Mungu Yupo: Majibu kwa Wasioamini

Status
Not open for further replies.

Sisi tumeshasema Mungu yupo na sababu tumetoa
Ni jukumu lako wewe kuthibitisha kuwa ushahidi wetu sio wa kweli

Badala ya kufanya hilo wewe unasema hujui
Sasa unakataa nini?
 
Thibitisho ni kwamba umeomba uthibitisho.

Ni sawa na kusema kuwa umethibitisha kuwa huna hela kwasababu umeomba hela
Hujui kuwa kuomba hela sio ishara ya kutokuwa na hela!
 
Hata ulicho quote hukielewi?
Kazi ipo!

Kimeparaganyishwa kwa bad formatting kiasi haijulikani nani kam quote nani na ipi ni subquote ya ipi.

Kabla hata ya kuanza kusoma, ile formatting tu ni headache!

I had to insert two more end quotes just to put it up in a way that is visually logical, lakini hata sina hakika nani kam quote nani hapo.

It's a mess simply.

Jifunze ku format quotes kwanza, otherwise hata kama una arguments tutaziruka tu kwa sababu ya bad formatting.
 
kaka Kiranga kuwa chonjo sana na huyu mkuu Stefano Mtangoo.nina wasiwasi atakuwa ni askofu kilaini au ni mseminary wa level ya juu sana.hawa jamaa kabla hawajapata upadre huwa wanasoma philophy kwanzwa.u can tell frm the way he argues/present his point.kwa kweli mleta mada upo juu.nakushauri kiranga round hii rudi library ukajipange upya kaka.
 
Last edited by a moderator:

Nimekuuliza maziwa ni nini unajibu mahindi ni chakula cha nguruwe huko Marekani
Yaani hujui hata nimekuuliza nini

Pia hujui ulichouliza

Umeuliza sio kweli nini
Maana yake unataka kujua ni kwanini nimesema sio kweli
Nikakuambia hata ulichokiquote hujakielewa nikirejea ulipotoa kauli yangu ya kanushi

Hapa unakuja na maelezo yanayozungumzia post nyingine ambayo hata hivyo nimeshayajibu tayari
Hii pia inaonesha vile ambavyo huwezi kujenga hoja kutokana na maandishi husika
Unachanganya mambo tu

Hujui ni wapi nimesema sio kweli na wapi nilijiquote kimakosa
Wewe unaona hayo ni jambo moja

Utaelewekaje wewe?
Utaweza kujieleza hata kile unachokihitaji kweli wewe?

Jifunze kujibu na kuuliza kwa utaratibu mzuri laa sivyo utaonekana hamnazo zaidi ya ulivyokwisha kuonekana hapa!
 

Hahahaa,

Waseminari waliosoma philosophy ya juu hawawezi kuingiza mguu hapa, wakiingiza mguu watachomoa mara moja kama alivyofanya mwalimu Augustine Mushi , mzee wa kilatini ambaye nilikuwa nakwenda naye pound for pound kuanzia ontological argument, cosmological argument, tunazama kwenye ma Anselm na Augustine philosophy huko, tunarushana kwenye Bertrand Russell na wengine wengi.

Hawa wengine hata "immanent criticism" hawajawahi kuisikia.

Huyo champion wako nimemchallenge kwa swali moja tu la "the problem of evil" mpaka sasa hajanijibu.

Wengine wananijibu wananiambia mungu anapunish watu kwa dhambi zao, sasa mtoto anayezaliwa kilema kafanya dhambi gani? Kama wazazi wake wamefanya dhambi, ni haki kumhukumu yeye?

Wengine wananiambia ooh, mungu anataka tuwe na uchaguzi kwa sababu anapenda sana uhuru wa uchaguzi.

Kama anapenda sana uhuru wa uchaguzi mbona hakuniuliza kama nataka kuzaliwa dunia hii kabla sijazaliwa?

Watu jiiii.

Majibu yao yanaza maswali zaidi ya majibu.

Na hawayajibu hayo maswali.

Hapana, usiwapandishe chati bure.

Hawajajibu maswali yangu bado.

Wamefanya kubabaisha tu, halafu wanasema "si jibu umepewa, kwani lazima liwe jibu sahihi, jibu si jibu tu?"

Wababishaji kama hawa hawawezi kuwa watu waliosoma falsafa ya juu na theolojia, kama wapo watu hao wanaoweza kunipa majibu hapa JF sijawaona bado.
 

Wewe unayeleta haya bila ushahidi ndiye unayechanganya mambo zaidi yangu.

Weka link hapa, wapi umeuliza maziwa.
 

Mmmh; Kiranga, mwaka huu kazi unayo!
 
Last edited by a moderator:
Kwani mfinyanzi akiamua kuvunja vitu vyota alivyovifinyanga, ni kipi kati ya hivyo kitamwuliza kwa nini amevivunja?
 
