawawaoni nadhani waga wanalia(Kusali) kwa imani zaidi namaanisha meditation.

Nilisema hapo juu kua mkuu wa walokole namaanisha Mungu wao ana nguvu sana maana wale walokole baada ya kulia kwa mkuu wao huwezi kuwasogelea katika hali ya nje ya ubinadamu au katika hali ya ushirika na jamii nyingine za kiroho zaidi ya mkuu wao na wale watu wa kuakisi mwanga.Kila mlokole anakua na yule mtu wa kuakisi mwanga na yule mtu haongei ila macho yake ni ishara tosha kua usimsogelee mlokole aliyenae.Cha ajabu wengi ya walokole hao katika hali ya ubinadamu wa kawaida hawana habari yoyote ile unawakuta sokoni au kwenye daladala au barabarani au ofisini au kwenye nyumba zao za ibada.

Sasa ikabidi nifanye uchunguzi juu ya huyo mkuu (Mungu) wa walokole,yupoje na ni nani, wale watu wa jamii ya kuakisi mwanga wanaishi nae vipi maana wana ushirika nae.Sababu ukitoka nje ya mwili kupitia(meditation) huwezi kuwasogelea hawa watu wa jamii ya kuakisi mwanga au hao walokole.Nikajikuta napata hamu ya kuchunguza mambo ya ulimwengu usionekana na hasa jamii za wale watu warefu wa angani na walokole hasa wale wa kulialia sisi binadamu tunaita kusali ila wao walokole wanaita kunena kwa lugha,na ni lugha ambayo inawafanya wawasiliane na wale watu warefu wa kuakisi mwanga.

Udadisi wangu ulijikita katika mambo makuu matano(5)
Mosi: Kwanini walokole wana uhusiano na wale watu wa kuakisi mwanga wanaotokea kule juu kusikofikika hata ukitoka nje ya mwili na kusafiri nje ya mzunguko wa sayari za kawaida kwa maelekezo ya wanajimu wa nyota?

Pili: Kwanini mkuu wa walokole namaanisha Mungu wao ana uhusiano wa moja kwa moja na wale watu wa kuakisi mwanga na sio ile jamii ya chini ya bahari?

Tatu: Kwanini katika jamii za nje ya mwanadamu au mtu, hasa ile jamii ya watu wa kuakisi mwanga ina nguvu sana kuliko jamii za wale watu wanaokaa chini ya bahari na wasioakisi mwanga wa jua na mwezi?

Nne: Mkuu wa walokole kwanini yeye na wale watu wa kuakisi mwanga,hawana ukaribu na Mkuu wa wale watu wa jamii inayokaa baharini na chini ya maziwa na mito(Maana nayo ina mkuu wake) na hataki wafuasi wake wa dini yake wawe na ukaribu na walokole kwa namna yoyote ile?

Tano: Kwanini mkuu wa walokole namaanisha Mungu wao pamoja na nguvu zoote ila hawapi utajiri wa kibinadamu hao walokole ila ukitoka nje ya mwili hawa walokole wana nguvu sana mpaka uñashindwa kuwaelezea labda uone kwa macho.Tofauti na mkuu wa ile jamii nyingine ambayo karibia robo ya wafuasi wake wana access ya kupata mali za dunia hii tunayoishi binadamu wote.

Basi nikajikuta naanza utafiti kufuatilia nguvu za mkuu wa walokole namaanisha Mungu wao.Ni nani na yupoje na anaishi wapi..Utafiti wangu ukanipelekea kuja na kichwa cha habari hapo juu kua Mungu wa walokole ana nguvu sana maana nilishuhudia mengi kumuhusu huyu Mungu wa hawa watu wa kulialia mnawaitaga walokole.

Safari yangu ya utafiti ilinikutanisha na wazee wa kibantu,wanajimu,viongozi wa dini za wanadamu zinazoonekana na zisizoonekana na watu wa jamii zile za nje ya ulimwengu wa mwanadamu.

