Hata maraıs wote walio pita walikuwa na mazuri na mapungufu mengi tu.
Na hii inahusu marais wa nchi zote.
Mbowe ana sıfa zake, lakini anataka maridhiano yasiyo na faida wa CDM.
Kusema kuwa watu wametolewa gerezani sababu ya maridhiano iwe ndivyo au sivyo siyo hoja ya kuifanya CDM ipoe.
Itakuwa ni mchezo wa onea, weka gerezani, maridhiano, achia. Je, CDM iishi kwa namna hiyo?
Tunataka viongozi wa upinzani, wanao tabirika, wenye misimamo, wanao kemer kila uovu, wenye kudai haki siyo kubembeleza.
Nina hakika ikitokea CCM ni wapinzani hawawezi kuwa legelege hata kidogo.
Tuna vyama vingi vya upinzani lakini vipo kusubiri matukio na kupongeza pongeza tu. Na CDM sasa inaenda kwenye mkumbo huo.
Leo hii, hata wana CCM walio kuwa wapondaji wa CDM eti wanashauri CDM ichague kiongozi yupi, kwa upendo gani?
Kama wapiga kura wa CDM wanataka chama chao kiwe bingwa wa maridhiano, pongeza pongeza na kuvizia matukio, wakamchague Mbowe.
Lakinı kama wanataka chama motomoto kinachotoa changamoto mfululizo ndani na nje ya bunge wamchague Lissu.
Rejea kauli za marais watatu wa Tanzania nyakati tofauti tofauti. (Mmoja alisema. Bora Slaa awe rais kuliko Lissu kuwa mbunge)