Bana likasi
JF-Expert Member
- Jan 7, 2020
- 6,926
- 6,422
Nia yao si nzuri Wana nia ya kuumiza watu thus wanajiwekea Kinga.Sisi tunashtakiwa wao kwann wasistakiwe
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwa akili hizi safari ya tz kurudi misri ipo pale pale amna wakutupeleka nchi ya ahadi hapa!Rais magufuri ni rais bora na mtumishi mwaminifu kuwa tumikia watu na wanademocrasia bora afrika na duniani. Ni rais anaye waokoa na kuwa jari watu kipato cha chini. imeonyesha haki,usawa na democrasia ya kweli katika vita corona,hajamfungia hata mtu mmoja afe na njaa
Toka kwa shemeji kajitegemee upate akiliRais magufuri ni rais bora na mtumishi mwaminifu kuwa tumikia watu na wanademocrasia bora afrika na duniani. Ni rais anaye waokoa na kuwa jari watu kipato cha chini. imeonyesha haki,usawa na democrasia ya kweli katika vita corona,hajamfungia hata mtu mmoja afe na njaa
Hii ishu ni very simple! Ukichukua madaraka una SUSPEND katiba unawashitaki.Viongozi hawa wakuu wa nchi wanapoingia madarakani wanaapa kulinda katiba ya nchi. Sasa endapo watakiuka na kuvunja katiba kwa namna yo yote ile wanapaswa kuwajibika au kuwajibishwa.
Kitendo cho chote cha kuwalinda kwa uvunjifu wa katiba ni uhaini. Muswada huu wa kuwalinda viongozi hawa kwa kuvunja katiba ya nchi ni kuhalalisha uhaini, jambo ambalo hakikubaliki. Haiwezekani kabisa Rais aape kulinda katiba halafu aivunje kwa sababu yo yote ile aachwe bila kuchukuliwa hatua za kisheria.
Tanzania tutakuwa nchi ya ajabu duniani inayoamini katika demokrasia kuwa na sheria ya namna hii. Kwa namna nyingine tutakuwa tunaiambia dunia kuwa Rais wetu ndiyo katiba yetu na kwamba Rais anaweza kuichezea katiba yetu kwa kadri anavyotaka.
Wito kwa wote wapenda haki nchini kupinga muswada huu kwa nguvu zote.
Atafika mwisho mbaya sana.Hili ni jambo la kuogofya sana linaelekea kutokea nchini, serikali imepeeleka mswada bungeni ili kumuongezea kinga rais na viongozi wengine wa bunge na mahakama kinga dhidi ya kushatakiwa moja kwa moja kwa kukiuka katiba ya nchi.
Huu ni mswada wa ajabu na wa kuogofya sana, mtu aliyeapa kuilinda na kuitetea katiba ya nchi inakuwaje leo anatafuta uhuru wa kuivunja katiba hiyohiyo?
Inakuaje marais wengine wote waliotangulia hawakuona kikwazo chochote kwenye kufuata katiba lakini huyu wa sasa kwake yeye katiba imekua kero kwake?
Ni nini hatma ya nchi yetu ikiwa tutaruhusu ujinga wa namna hii kuendelea kutokea? Unajua hata Adolf Hitler aliingia madarakani kwa njia halali kabisa, lakini taratibu akaanza kujiongezea mamlaka na kuwanyamazisha wote aliowaona kuwa kikwazo. Mwisho wake sote tunajua kilichotokea. Binadamu wote ni corrupt kwa viwango tofauti tofauti, hauwezi kumpa binadamu mwezako mamlaka yasiyo na mipaka, mwisho wake ni mbaya tu.
Wito wangu kwa wote mlioapa kuilinda na kuitetea katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania, wakati wenu ni sasa kufanya hivyo, the republic as we know it is under attack.