ITAENDELEA
Uko sahihi kiongozi wangu [emoji120]

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
 
Ubarikiwe
Napokea Baraka hizo,Kwa Mikono yote, nakushukilu Sana , kwakunitakia Baraka ,

Ngoja nikufafsnulie,

Mtu akikubaliki Lile neno ni Roho ,hivyo amekubariki rohoni , maana mtu akitamka ubalikiwe hio baraka HAIONEKANIKI , maana ni ya Rohoni , Ila tu kwakuwa japo huioni unaipokea Kwa Imani ,kama Mimi nilivyoipokea Yako ,inakaa rohoni mwangu Mimi, na kuwa baraka ya kiimani maana nimepokea kiimani na ikaumbika rohoni Kwa Ile Imani , Ili Sasa inapokuja mwilini kuwa baraka kitendo, Ina mfanya mtu Huyo kuwa Baraka Kwa jamii, baraka Kwa wazazi ,ndugu ,jamaa na marafiki, Wanakuwa wanajikuta wanabarikiwa Kwa uwepo wako , maana uwepo wako ni WA mwili wako ni baraka kwao ,
 
Napokea Baraka hio ,Kwa jina lake kuu yesu kristo,

Mtu ,anapokubariki ,kama wewe ulivyo nibariki sio swala la kuchukuliwa masihara,


Maana ni moyo wa MTU umekubariki,
Na unaelewa moyo unapotowa hazina yake ya baraka,kwenda Kwa mwingine, yaani unapokerewa na moyo wangu,

Unasafirishwa kwenda Rohoni hio baraka na inakaa rohoni Kwa Ile Imani ya moyo wangu ,na huku mwilini inakuja kunipa kibari Cha kufanyika baraka wa watu wote.

Toka nijitambue ,hakuna baraka ninayoiacha kimasihara,

YAKOBO ALIIPANBANIA BARAKA MARA MBILI TENA KWA MBINDE, MPAKA MOJA WAKAGOMBANA NA KAKAE NA NYINGINE NGUMI HASWA MPAKA AKATEGUKA ,KISA BARAKA HIIHII , UNAYO NIBARIKIA KWA BURE KABISA,

ASANTE,

NA WEWE PIA UBARIKIWE
 
1.BARAKA ZA MUNGU ROHONI,
Kirohoni tumebalikiwa na Mungu Ili Kwa njia ya ROHO WAKE MTAKATIFU ACHUKUE KILE CHA ROHONI KUJA MWILINI.

2.BARAKA ZA WATU MWILINI,
Kimwili tunabarikiwa na watu ,Ili Kwa Kupitia NENO LA BARAKA,NENO ACHUKUE ILE BARAKA YA MWILINI KUIPEREKA ROHONI , NA NGUVU INAYOITEGEMEA NENO LILE LISAFIRI NI IMANI TU ,SASA INAENDA ROHONI,

SASA BARAKA ILE IKIENDA ROHONI KWA NENO INAKUTANA NA ROHO ANALIBADILISHA NENO ROHO KUWA MWILI NA KULITUMA MWILINI KWENYE ULIMWENGU WA MWILI,


NA KWA UPANDE WA MUNGU , TEARI TUMEBARIKIWA BARAKA ZOTE ,NI SWALA LA KUWA NA ROHO MTAKATIFU ,ILI AZITOWE BARAKA HIZO ZA MUNGU ROHONI KUJA MWILINI.
.
 
Napokea Baraka hio ,Kwa jina lake kuu yesu kristo,

Mtu ,anapokubariki ,kama wewe ulivyo nibariki sio swala la kuchukuliwa masihara,


Maana ni moyo wa MTU umekubariki,
Na unaelewa moyo unapotowa hazina yake ya baraka,kwenda Kwa mwingine, yaani unapokerewa na moyo wangu,

Unasafirishwa kwenda Rohoni hio baraka na inakaa rohoni Kwa Ile Imani ya moyo wangu ,na huku mwilini inakuja kunipa kibari Cha kufanyika baraka wa watu wote.

Toka nijitambue ,hakuna baraka ninayoiacha kimasihara,

YAKOBO ALIIPANBANIA BARAKA MARA MBILI TENA KWA MBINDE, MPAKA MOJA WAKAGOMBANA NA KAKAE NA NYINGINE NGUMI HASWA MPAKA AKATEGUKA ,KISA BARAKA HIIHII , UNAYO NIBARIKIA KWA BURE KABISA,

ASANTE,

NA WEWE PIA UBARIKIWE
amina!
 
Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo
warumi 10:17

4 Ninyi, watoto wadogo, mwatokana na Mungu nanyi mmewashinda, kwa sababu yeye aliye ndani yenu ni mkuu kuliko yeye aliye katika dunia.
'1 Yohane 4:4'

12 Yeye aliye naye Mwana, anao huo uzima; asiye naye Mwana wa Mungu hana huo uzima.
'1 Yohane 5:12'

12 Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake;
'Yohane 1:12'

Kwa maana ndani yake yeye tunaishi, tunakwenda, na kuwa na uhai wetu. Kama vile mmoja wenu, mtunga mashairi alivyosema, Maana sisi sote tu wazao wake.
Mdo 17:28

Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu. Nayo nuru yang’aa gizani, wala giza halikuiweza.
1Yonaha 4:5

Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.
Wafilipi 4:13
 
UNAMUHITAJI YESU KRISTO ZAIDI YA CHOCHOTE

Unaposema "mimi ni Mkristo" maanake unasema MTU NDANI YA KRISTO
Hii inamaanisha kwamba YESU KRISTO yuko kwako ambavyo naweza kusema Wakristo wengi kwasasa ni tumelibeba tu hili jina lakini YESU KRISTO hayumo ndani yetu.

YESU AMESEMA YEYE NI NJIA
Yohana 14:6

[6]Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.

Yaani YESU akiwa ndani yako basi iko njia kuu ndani yako ya kumuona MUNGU WETU WA MBINGUNI....na uzima wote unakuwa nao.....jiulize unamuona Mungu?
Unao uzima kweli?
Unatambulika ndani ya Yesu Kristo?
Kama majibu ni hapana basi hujamuweka Yesu Kristo ndani yako

Jina la Yesu lina nguvu maana hata kuzimu wanaliogopa sana. Shetani hana uwezo wowote juu ya jina la Yesu Kristo?

Hivi unajua kwamba Shetani alinyang'anywa funguo za kuzimu? Shetani hana uwezo wa kuwaweka watu kuzimu na kuwatunza huko ila mwanadamu ndo amesababisha shetani awe na uwezo wa kumiliki vile ambavyo sio vya kwake.

Ufunuo wa Yohana 1:17-18

[17]Nami nilipomwona, nalianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kuume juu yangu, akisema, Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho,
[18]na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu.

KWANINI UNATESEKA SASA?
Yesu Kristo alituondoa utumwani maanake hatupo tena utumwani. Kama upo utumwani basi unahitaji msaada leo ili uwe huru.

Unapokuwa huru maanake unaye yule anayekuweka huru ambaye alitupa nafasi kubwa ya kuishi.
Tumepewa nafasi ya kuomba lolote lakini ni mpaka tuwe ndani yake na yeye awe ndani yetu(NENO LAKE)

Yohana 15:7

[7]Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa.

BASI TUNAMUHITAJI YESU KRISTO KILA SAA ILI TUWEZE KUUSHINDA HUU ULIMWENGU.

YEYE ANATOSHA HAKIKA
NA ATAKUINUA HAKIKA

MUWEKE NDANI YAKO.....SHETANI HANA UWEZO WOWOTE JUU YA WALE WAAMINIO NA KUTEMBEA NDANI NJIA ZA MUNGU NA KUZITII SHERIA ZAKE.

SIMAMA WAKATI NI HUU UKAUTANGAZE UKRISTO ULIO HAI
 
IJUE SIRI HII ITAKUSAIDIA

Zaburi 34:16-22

[16]Uso wa BWANA ni juu ya watenda mabaya,
Aliondoe kumbukumbu lao duniani.
[17]Walilia, naye BWANA akasikia,
Akawaponya na taabu zao zote.
[18]BWANA yu karibu nao waliovunjika moyo,
Na waliopondeka roho huwaokoa.
[19]Mateso ya mwenye haki ni mengi,
Lakini BWANA humponya nayo yote.
[20]Huihifadhi mifupa yake yote,
Haukuvunjika hata mmoja.
[21]Uovu utamwua asiye haki,
Nao wamchukiao mwenye haki watahukumiwa.
[22]BWANA huzikomboa nafsi za watumishi wake,
Wala hawatahukumiwa wote wamkimbiliao.

