Uchaguzi 2020 Musoma: Tundu Lissu alala Butiama nyumbani kwa Mwalimu Nyerere

Uchaguzi 2020 Musoma: Tundu Lissu alala Butiama nyumbani kwa Mwalimu Nyerere

Watu wa Butiama unawajua ? Mpaka wakawapa kura kidogo hivyo wakati wanamjua baba yao vizuri INA maana waliwaona hawako vizuri kabisa

Hata familia na ukoo wa Nyerere ulioko Butiama maana yake umewakataa haiwezekani Madaraka apate kura 2 na mwenzie Makongoro apate kura Tano

Huo ni ujumbe wa wazi kuwa ukoo wa Nyerere hawawataki
Sasa kama ukoo umetuma hiyo meseji huwezi force
Ukoo wa Nyerere siyo uliopiga kura za maoni acha upotoshaji.

Ukoo wa Nyerere ni mdogo sana pale Zanaki, hata kura zingepigwa kwa koo wasingeshinda acha kupotosha.

Musoma hakuna tabia za kujipendekeza kwa familia maarufu, hayo mambo yapo huko kwa waswahili wenzenu, Chalinze, Lindi and likes.
 
Hasira zao za kushindwa tu kura za maoni

Watoto wa Mwalimu Julius Nyerere, Makongoro na Madaraka, wamepata kura chache katika kura za maoni Jimboni kwao Butiama, Mara.




Jimbo la Butiama lilikuwa na wagombea 59 na wajumbe waliopiga kura walikuwa 555 na matokeo yaliongozwa na Jumanne Sagini aliyepata kura 84, akifuatiwa na Frank Mahemba aliyepata kura 80, wa tatu akiwa Joseph Nyamboha kura 46.

Katika kura hizo za maoni Makongoro Nyerere alipata kura 5 na Madaraka Nyerere aliambulia kura 2. Makongoro Nyerere aliwahi kuwa Mbunge wa Arusha kupitia NCCR-Mageuzi.
Shida mnasahau utu mnawaza siasa kila saa.... acheni roho za kwanini.. ukarimu ni asili yetu wa TZ. Itikadi za vyama sio sababu ya kunyimana msosi babu

Ule msemo Wa maendeleo haya chama mbona kama hujauwelewa vile
 
Mbona na breakfast alipata hapohapo nyumbani kwa mwalimu?

Magufuli amekwenda mkoa wa Mara, badala ya kwenda nyumbani kwa mwalimu yeye amemsumbuwa yule bibi kizee kutoka Butiama mpaka Musoma mjini kwenda kuongeza vichwa, hivi nyinyi mna akili timamu kweli?
Wazitoe wapi?? [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Waligombea kura za maoni watu wa jimbo hilo wakawanyima kura Makongoro alipata kura tano mwiingine huyo madaraka alipata kura tatu naona wana hasira

Kura wakose wao hasira wazioyesheee kwa kumlaza Lisu kwao!!!!!!
Hayajitambui, mtu alimtukana baba yao hadharani kabisa
 
Hii lazima magufuli atalipa kisasi kwa kuombwa kukaribishwa na familia ya Nyerere.....

Tundu Lissu akili mingi
 
Msimamo wa Lissu upo wazi kw mambo anayokubaliana na Nyerere na mengine amepinga hadharani. Na hata Nyerere mwenyewe amewahi kujikosoa katika hayo kwa kauli yake. Huyu Mujuba wa CCM anasema yeye anamuenzi na anafanana na Nyerere nje ndani ila cha ajabu huyu anatofautiana na Nyerere kwa kupenda sifa za kijinga na umimi. Hajali uhai wa mtu mmoja ukipotea.
 
Huyu jamaa alisema Bungeni kuwa Nyerere alikuwa ni Mwongo, hali iliyosbabaisha Tundu awe na uhusiano mbaya sana na mwasisi wa CHADEMA, Edwin Mtei; leo anajisikiaje furaha kwenda nyumbani kwa mtu aliyemwita mwongo? Opportunist wa kutafuta photo ops tu.

Mwitongo ni sehemu ya makumbusho ya taifa ambayo kila mtu anayeitembelea atapokelewa vizuri tu.

..hiyo lodge aliyofikia inasemekana ni mali ya Madaraka Nyerere.

..sasa nyinyi mlitaka wamnyime huduma Tundu Lissu na msafara wake? sheria zinazuruhusu?

..Siku chache baada ya Tundu Lissu kurejea nchini, Andrew Nyerere alilamika kumkuta Cyprian Musiba nyumbani kwao Msasani akirekodi video zake za kumkashifu Tundu Lissu. Na inasemekana aliyempeleka Musiba nyumbani kwa Mwalimu ni Makongoro Nyerere.

..Tukio hili la Mwitongo, na tukio la Msasani, linatonyesha kwamba watoto wa Mwalimu Nyerere wana mitizamo tofauti kuhusu Tundu Lissu.
 
Mgombea wa Urais wa CHADEMA amelala Nyumbani kwa Mama Maria Nyerere Mjane wa Baba wa Taifa

Kwa heshima anayopewa Baba wa Taifa ndani ya CCM na nchi kwa Ujumla hii haina madhara kwa familia na Chama?

Ukiipangia familia ya Nyerere nani wa kulala nyumbani kwao leo mwisho utawapangia mboga ya kupika leo.
 
Imesikika mama Maria akilalamika kukosa Raha, amedai yule mlinzi wake wa ccm anamganda kweli mpaka kusikiliza simu anazopokea, kudhibiti wageni wake,

Yote hiyo Ni hofu ya mtawala wa sasa wa ccm, ambaye miaka yote 5 amedukua simu za wenzie mpa uchagoni
 
Mgombea wa Urais wa CHADEMA amelala Nyumbani kwa Mama Maria Nyerere Mjane wa Baba wa Taifa

Kwa heshima anayopewa Baba wa Taifa ndani ya CCM na nchi kwa Ujumla hii haina madhara kwa familia na Chama?


Mimi kabla ya kusema lolote, labda na wewe mleta mada useme mantiki ya hoja yako ni nini?

Je, una maana kuwa kuna mtu ama taasisi inataka kuichagulie familia hii ya mzee Nyerere marafiki na maadui?
 
Kwa nafasi ya Familia ya Nyerere hawatakiwi kuwa na upande. Kwa sababu hata mfumo wa vyama vingi ulihasisiwa na Nyerere na hupo kisheria. Na Nyerere ni Baba wa Taifa.
 
Mgombea wa Urais wa CHADEMA amelala Nyumbani kwa Mama Maria Nyerere Mjane wa Baba wa Taifa

Kwa heshima anayopewa Baba wa Taifa ndani ya CCM na nchi kwa Ujumla hii haina madhara kwa familia na Chama?

Lissu aliombwa kwa heshma na familia hii akapumzike kwao. Ujue kwamba watu wengi sana wamechoka na magufuli wakiongozwa na familia ya Nyerere. Hakuna madhara kwa akina Nyerere ila yapo madhara makubwa kwa ccm na magufuli kwani hawajubaliki.
 
Back
Top Bottom