Muswada wa Mabadiliko ya Sheria ya Usalama wa Taifa, umewapa 'Kinga ya Jinai' Maafisa Usalama
Serikali ya Rais Samia imepeleka muswada wa mabadiliko ya sheria ya usalama wa taifa - TISS ambao kwa ujumla wake una mapungufu mengi ikiwemo kuwapa kinga ya makosa ya jinai kwa maafisa wa idara hiyo. Jambo hili limezua mijadala maeneo tofauti watu wakiuliza Rais Samia anataka kuwatumia maafisa hao kufanya jinai gani kiasi kwamba analazimika kuwatungia sheria ya kuwalinda na jinai watakazofanya?

Ukiachilia mbali maafisa wa TISS kupewa kinga ya kijinai pia muswada huo unapendekeza kuwemo manaibu wakurugenzi wakuu wawili wa usalama wa taifa - TISS upande wa Zanzibar na Bara au Tanganyika. Katika mapendekezo hayo vigezo vya naibu mkurugenzi mkuu wa Zanzibar lazima awe Mzanzibar wakati huo upande wa naibu mkurugenzi mkuu Bara hakuna kigezo cha Uzanzibari au Utanganyika, yani anaweza kuwa yeyote.

Mambo mengine ni kwamba katika muswada huo Idara hiyo ya usalama wa taifa - TISS imeondolewa usimamizi wake chini ya waziri na kupelekwa kwa Rais moja kwa moja. Yani muswada huo ukipitishwa ni kwamba idara ya usalama wa taifa - TISS itapewa mamlaka makubwa ambayo sio waziri wa bunge ambalo linaweza kuhoji au kuwawajibisha kwa makosa yoyote yakiwemo utekaji na mauwaji ya raia au viongozi ndani na nje ya nchi. Kwamba kwa sheria hiyo TISS wanaweza kumuuwa waziri mkuu, mbunge ,viongozi wa upinzani etc na wakasingizia kuwa wamefanya mauwaji hayo kwa sababu ya usalama wa taifa.

Fikiria mashirika makubwa ya kijasusi duniani ikiwemo CIA ya Marekani, M16 ya Uingereza na mengineyo yanawajibika kwa bunge na wakurugenzi wakuu wa mashirika hayo lazima wafanyiwe vetting na bunge. Kwamba wakati nchi zingine zikipambana kuimalisha mashirika yao ya kijasusi kwa ajili ya kulinda uchumi wa taifa, pesa za umma na usalama wa raia na mipaka sisi idara yetu ya ujasusi ndio inazidi kudidimizwa kwa kutungiwa sheria ambazo haziisaidii taifa kwa usalama wa uchumi, pesa na mali za umma n.k.

Nilitegemea kwamba Rais Samia angeboresha idara hiyo ya usalama wa taifa - TISS kimafunzo na sheria ili imsaidie kukabiliana na usalama wa uchumi, kudhibiti ufisadi na wizi kama ilivyo hapo jirani Rwanda na baadhi ya nchi zingine ambazo idara za usalama zinafanya vema katika eneo hilo. Matokeo yake yamekuwa kinyume na kwamba idara hiyo ambayo ni maarufu kwa jina la wasiojulikana inaenda kupewa nguvu za kisheria kufanya chochote kwa mtu au kiongozi yeyote katika jamii.

Pengine Rais Samia hajui madhara ya sheria hii au anajua ila anataka kuitumia kuwadhibiti wapinzani wake ndani ya chama na nje ya chama kwa kisingizio cha usalama wa taifa.

Huko miaka ya nyuma Rais wa Argentina Cristina Fernández de Kirchner alitunga sheria ya namna hiyo kwa ajili ya kujilinda yeye na madaraka yake. Idara ya usalama wa taifa katika nchi hiyo ilipewa nguvu za kufanya chochote bila kuhojiwa wala kuwajibishwa na yeyote kama ambavyo muswada huu unavyotaka kuwapa nguvu TISS. Kwamba watu walitekwa na kuuliwa na idara hiyo wakiwemo wanahabari na wapinzani wa serikali tangu miaka ya 1990+

Baada ya mauwaji na utekaji huo kukithiri tarehe 18 January 2015 bunge la Argentina lilitakiwa kupokea ripoti ya mpelelezi binafsi Bw. Alberto Nisman aliyefanya kazi ya kupeleleza vifo tata, utekaji na ufisadi uliokuwa unaikumba nchi hiyo. Lakini kabla ya mpelelezi huyo kufika mbele ya bunge aliuwawa na idara hiyo ya usalama wa taifa kwa kisingizio kile kile cha usalama wa taifa. Kwamba nchi imeibiwa na kufisadiwa watu wanataka kufichua wezi wa taifa wanauliwa kwa kisingizio cha usalama wa taifa.