Ubaya wowote unaotenda kila saa unakuondolea haki ya kuitwa MWANA WA MUNGU maana Mungu hakai mahala palipo na ubaya.
Imeandikwa "UACHE MABAYA UKATENDE MEMA, UTAFUTE AMANI UKAIFUATIE.
Maanake ukayaache hayo mabaya ili uweze kusimama mbele za Mungu.

Jiulize uso wa Mungu upo kwako kama mtu wa aina gani?
Hapa ndo wengi umlilia Mungu na kupeleka haja zao wakihisi watajibiwa......lazima ukayaache mabaya na kuwa katika njia iliyo ya kweli ili ukategemezwe na Mungu

Mungu anawapenda wao walio wanyenyekevu....wale walionewa na wana haki ya kutazamwa kama wahitaji na wenye kutaka msaada kwa ajili ya haki yao.

Haijalishi yako magumu mangapi unayapitia....inakuhitaji ujue hili.....UNA HAKI MBELE ZA MUNGU?


TUNAYO NEEMA KUBWA KWA MUNGU na Mungu ameweka heshima kwa yule mwenye haki(asiye na dhambi)

"UOVU UTAMWUA ASIYE HAKI,
NAO WAMCHUKIAO MWENYE HAKI WATAHUKUMIWA"

Bwana hawezi kukutupa kama umesimama naye

Jitaidi sasa unautafuta uso wa Mungu kila wakati.....tengeneza palipoharibika ili uketishwe mahala pa watakatifu wa Mungu

MUNGU ATAKUHESHIMISHA HAKIKA

OMBA NA TENGENEZA SASA

OMBA KUWA WA HAKI KWA MUNGU

ONDOA KILA AMBACHO HAKIKUPI NAFASI YA KUSIMAMA MBELE ZA USO WA MUNGU

UNAO MUDA HUU USISUBIRIE KESHO KUTENGENEZA NA MUNGU
 
Mwanzo ulipokua unasema walokole walokole sikuelewa, niakajua unaongelea makanisa ya kilokole.
Lakini kadri uzi unavyoenda nikaelewa kua watu wanatangatanga na makanisa bure tu, MUNGU yupo popote..

Wakati niko primary nilikua na imani kwelikweli, nikikumbuka enzi zile nilikua tofauto kiimani na watoto wenzangu. Nilikuwa nikimuomba MUNGU kitu kinakua.
Nakumbuka kuna siku nilipoteza kitabu cha hesabu na tulikua tunakaribia kufunga shule, na ticha alisema kama umepoteza kitabu itabidi ulipe na mimi kumwambia mshua naogopa. Basi kuna siku nilisali sana, nililia na MUNGU mno, ajabu kesho yake nilikuta kitabu kwenye begi langu wakati kilipotea kitambo sana.

Kiukweli kipindi kile nilikua na imani sana, nikisali inakua, tena vilevile au zaidi ya kile kwa njia tofauti.
Kwasasa nshakua kijana wa hovyo ila maisha ya wokovu yana raha sana aisee. Ukianza wokovu tangu utoto wako bila kupuliziwa moshi akilini alooo utapata raha maisha yako yote, utakua na stress ila MUNGU atakushangaza.
Mitihani mingi shule nimepass kimiujiza tu baada ya kusali sana.

One day Yes nitarudi kwa miguu yote miwili kwa Muumba.
Safi Sana, nimesoma ushuhuda wa kitabu Nika Kumbuka kijana wangu pia alipata muujiza kama huo, maana alipoteza akiwa likizo na alipokua a arudi shule ndio kastuka hanacho, alilia Sana, tu kamwambia mlilie Mungu anajua kilipo, a kaenda shule alipokua a natoa madaftari anasema akakiona ktk ya madaftari akafurahi yaani katoka shule anashuhudia kakwepa fimbo kwa Muujiza huu... Asee kumwamini Mungu raha Sana... Kamanda Rudi tu kwa Mungu, haja kuacha Bali umemuacha na yeye anakutamani Sana uwe mwanawe Tena.. Njoo kwa Yesu!
 
