Musoma: Padri wa Kanisa Katoliki Jimbo la Bunda apandishwa Kortini kwa kuongoza Genge la Uhalifu

Ithibitishe nini? Mtu anaiba 1.7B? Kwaninn wamemtuhumu yeye na wahasibu wake? Kwanini wasikutuhumu wewe?
Kuna kitu kinaitwa accountability, askari anaua raia halafu IGP anaambiwa ajiuzuru, au timu inafugwa halafu kocha ndio anafukuzwa. Inawezekana hajaiba ila hakutimiza wajibu wake vizuri na kusababisha hizo pesa zikaibwa ndio maana nimesema tuwe na akiba ya maneno mpaka pale aitakapothibitika kuwa ameiba.
 

Hamna cha accountability , kuna Due diligence huawezi ku approve hela itoke bila kwanza kukaa vikao vya kupitisha ,hela kabla haijaombwa kwanza mnaandaa vikao vya bajeti ikiwa na wadau wote then mkisha jadiliana then ndiyo zinakuja official approval...Kwahiyo huyo Padre na muhasibu wake wanajua A to Z wizi wa 1.7B na other currencies.
 
Jamaniii tunahitaji kufuatilia kwa kina kuhusu taarifaa zinazotolewa na vyombo vya habari... Kiuhalisia Papa hatoi hamasa ila ameomba watu Hawa wasitengwe Bali kujenga ukaribu nao nakuwapa mafundisho kutokana na maandiko yanavotuomba kufanya

Vinginevyo watu hai wakiachwa wajitawale waoo pekee wataharibu jamii na kuteka idadi kubaa ya watu lkn Kama tutakuwa karibu nap bila kuwatenga na tukizidi kuwaonya na kukemea tabia ilee wapo watakaooongoka miongon mwao na kuwasaidia wengine pia miongoni mwaoo
 
Zaidi Sana jamani hakuna ufahari Wala amani kuona ndugu ama rafiki yako akiangamia ilee Hali unao uaezo wa kumsaidia... Walakini swali kuwa utatumia njia gani iliyosahihi kuokoa nafsi yakee??

Tuone hapa kidogo..

a mathayo 18:12-14
“Mnaonaje? Kama mtu ana kondoo mia moja na mmoja wao akapotea, hatawaacha wale tisini na tisa mlimani aende kumtafuta yule aliyepotea? Na akisha mpata, nawaambia kweli, anafurahi zaidi kwa ajili ya huyo kondoo kuliko kwa wale tisini na tisa ambao hawakupotea. Hali kadhalika, Baba yenu wa mbin guni hapendi hata mmojawapo wa hawa wadogo apotee.”

Hawa wenzetu wamekosaa kweli ila tujitahidi kutoa ushauri wa njia Bora zaidiii ktk kunusuru Hali hiii ktk jamii yetu.
 
Musoma: Padri wa Kanisa Katoliki Jimbo la Bunda apandishwa Kortini kwa kuongoza Genge la Uhalifu

Padri wa Kanisa Katoliki Jimbo la Bunda mkoani Mara nchini Tanzania, Karoli Mganga amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Musoma akikabiliwa na mashtaka 178, likiwemo la kuongoza genge la uhalifu.

Mbali na padri huyo, mshtakiwa mwingine katika kesi hiyo ni aliyekuwa mhasibu wa kanisa hilo Jimbo la Bunda, Gerald Mgendigendi.

Washtakiwa hao wamefikishwa mahakamani hapo leo Jumanne Agosti 6, 2024 mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Aloyce Katemana na kusomewa mashtaka yanayowakabili.

Akiwasomea mashtaka hayo, Mkuu wa Mashtaka Mkoa wa Mara, Amoscsye Erasto amedai walitenda kosa la kughushi nyaraka, kinyume na sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16, marejeo ya mwaka 2022.

Amedai washtakiwa hao wakiwa watumishi wa kanisa hilo, waliiba fedha Sh1.7 bilioni pamoja na fedha za kigeni, ikiwepo Dola zaidi ya 100,000 na Euro zaidi ya 20,000.

Amedai jumla wanakabiliwa na mashtaka 178, yakiwemo ya kuongoza genge la uhalifu, utakatishaji fedha pamoja mashtaka mengine mengi.

Hata hivyo, baada ya kusomewa mashtaka hayo hawakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa Mahakama hiyo haina mamlaka kisheria kusikiliza kesi hiyo. Kesi itatajwa tena Agosti 20, 2024 na washtakiwa wamepelekwa rumande.
 
Well-done jeshiketu

Na wale wahuni pls 😂😂😂

✍️Kwa buza
 
Huyo Padre kama ni yule mchaga kuna kipindi alikuwa Parokia moja huko ukrewe ndani maeneo ya Serema, anapenda hela sana na mwizi haswa ndani ya miaka miwili baada ya kuhamia pale alifanya vitu binafsi vilivyowafikirisha wenyeji wapi anapata ukwasi
Mchaga hata awe padri ni mchaga tu lazima maokoto kwanza
 
Ndugu zangu Watanzania,

Soma mwenyewe hapa maana sitaki kuweka maneno mengi.
---
Padri wa Kanisa Katoliki Jimbo la Bunda pamoja na Mhasibu walifikishwa Mahakamani Agosti 6, 2024 na kusomewa mashtaka na Mkuu wa Mashtaka wa Mkoa wa Mara, Amoscsye Erasto ambapo wana jumla ya mashtaka 178 ikiwemo wizi wa takriban Tsh. Bilioni 1.7

Aidha, washtakiwa hawajajibu chochote kwa kuwa Mahakama hiyo haina Mamlaka Kisheria kusikiliza kesi hiyo. Kesi itatajwa tena Agosti 20, 2024 na Washtakiwa wamebaki rumande

Viongozi wa Dini kuhusishwa na tuhuma za ulaghai au udanganyifu, kuna athari zipi katika jamii?

​

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…