Huwa siwaelewi mnapomkana Mungu na kuleta "problem of evil". hili swali nimelijibu katika uzi huu na kama hujaelewa nitarudia.
Kiranga , unaposema "problem of evil" huoni unafanya "assumption" zinazodai/zinazolazimu uwepo wa Mungu? Unatofautishaje mema na mabaya katika ulimwengu ambao hakuna Mungu? Maana kusema tu "evil" una "imply" aina fulani ya sheria ya maadili (Moral Law) na hivyo Mtoa/Mtunga sheria hiyo (Mungu). Sasa kama wewe huamini kuwa Kuna Mungu, unatofautishaje kati ya zuri na baya? utuambie hili kwanza kabla hata hujauliza kuhusu "problem of evil". maana kama huwezi kutuambia tofauti ya jema na baya, then kwanini tuendelee zaidi ya hapo?
Wewe ulitaka afanyeje? atengeneze watu ambao hawana uhuru wa kuchagua? Kama angefanya unavyotaka unafikiri angekuwa ameumba watu kwa mfano wake? Unafikiri kuna upendo bila kuchagua?
Imagine mke wako ukitaka akubusu anakubusu hata kama yeye hataki. Utakwenda mtaani kifua mbele kuwa kuna upendo kati yenu?
Mungu yuko sahihi kabisa kuumba ulimwengu wa namna hii na ndio maana Yesu ni mwanakondoo aliyechinjwa kabla ya misingi ya ulimwengu kuwekwa. Hii ni kwa sababu Mungu aliamua (in his Sovereign choice) kuumba ulimwengu ambao si tu kwamba alijua maovu yanawezekana bali alijua pia Mwaadamu huyu ataasi. Na akaamua kuonyesha ni wa Upendo zaidi kwa kufanya njia ya kumwokoa toka katika uovu wake: Mpango ambao wewe
Kiranga unaukana leo hii.
Kwa kuumba ulimwengu wa namna hii Mungu amedhihirisha upendo mkuu sana (Yohana 3)
Simple! Kuna Magonjwa kwa sababu kuna dhambi. Kuna dhambi kwa sababu Mwanadamu aliamua kumwasi Mungu. Mwanadamu alimwasi Mungu kwa sababu ya kutumia vibaya utashi wake. Mwanadamu alikuwa na utashi kwa sababu Mungu alimuumba na uwezo wa kuchagua. Mungu alimuumba na uwezo wa kuchagua kwa sababu Mungu nu pendo. Kwa hiyo "ultimately" kuna magonjwa kwa sababu kuna Mungu!
Unadhani kuna mahali popote ambapo ni sahihi kwa mtu kumbaka mtoto mchanga na kumkatakata vipande kisha kula nyama yake? Jibu lako lina maana gani (what does your answer imply)?
Hili tatizo lingine la wasioamini Mungu! Kama unaamini katika naturalism (kama ambavyo nimekusoma katika nyuzi kadhaa) kwa nini utumie "compassion, logic, ethics," vitu ambavyo havionekaniki wala kushikika? Na pia hapa unajaribu kusema kuwa "God is morally wrong" na mimi nauliza "Under which Moral Law is God wrong?". Unapimaje ethics za Mungu na kuzithibitisha kuwa ziko chini? What are the scales?
Katika ulimwengu/Dini unayoiamini ya "random and chance" kuna tatizo gani mtoto kuzaliwa kipofu? Katika dini yako ya "Hakuna Mungu" na hivyo hakuna "Ultimate Law" kuna tofauti gani kati ya mema na mabaya? Hitler aliona ni jambo Jema kuua wayahudi Mil 6+ na Stallin akaona ni jambo zuri tu kuua mamilioni ya Warusi. Kuna watu wanaona ni vyema wakibaka au kuua. Katika dini yenu ya hakuna Mungu, unawahukumu wana kosa? Kwa sheria ipi?
Baba A akiona ni vyema kuwapa watoto chakula na Baba B akaona ni vyema watoto wake wakafa na njaa, na wote hawa ni binadamu, nani atakuwa amekosea? Kwa sheria ipi hiyo ya ubinadamu maana hawa wote ni wanadamu!
Hujatuambia pa sheria hiyo mtunzi wake ni nani na kwa mamlaka gani aliitunga sheria hii!
You are right na ndivyo alivyo!
Una maana hata pale viumbe hawa wanapochagua mauti badala ya uzima Mungu awalazimishe? Mfano, wewe Kiranga leo umemkataa Mungu mbele yetu sote, halafu unatarajia kwa sababu ya upendo wake akuachie tu uende, are you kidding? Hakimu anapotoa hukumu huitoa kwa upendo kwa kuwa ni haki stahili. Haya Magonjwa ni haki stahili ya Mwanadamu kwa sababu ya kuukaribisha uasi (dhambi). Huwezi kukaribisha adui halafu ukalalamikia madhara yake. Each choice have its consequence!
Bill hajawahi kumsaidia Mungu kazi hata siku moja. kupeleka chanjo Afrika haijawahi kuwa kazi ya Mungu. Umelipata wapi hili?
Jibu la swali hili nimeshalijibu hapo juu...madhara ya kukaribisha adui si kazi ya Mungu kuyabeba. Ukweli hata kama unauma ndio ukweli wenyewe!
Check the answer above! Huna haki ya kudai habari ya mabaya wakati unasema hakuna Mungu!
Swali hili unabadili tu namna ya kuliuliza na nimeshalijibu hapo juu!
Anyway hujaweka ushahidi wowote kuwa hakuna Mungu zaidi ya kuhoji kwa nini Mungu kama yupo alifanya A B C. Hakuna mahali umefuta point zangu na kwa ukweli umehakikisha nilichokisema kuwa ni dini yako tu inayokataa uwepo wa Mungu inakulazimisha kufika uliko. Si kwa sababu hakuna Mungu bali kwa sababu hutaki kukubali uwepo wake ambao pia wajua ni halisi
Umeruka na kukimbia point zangu badala ya kuzijibu moja baada ya nyingine.
Mungu yupo, alikuweko na ataendelea kuwepo!
Huu ndio ukweli mchungu!