Baada ya kifo cha mpelelezi huyo bunge liliamua kumwita mkurugenzi wa mkuu mstaafu wa shirika hilo la kijasusi ili ahojiwe na kamati ya usalama ya bunge na aweze kuwapa mwongozo namna ya idara hiyo ya upelelezi inavyofanya kazi. Wakati huo hata Rais wa nchi hiyo alikuwa akitafuta namna ya kuifuta idara hiyo ya usalama ambayo kwa wakati huo ilikuwa imeota mizizi mikubwa na inamwaribia mpaka uongozi wake kwa umma.

Siku moja kabla ya mkurugenzi mkuu huyo mstaafu wa idara ya usalama kufika mbele ya bunge la Argentina alitekwa na idara ya usalama wa nchi hiyo na kufichwa kusikojulikana. Bunge la Argentina likaona huo ni upumbafu na kwamba hiyo haikuwa idara ya usalama wa nchi tena bali lilikuwa genge la wezi walioiba pesa na mali za umma na kutesa raia, wanahabari pamoja na wapinzani. Hivyo bunge hilo likafanya maazimio na kufuta idara hiyo.

Sheria ya namna hii ilitumika katika utawala wa madikteta wengi hapa Africa kutesa wapinzani na kuiba mali na pesa za umma. Idd Amin alitumia sheria hii kutesa na kuuwa wapinzani wake, Hastings Kamuzu Banda aliitumia sheria kuwateka na kuuwa mawaziri wake na wabunge. Mobutu alitumia sheria hii kuwauwa Waziri Mkuu Evariste Kimba, Jerome Anany -Waziri wa Ulinzi, Emmanuel Bamba - Waziri wa Fedha na Alexandre Mahamba - Waziri wa Nishati na Madini kwa madai kuwa usalama wa taifa waligundua viongozi hao walikuwa hatari kwa taifa.

Idara ya usalama ya taifa ya Zaire au Congo wakati wa Mobutu mwaka 1968 lilimkamata Pierre Mulele aliyekuwa rafiki mkubwa wa waziri mkuu wa kwanza na mpigania uhuru wa nchi hiyo Patrice Lumumba. Mulele ambaye alikuwaga waziri wa elimu wakati wa serikali ya Lumumba alikamatwa na kupelekwa kwenye black site za usalama wa taifa na kuanza kukatwa kidole kimoja badala ya kingine, mguu mmoja badala ya mwingine mpaka alipopoteza maisha akiwa kwenye mateso makali.

Sasa leo ndio Samia anaturudisha na sheria hizi ambazo madikteta walizitumia kujilimbikizia mali huku wakitesa na kuuwa wapinzani wao. Fikiria sheria za gizani namna hii zinaletwa karne ya 21 ambayo tunafikiria kuwa na katiba mpya yenye mambo mapya pamoja na kuboresha idara ya usalama wa taifa kwa maslahi ya taifa na sio kwa maslahi binafsi ya viongozi.

Kataeni sheria hii ya Samia ni hatari na haifai kwa nchi hii kwa hapa ilipofikia.

Mdude Nyagali 7 x 70 Sumu ya Nyigu.View attachment 2640691
Acha wafu wazike wafu wenzao.

Sent from my SM-G970U using JamiiForums mobile app
 
Serikali ya Rais Samia imepeleka muswada wa mabadiliko ya sheria ya usalama wa taifa - TISS ambao kwa ujumla wake una mapungufu mengi ikiwemo kuwapa kinga ya makosa ya jinai kwa maafisa wa idara hiyo. Jambo hili limezua mijadala maeneo tofauti watu wakiuliza Rais Samia anataka kuwatumia maafisa hao kufanya jinai gani kiasi kwamba analazimika kuwatungia sheria ya kuwalinda na jinai watakazofanya
Nadhani majibu yako wazi kwa hiki kinachoendelea sasa. Nilitamani katika hiyo sheria tuweze kujua "afisa usalama" ameelezwa kama nani. Wasiwasi wangu ni kwamba kama polisi nao wamehisishwa katika kundi hili basi tuko katika kipindi kigumu zaidi. Huwa najiuliza maswali kuhusu ile kauli "tuviache vyombo vya ulinzi na usalama vifanye kazi" huwa ni vyombo gani hasa huwa vinaachwa vifanye kazi yake.
 