Mmmh; Kiranga, mwaka huu kazi unayo!

Kazi wanayo wao ambao hawajajibu "the problem of evil".

Huyo mseminari uchwara anakwambia huwezi kuwa na ethical system bila mungu.

Wakati watu wanakwiba mpaka Vatican huko na makanisani kwingine, huku huko Asia kuna jamii ambazo zinakataa kuwepo kwa mungu na zina ethics nzuri tu.

Tatizo ni kuwa mtu wa kitabu kimoja, hujui hata watu wengine wanaishije duniani, lazima utakuwa kama yule kipofu aliyepata kushika mkia wa tembo.

Akiulizwa "Tembo yukoje?" ni lazima aitaje reference yake moja tu anayoijua.

Atakwambia "Tembo yupo kama kamba hivi".

Kwa sababu ndiyo experience yake pekee ya tembo.

Mkia.
 

Csemi kitu...haya mkuu.
 
Kwani mfinyanzi akiamua kuvunja vitu vyota alivyovifinyanga, ni kipi kati ya hivyo kitamwuliza kwa nini amevivunja?

You are getting ahead of yourself in a circular way.

Ni lazima uoneshe kwamba kuna mfinyanzi kwanza.

Halafu, mfinyanzi akijinadi kwamba yeye anapenda sana kazi yake, na ana uwezo na ujuzi wote, na alivyovifinyanga vina uhai, na vinaogopa kufa, na kavikataza kuuana, akija yeye kuvivunjilia mbali na kuviua wakati ana uwezo wa kuviepusha na maumivu na kifo, atakuwa haeleweki.

Upande mmoja anasema anavipenda viumbe vyake, upande mwingine ana uwezo wa kuzuia visipate maumivu, vilema etc, lakini hazuii.

Ni contradiction.

Mungu angesema "mimi ni badass, nimewaumba binadamu lakini siwajali, kivyenu" nisingeshangaa.

Lakini tunaambiwa mungu ana uwezo mkuu na ujuzi mkuu na upendo mkuu.

Sasa mbona huu upendo mkuu kama unapitwa na upendo wa kibinadamu tu?

Mungu anawaumba binadamu bila chanjo. Wamekufa kwa kupuputika kwa mamilioni ya miaka, wameumwa magonjwa yanayozuilika kirahisi kwake, na mpaka leo wanatatizwa.

Yeye kaangalia tu.

Mpaka binadamu wahangaike saaana wagundue dawa/ chanjo wenyewe.

Kwa nini anakuwa anatubania hivi wakati yeye mwenyewe ndiye aliyetuumba na ana uwezo wote na upendo wote?

Au hizi ni stories tu?

Mana hali halisi imekaa inconsistent na mungu mwenye uwezo wote na upendo wote anavyoweza kufanya.

Hata wanadamu tu ambao hawana uwezo wote na upendo wote na ujuzi wote wana moyo wa huruma zaidi ya huyu mungu.

Sasa inakuwaje mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote awe mkatili kuliko wanadamu amabao hawana ujuzi wote, uwezo wote wala upendo wote?

cc Anheuser
 
Csemi kitu...haya mkuu.

Hata kusema husemi kitu ndo ushasema hivyo.

Old schoolers wanaweza kukumbuka hadithi ya darasa la pili "Heri mimi Sijasema".

Kuna mtu alipigwa mkuki vitani (mafichoni) kwa kusema "heri mimi sijasema" akikebehi wenzake waliopigwa mikuki kwa kulia badala ya kuvunga kufa.

Kama unavunga kufa vunga kufa tu.

Ukisema "heri mimi sijasema" ndiyo unakuwa ushasema hivyo, mkuki unakufuata.
 
Wewe unayeleta haya bila ushahidi ndiye unayechanganya mambo zaidi yangu.
Weka link hapa, wapi umeuliza maziwa.

Hii akili ndio iweze kumjua Mungu kweli?

Mtu haelewi anachoandikiwa ataelewa kikubwa kuliko hicho?
 

Naomba majibu ya maswali yangu
Yapo page no 5

Hebu jibu acha kupiga blabla tu hapa!
 

hahaha
 
Hii akili ndio iweze kumjua Mungu kweli?

Mtu haelewi anachoandikiwa ataelewa kikubwa kuliko hicho?

Haiwezi kumjua mungu, kwa sababu hayupo.

Kama yupo toa uthibitisho.
 

Hahaa yaani binadamu yuko compassionate zaidi ya mungu!

Ndo maana nishasema ukiamua kuamini hizi habari za mungu ni lazima ujitoe fahamu walau kidogo la sivyo utaishia kuona dhani nzima ni a bunch of BS tu.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…