Bana likasi
JF-Expert Member
- Jan 7, 2020
- 6,926
- 6,422
Viongozi wa hivo vyombo, viongozi wa dini, wastaafu,TISS Hawa ni wanufaika hivo usitegemee waangalie maslai ya nchi waache yao.Maana wanajua Kama akiingia mwingine uenda hawatoweza kunufaika hivo ni lzm wayalinde maslai yao ya Sasa.Ni Hadi pale mirija yao ikikatwa.Sioni hao viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama wakifanya wajibu wao, maana wao ni sehemu ya huu ukandamizaji na uvunjwaji mkubwa wa katiba. Nadhani kuna malipo fulani wanapata ya upendeleo, hivyo hawana uhakika huyu anayewapa sasa, kama akija mwingine watapata upendeleo binafsi. Na ukifuatilia kwa ukaribu sana utaona viongozi wa hivyo vyombo vya dola ni watii kwa rais kama mtu, na sio rais kwa muongozo wa katiba. Ndio maana chaguzi za nchi hizi zinaharibiwa, wapinzani wa chama cha rais wanafanyiwa ukatili wa wazi, lakini vyombo vya usalama ndio wanakuwa wakwanza kuficha ukatili huo.
Hapa tulipofikia bila kuingia mabarabarani kwa amani sioni nchi yetu kutokuangukia kwenye mauaji ya kutisha. Kuna ghiliba inachezwa kuwa kiongozi huyu ni mcha Mungu kwa kuwaweka viongozi wa dini mbele kwenye shughuli za kitaifa, lakini lengo ni kufunika unyama uliopo na unaopangwa kufanywa. Kama kweli kiongozi huyu ni mcha Mungu, na anafanya mambo mema, ni kipi kinafanya ajiwekee kinga za kibinadamu na sio hizo kinga za Mungu?
Duniani kote dikteta sio tatizo tatizo ni wapambe wanufaika backup hawa ndio umtia ndimu dikteta asiachie sababu wanajua bila yeye ni lzm watakufa njaa.Wenzetu weupe wao ndio wenye hulka za kujali maslai ya Jamii na sio ya kikundi cha wanufaika.