Kutokana na hali mbaya kabisa ya kiusalama iliyopo hapa nchini hivi sasa, kuna kila sababu ya ku-declare the State of Emergency.

Siyo siri, hali ni mbaya sana.
Uhakika wa kufa leo hii ni mkubwa zaidi kuliko matumaini ya uwezekano wa kuiona kesho.
 
Serikali ya Rais Samia imepeleka muswada wa mabadiliko ya sheria ya usalama wa taifa - TISS ambao kwa ujumla wake una mapungufu mengi ikiwemo kuwapa kinga ya makosa ya jinai kwa maafisa wa idara hiyo. Jambo hili limezua mijadala maeneo tofauti watu wakiuliza Rais Samia anataka kuwatumia maafisa hao kufanya jinai gani kiasi kwamba analazimika kuwatungia sheria ya kuwalinda na jinai watakazofanya?

Ukiachilia mbali maafisa wa TISS kupewa kinga ya kijinai pia muswada huo unapendekeza kuwemo manaibu wakurugenzi wakuu wawili wa usalama wa taifa - TISS upande wa Zanzibar na Bara au Tanganyika. Katika mapendekezo hayo vigezo vya naibu mkurugenzi mkuu wa Zanzibar lazima awe Mzanzibar wakati huo upande wa naibu mkurugenzi mkuu Bara hakuna kigezo cha Uzanzibari au Utanganyika, yani anaweza kuwa yeyote.

Mambo mengine ni kwamba katika muswada huo Idara hiyo ya usalama wa taifa - TISS imeondolewa usimamizi wake chini ya waziri na kupelekwa kwa Rais moja kwa moja. Yani muswada huo ukipitishwa ni kwamba idara ya usalama wa taifa - TISS itapewa mamlaka makubwa ambayo sio waziri wa bunge ambalo linaweza kuhoji au kuwawajibisha kwa makosa yoyote yakiwemo utekaji na mauwaji ya raia au viongozi ndani na nje ya nchi. Kwamba kwa sheria hiyo TISS wanaweza kumuuwa waziri mkuu, mbunge ,viongozi wa upinzani etc na wakasingizia kuwa wamefanya mauwaji hayo kwa sababu ya usalama wa taifa.

Fikiria mashirika makubwa ya kijasusi duniani ikiwemo CIA ya Marekani, M16 ya Uingereza na mengineyo yanawajibika kwa bunge na wakurugenzi wakuu wa mashirika hayo lazima wafanyiwe vetting na bunge. Kwamba wakati nchi zingine zikipambana kuimalisha mashirika yao ya kijasusi kwa ajili ya kulinda uchumi wa taifa, pesa za umma na usalama wa raia na mipaka sisi idara yetu ya ujasusi ndio inazidi kudidimizwa kwa kutungiwa sheria ambazo haziisaidii taifa kwa usalama wa uchumi, pesa na mali za umma n.k.

Nilitegemea kwamba Rais Samia angeboresha idara hiyo ya usalama wa taifa - TISS kimafunzo na sheria ili imsaidie kukabiliana na usalama wa uchumi, kudhibiti ufisadi na wizi kama ilivyo hapo jirani Rwanda na baadhi ya nchi zingine ambazo idara za usalama zinafanya vema katika eneo hilo. Matokeo yake yamekuwa kinyume na kwamba idara hiyo ambayo ni maarufu kwa jina la wasiojulikana inaenda kupewa nguvu za kisheria kufanya chochote kwa mtu au kiongozi yeyote katika jamii.

Pengine Rais Samia hajui madhara ya sheria hii au anajua ila anataka kuitumia kuwadhibiti wapinzani wake ndani ya chama na nje ya chama kwa kisingizio cha usalama wa taifa.

Huko miaka ya nyuma Rais wa Argentina Cristina Fernández de Kirchner alitunga sheria ya namna hiyo kwa ajili ya kujilinda yeye na madaraka yake. Idara ya usalama wa taifa katika nchi hiyo ilipewa nguvu za kufanya chochote bila kuhojiwa wala kuwajibishwa na yeyote kama ambavyo muswada huu unavyotaka kuwapa nguvu TISS. Kwamba watu walitekwa na kuuliwa na idara hiyo wakiwemo wanahabari na wapinzani wa serikali tangu miaka ya 1990+

Baada ya mauwaji na utekaji huo kukithiri tarehe 18 January 2015 bunge la Argentina lilitakiwa kupokea ripoti ya mpelelezi binafsi Bw. Alberto Nisman aliyefanya kazi ya kupeleleza vifo tata, utekaji na ufisadi uliokuwa unaikumba nchi hiyo. Lakini kabla ya mpelelezi huyo kufika mbele ya bunge aliuwawa na idara hiyo ya usalama wa taifa kwa kisingizio kile kile cha usalama wa taifa. Kwamba nchi imeibiwa na kufisadiwa watu wanataka kufichua wezi wa taifa wanauliwa kwa kisingizio cha usalama wa taifa.

