King Jody
JF-Expert Member
- Oct 8, 2022
- 1,834
- 3,456
Tuombe,
Eeeh Mungu Mwenyezi Muumba Mbingu na ardhi pamoja vyote tunavyoviona na tusivyoviona, Tunakushukuru kwa zawadi ya uzima na afya njema, Tunakusifu na kukuabudu wewe kwa kuwa hakuna mungu kama wewe,
Baba tunakuomba ubariki kazi za mikono yetu, tusipungukiwe na chochote,
-Utusamehe makosa yetu
-Utuepushe na kila aina za hatari na bahati mbaya
-Uwasaidie wale wote wanaopitia changamoto mbalimbali za kimaisha, wagonjwa, waliofungwa kwa kesi za kusingiziwa , wasio na ajira na wote wanaopita changamoto za kiuchumi.
-Uwaepushe na ajali wale wote waliopo safarini.
-Ulilinde taifa letu, Uwape viongozi wetu hekima ya kuongoza nchi vema na kuwa na hofu juu yako.
Ninaomba kwa ajili ya wote wanaokumbuka na wasiokumbuka kuomba, tazama sisi sote ni watoto wako,
Katika Jina la YESU KRISTO, jina lipitalo majina yote ninaomba nikiamini AMEN.