Musukuma afunguka Mazito Mkataba wa Bandari/Sijajongwa Gari, Nina Hela

Musukuma afunguka Mazito Mkataba wa Bandari/Sijajongwa Gari, Nina Hela

Kipengere Cha juu kinazungumzia jinsi ya kuvunja mkataba,mambwiga wenye uelewa finyu wanalalama mkataba wa milele Mara miaka mia,wajinga wengi Sana nchi hii
Kwani nchi hii mara ngapi imeingizwa chaka na mikataba fake? Maana kama mabwiga basi ndio watakuwa hao walio andaa Dowans,Escrow, Richmond nk na ndio inawezekana wakawa ndio hawa hawa kwenye bandari.

Kweli wajinga wengi sana nchi hii na ndio maana hao mbwiga wakaingiza chaka nchi hii kwenye Escrow, Dowans na Richmond.

Ila kumbuka hata saa mbovu kuna mda inapatia majira, pili kwenye malumbano ya hoja jifunze kuheshimu watu sometimes unaweza hata kujifunza kutokea kwa huyo unaye muona mjinga.

Train your brain kuhimili hoja ngumu hata kama kwenye swala hilo kuna maslahi yako na si kuanza kuprovoke watu.
 
Kuna kigogo awamu ya nne alihongwa binti na muarabu mashuhuri iringa hata sasa anamke iringa.... haya maneno kuwa msukuma alipewa namba ya simu siwezi kuona kama ni uzushi kabisa
Mhusika mwenyewe alisema kuwa alimshuhudia huyo Binti akiongoza mashine huko Dubai... Na namba alichukua... Na Bado anayo!
 
Angekua na akili angenyamaza raia wangeipotezea. Lkn kwa kuliongelea ameonyesha moja kwa moja amehongwa Kama Malaya yoyote yule anayehongwa ili mwili na utu wake udhalilishwe na waarabu.
 
Watu kama hawa inatakiwa akirudi nyumbani kwake anakuta mji wake umepigwa moto na maslahi yake popote yalipo yanakuwa targeted!
Uone kama atakuja kurudia upuuzi wake, Watanzania sisi wapole sana!
nenda wewe ukafanye hivyo.
 
Huyu Msukuma ni very bright aingie Open University achukue Degree zake pesa anayo.

Ana uwezo mkubwa wa kupambanua mambo, sio wale wa Mbina nyama nyoo na walwa.
 
Hivi Siku tisa zinaweza kufundisha kitu ukapewa cheti? Vp kwamba umeonyeshwa sukari kumbe nyuma ya pazia kuna shubiri? Sio kila kinacho nga'aa Siku tisa ni dhahabu. Soma kesi za hiyo kampuni ya dp world
 
Huyo Sukuma gang ni useless kama wengine tu wale chawa pro hana jipya.
Tatizo lake King Dk. Msukuma ni La Saba. Anafuata tu upepo unapopuliza! Miaka kadhaa nyuma kabla hajawa Mbunge niliwahi kukutana nae Plazma Hotel pale Kona ya Nyegezi, Mwanza Jiji kuelekea SAUT nilijidhisha ni mtu mwenye uwezo mdogo sana. Unachohitaji ni kumshawishi tu!
 
Sisi hatutaki hela tunataka mali yetu tusimamie wenyewe sisi sio wajinga kuweka pesa mbele sisi tunataka heshima, tutajirike wenyewe wageni waarabu watakusaidia nini wakati na wao wanataka kupata faida.
 
Mh msukuma hajaelewa hoja iliyoko mezani.
Hakuna mtu anakataa wawekezaji ila tunanufaikaje kusema tu mapato yatapanda haitoshi...yatapanda katika makubaliano gani?
Amesema miaka mia ni uzushi je mkataba ni WA miaka mingapi wewe mzee uliyeenda Dubai tuambie?
Halafu amesema hakuna mkataba usio na pa kutokea kama makubaliano hayajafikiwa bila kutaja kifungu cha mkataba kinachoruhusu kuvunjwa.
Anataja nchi ambazo DP inaoperate bila kusema ni kwa namna gani mikataba hiyo inafanana na wa kwetu jamani huyu mtu vipi.
Wakuu pelekeni watoto shule.
 
Jibuni hoja zake kiuchumi kasema badala ya kukusanya 7bn wanapanda 18bn ajira kutoka 1200 kuenda 75000, hojini hivyo kuliko kipiga kelele

Usitazame katika Angle moja tu , Litazame hili swala Kiusalama pia.
 
Usitazame katika Angle moja tu , Litazame hili swala Kiusalama pia.
Kwamba tutavamiwa? Serikali inauwezo wa kupenyeza Tiss katika kila tasisi ataikiwa ya kimataifa kwahilo sidhani kama kutakua na shida yeyote
 
Kwamba tutavamiwa? Serikali inauwezo wa kupenyeza Tiss katika kila tasisi ataikiwa ya kimataifa kwahilo sidhani kama kutakua na shida yeyote

[emoji849]

Kiusalama hatutakuwa Salama.
Bare hii statement utaikumbuka siku moja endapo hili dili halamu litapitishwa.
 
[emoji849]

Kiusalama hatutakuwa Salama.
Bare hii statement utaikumbuka siku moja endapo hili dili halamu litapitishwa.
Kivip mkuu? Hi nchi masikini mtu akiiraji chochote anauwezo wakutufikia maadui wetu wakuu ni wana siasa hatuna adui wa nje ya nchi anae tisha
 
Majizi kama hao ni hatari kwenye nchi. Hivi kweli CCM wameamua kuuza Bandari yetu?
Waache wauze,ikiwezekana wauze na uwanja wa ndege...wauze kila kitu kinachouzika...BORA TUUUZWE TU KULIKO KUWA CHINI YA CCM
 
Ukiachana na kichwa chako cha habari. Alichokiongea Msukuma kuhusu mfumo wa sasa wa bandari yetu ni kweli tuko nyuma sana. Inahitaji mwekezaji. Tena ningependa awe pia ndio mtoza kodi tuondokane na hawa TRA. Ameongea point sana hii kuwa na bandati ya kisasa kubwa ni lazima ikumbane na vikwazo vikubwa ksbb moja kwa moja unaingia kwenye vita kubwa ya kiuchumi na mataifa yenye bandari.

Pia tayari tunaenda kukata mirija ya miaka mingi ya baadhi ya watu pale bandarini. Ni muhimu sana sasa kwa bandari yetu kuingia ktk hii hatua. Tumechelewa mno. Naunga mkono hoja 100%.
 
Back
Top Bottom