Baada ya kifo cha mpelelezi huyo bunge liliamua kumwita mkurugenzi wa mkuu mstaafu wa shirika hilo la kijasusi ili ahojiwe na kamati ya usalama ya bunge na aweze kuwapa mwongozo namna ya idara hiyo ya upelelezi inavyofanya kazi. Wakati huo hata Rais wa nchi hiyo alikuwa akitafuta namna ya kuifuta idara hiyo ya usalama ambayo kwa wakati huo ilikuwa imeota mizizi mikubwa na inamwaribia mpaka uongozi wake kwa umma.

Siku moja kabla ya mkurugenzi mkuu huyo mstaafu wa idara ya usalama kufika mbele ya bunge la Argentina alitekwa na idara ya usalama wa nchi hiyo na kufichwa kusikojulikana. Bunge la Argentina likaona huo ni upumbafu na kwamba hiyo haikuwa idara ya usalama wa nchi tena bali lilikuwa genge la wezi walioiba pesa na mali za umma na kutesa raia, wanahabari pamoja na wapinzani. Hivyo bunge hilo likafanya maazimio na kufuta idara hiyo.

Sheria ya namna hii ilitumika katika utawala wa madikteta wengi hapa Africa kutesa wapinzani na kuiba mali na pesa za umma. Idd Amin alitumia sheria hii kutesa na kuuwa wapinzani wake, Hastings Kamuzu Banda aliitumia sheria kuwateka na kuuwa mawaziri wake na wabunge. Mobutu alitumia sheria hii kuwauwa Waziri Mkuu Evariste Kimba, Jerome Anany -Waziri wa Ulinzi, Emmanuel Bamba - Waziri wa Fedha na Alexandre Mahamba - Waziri wa Nishati na Madini kwa madai kuwa usalama wa taifa waligundua viongozi hao walikuwa hatari kwa taifa.

Idara ya usalama ya taifa ya Zaire au Congo wakati wa Mobutu mwaka 1968 lilimkamata Pierre Mulele aliyekuwa rafiki mkubwa wa waziri mkuu wa kwanza na mpigania uhuru wa nchi hiyo Patrice Lumumba. Mulele ambaye alikuwaga waziri wa elimu wakati wa serikali ya Lumumba alikamatwa na kupelekwa kwenye black site za usalama wa taifa na kuanza kukatwa kidole kimoja badala ya kingine, mguu mmoja badala ya mwingine mpaka alipopoteza maisha akiwa kwenye mateso makali.

Sasa leo ndio Samia anaturudisha na sheria hizi ambazo madikteta walizitumia kujilimbikizia mali huku wakitesa na kuuwa wapinzani wao. Fikiria sheria za gizani namna hii zinaletwa karne ya 21 ambayo tunafikiria kuwa na katiba mpya yenye mambo mapya pamoja na kuboresha idara ya usalama wa taifa kwa maslahi ya taifa na sio kwa maslahi binafsi ya viongozi.

Kataeni sheria hii ya Samia ni hatari na haifai kwa nchi hii kwa hapa ilipofikia.

Mdude Nyagali 7 x 70 Sumu ya Nyigu.View attachment 2640691
Kuna mambo ukiyafikiria unapata uchungu. Nadhani tumelaaniwa kabisa!
 
Matokeo ya Sheria hii sasa tunayaona.

Tunavuna matunda yatokanayo na Sheria hii.
 