Safi Sana, nimesoma ushuhuda wa kitabu Nika Kumbuka kijana wangu pia alipata muujiza kama huo, maana alipoteza akiwa likizo na alipokua a arudi shule ndio kastuka hanacho, alilia Sana, tu kamwambia mlilie Mungu anajua kilipo, a kaenda shule alipokua a natoa madaftari anasema akakiona ktk ya madaftari akafurahi yaani katoka shule anashuhudia kakwepa fimbo kwa Muujiza huu... Asee kumwamini Mungu raha Sana... Kamanda Rudi tu kwa Mungu, haja kuacha Bali umemuacha na yeye anakutamani Sana uwe mwanawe Tena.. Njoo kwa Yesu!
Imani ni ngao....I remember Kuna siku nlilala nkaota nlikua nimesimamishwa kweny mti Kuna watu walikua wanawapiga watu mishale..ikafika zamu yangu nikawaambia Namuamini Mungu wangu hataniacha yule mtu akasema tumuone huyo Mungu wako sasa...basi akafyatua mshale mshale ukawa unakuja lkn cha ajabu kabla haijanifikia Ile mishale ikawa inapotea Yan anafyatua mshale unakuja Ile unakaribia tu kunipiga gafla mshale unapotea kusikojulikana......Imani ndo Kila kitu shetani akikutafuta Kwa njia tofaut akishindwa anaanza kuishambulia Imani yako
 
Kuna siku nlikua nimekaa ndani kwenye vile viti vya ofisin vya kuzunguka nlikua nimekaa nimeegemea Yan kama nabembea hivi gafla kiti kikanguka nilipigiza kichwa chini nlichanganyikiwa nlihis kuzimia nlipata maumiv makali sana uzuri nlikua nimesuka at least ilizuia mpasuko kichwa kilibonyea ......nlikua siwez kula mwili ulikua weak nkienda hospital daktar kanikagua kichwa kimebonyea nikapiga c ray inaonyesha hakuna mvunjiko wowote dokta akaniambia nikafanye scanning ya kichwa....hapo mwili ushaanza kudhoofu kadri siku zinavozd kwenda nkawa nkiona mwanga au sauti iwe ya tv au radio naumwa kichwa nahis kuzimia mitikisiko ya gari ,Bajaj,pikipiki nkawa naumwa kichwa......................ndani ya lisaa tu maisha yalibadilika nakumbuka Io siku nlikaa kitandani nliomba nlilia nikawa namuomba Mungu aniponye nliomba nlilia sana nkiwa katika kuomba gafla Yale maumivu yote yaliondoka nikawa mzima ...kesho yake nikaamka sisikii hata muwasho wa mbu mwilini nikawa mzimaaaaaaa
 
Kisa changu kingine....niliitwa written interview na miongoni mwa taasis kubwa za serikali hapa nchini ambayo watu huamini kua Ili uajiriwe hapo lazima uwe connection au mtoto wa kigogo.......kama mjuavyo written interview za utumishi inabidi usome haswa....Mimi sikusoma sababu Kuna mambo yalinibana nkawa nashindwa kusoma............siku nimepanda bus from dar to dodoma ndo siku nliyosoma ambapo kesho yake ndo interview ...safari nzima nkawa nasoma tu Kuna kitu kikawa kinaniambia soma hapa nasoma kazania kusoma hapa hapa usisome soma hiki soma hiki .....cha ajabu kesho yake kwenye paper asilimia 90 ya vitu vilivyotoka ndo vile nlivokua nasoma kwenye bus aiseee........nikafaulu written Kwa kishindo nikaenda oral nikafaulu pia now Niko kazini,.........wenzangu nliosoma nao hata watu wengine wanafkiri nimeingia Kwa connection wakati sikua nafahamiana na yoyote ni maombi tu...wengine wananifata wananiambia niwape connection naishiaga kucheka tu nawaambia Sali sana ndo hua jibu langu.....
 
Back
Top Bottom