Mdude big up! Sasa nimeelewa
Kwa Nini Mzee kibao ametekwa na kuuwawa na tiss watasingizia usama wa taifa

Sheria ya kuwalinda walishaipitisha tayari
 
Nilitegemea kwamba Rais Samia angeboresha idara hiyo ya usalama wa taifa - TISS kimafunzo na sheria ili imsaidie kukabiliana na usalama wa uchumi, kudhibiti ufisadi na wizi kama ilivyo hapo jirani Rwanda na baadhi ya nchi zingine ambazo idara za usalama zinafanya vema katika eneo hilo. Matokeo yake yamekuwa kinyume
Duuh
 
Ukiachilia mbali maafisa wa TISS kupewa kinga ya kijinai pia muswada huo unapendekeza kuwemo manaibu wakurugenzi wakuu wawili wa usalama wa taifa - TISS upande wa Zanzibar na Bara au Tanganyika. Katika mapendekezo hayo vigezo vya naibu mkurugenzi mkuu wa Zanzibar lazima awe Mzanzibar wakati huo upande wa naibu mkurugenzi mkuu Bara hakuna kigezo cha Uzanzibari au Utanganyika, yani anaweza kuwa yeyote.
Ule mswaada sikuusoma kumbe ulikuwa na mambo mazito sana namna hii?
Huwa nawambia watu Zanzibar sio Nchi ya kuchezea. Wana mbinu sana kuanzia kwenye Muungano namna Nyerere alidhani amewakamata kumbe alikamatika.
 
Siku moja kabla ya mkurugenzi mkuu huyo mstaafu wa idara ya usalama kufika mbele ya bunge la Argentina alitekwa na idara ya usalama wa nchi hiyo na kufichwa kusikojulikana. Bunge la Argentina likaona huo ni upumbafu na kwamba hiyo haikuwa idara ya usalama wa nchi tena bali lilikuwa genge la wezi walioiba pesa na mali za umma na kutesa raia, wanahabari pamoja na wapinzani. Hivyo bunge hilo likafanya maazimio na kufuta idara hiyo.
Smelling fishy
 
Sheria ya namna hii ilitumika katika utawala wa madikteta wengi hapa Africa kutesa wapinzani na kuiba mali na pesa za umma. Idd Amin alitumia sheria hii kutesa na kuuwa wapinzani wake, Hastings Kamuzu Banda aliitumia sheria kuwateka na kuuwa mawaziri wake na wabunge. Mobutu alitumia sheria hii kuwauwa Waziri Mkuu Evariste Kimba, Jerome Anany -Waziri wa Ulinzi, Emmanuel Bamba - Waziri wa Fedha na Alexandre Mahamba - Waziri wa Nishati na Madini kwa madai kuwa usalama wa taifa waligundua viongozi hao walikuwa hatari kwa taifa.
Huu uzi ni mzito sana
 
Hiyo sheria itapita kama zilivyopita nyingine, kwa bunge hili la majizi ya kura. Hapo wasiojulikana wanaenda kuhalalishwa rasmi. Sheria za aina hii ndio hupelekea mabadiliko kwenye nchi kwa njia ya machafuko, ama serikali kupinduliwa. Lakini kabla ya hayo watu watakuwa wameumizwa na kupotezwa vya kutosha.
Hili nililiona mapema sana. Na sasa utekelezaji wa sheria hii upo kazini.
Tlaatlaah Lucas Mwashambwa ChoiceVariable
 
Mimi nakubaliana na hao kufanyiwa vetting, na kuwe na control za wao hao wakikosa integrity...

Power balance ni muhimu lakini ule upuuzi eti wa hao ndugu zetu kuwa wapendwa watazamaji tu na kushauri mtu ambaye halazimiki kutumia ushauri, hiyo iondoke haraka sana...

Raia wa kawaida hawana shida hata siku moja, ila wale wenye madaraka na access to our hazina kuna shida, wanahitaji udhibiti wa hawa wasiojulikana.
Umeoona sheria uliyokuwa unaipigia debe inavyofanya kazi?
 
Tatizo unapeleka mawazo kwenye siasa tu...
Umeona nini kinaendelea? Ni kipofu tu asingeweza kuona lengo la ile sheria mbaya. Ww ni mmojawapo wa vipofu hao, na si ajabu unafaidika na huu utekaji na haya mauaji.
 
Mama anawalinda wenzake wa zamani.

Kina bashite wameanza kulindwa kifaulo faulo kabla ya hiyo sheria.

Sasa ndiyo tutegemee vimungu watu.

Sheria mbaya kabisa hii.
Naam.
 
Hiyo sheria itapita kama zilivyopita nyingine, kwa bunge hili la majizi ya kura. Hapo wasiojulikana wanaenda kuhalalishwa rasmi. Sheria za aina hii ndio hupelekea mabadiliko kwenye nchi kwa njia ya machafuko, ama serikali kupinduliwa. Lakini kabla ya hayo watu watakuwa wameumizwa na kupotezwa vya kutosha.
Nguruvi3 Paskali mayalla
 
Back
Top Bottom