Ni kweli kabisa, bila kuwa na namna ya kumwajibisha kiongozi wa kiafrika basi ujue unafungua milango ya ukandamizaji mkubwa wa haki za watu na ubadhirifu wa mali za umma.Unampa Kinga mtawala wa kiafrica halafu unataka maendeleo ukapimwe akili, waafrika sisi tuendelee tu kuwa masikini ndo tunachodisevu
Hili taifa letu huko mbeleni isipotokea civil war , me nipo labda Magu abadili mambo yakeEti ndio wanamuabudu na kumwimbia mapambio, mzarendo huyo
Siku nyingi ilisemwa mkajizunguusha kuwa hayo madaraka ya rais ni makubwa sana ipo siku atatokea rais kichaa atalitumia vizuri hilo gap hamkujali 🤣🤣🤣Asasi za Kiraia 220 zimefanya uchambuzi wa muswada huo wa sheria na kuwasilisha mapendekezo ya mabadiliko ya muswada huo kwa Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria. Taasisi hizo zimeeleza kuwa japo kuwa zinafahamu muswada huo una lengo wa kusasisha Sheria iliyopo sana huku ikibaki kuendana na Katiba, ni mambo machache sana yanaenda na Katiba ya Tanzania ya Mwaka 1977
Asasi hizo zimesema wakati mambo machache yaliyopendekwa kwenye muswada huo yanaendana na Katiba au yanaifafanua Katiba vema, mambo mengi kwenye muswada huo yanakengeuka na kwenda kinyume na Katiba
Baadhi ya mambo yanayoenda Kinyume na Katiba ni;
1. Kifungu cha 7(b)(2) na 7(b)(3) of Written Laws (Miscellaneous Amendments) (No.3) 2020Mapendekezo ya mabadiliko ya sheria yanaruhusu wale tu walioathiriwa moja kwa moja na uvunjifu fulani wa haki kufungua mashitaka ya kudai haki zao. Mabadiliko haya yakipitishwa yatazuia raia wengine kufungua mashtaka kwa maslahi ya umma wanapohisi kuna uvunjifu wa Katiba.Kwa maana nyingine, hutaruhisiwa kumtetea raia mwenzako hata kama hana uwezo wa kujitetea, hutaruhisiwa kutetea nchi yako kupitia Mahakama isipokuwa pale tu unapokuwa umenyanyaswa moja kwa moja, na hutaweza kutoa mchango wako kuilinda Katiba yetu. Hii inaondoa uzalendo.>>> Mapendekezo hayo yakiwa hivyo, Ibara 26 ya Katiba inampa kila raia jukumu na uhuru wa kuilinda Katiba yetu kupitia Mahakama ya nchi.Athari kwenye maisha ya kila siku: Kwenye maisha ya kila siku tulio wengi tunakutana na changamoto za hapa na pale. Kuna mifumo tofauti kutusaidia kukabiliana na hizi changamoto ikiwemo, kwa matatizo makubwa na magumu, mifumo ya Mahakama.Kutoruhusu mtu au taasisi kufungua mashtaka bila kuathirika moja kwa moja inakulazimisha kujitegemea na kujitetea unapokutwa na unyimwaji wa haki zako unaohitaji Mahakama kuingilia.Kuna watu wengi ambao wamesaidiwa kudai haki zao na mashirika tofauti ambao wanawasaidia kwa utalaamu, rasilimali na mikakati na kusimamia kwa ujumla mashtaka yao. Mabadiliko haya yatawaathiri sana wasiokuwa na uwezo na ujasiri wa kujisimamia wenyewe kisheria kama vile walemavu, watoto, wajane na makundi mengine mengi ya kijamii ambayo yamekuwa yakisaidiwa na watetezi wa haki za binadamu kwa maslahi ya Umma.
2. Kifungu cha 7(b)(4) na 18A na 65A of Written Laws (Miscellaneous Amendments) (No.3) 2020Mabadiliko ya sheria yanaondoa maana ya kuwa Jamhuri na badala yake tunaanza kulekea kwenye utawala usiokuwa wa kisheria kama vile utawala wa kifalme. Kwenye Jamhuri watu wote, wananchi na viongozi, wanaangaliwa sawa kwa jicho la sheria. Ndio tunaoita utawala wa sheria – kila mtu awe mdogo au mkubwa, anawajibika kwa kile alichofanya mwenyewe.Kwa kuwatoa watu fulani kutoka mfumo wa kawaida wa haki, mfumo wa Mahakama, na kufanya hawawezi kuwajibishwa moja kwa moja, hata kama wamekiuka Katiba, inatupeleka kuwa na ngazi mbili za raia, wanaofuata sheria na wasiofuata sheria.Pamoja na haya, misingi ya demokrasia na Jamhuri yetu ni mihimili mitatu ya Serikali, Bunge na Mahakama. Kila mhimili una majukumu yake na haitakiwi kabisa kuingiliana.Mhimili mmoja unawajibisha mwingine kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo na haki. Hii haijalishi nani anashika cheo cha Rais, ni msingi wa Katiba yetu, nchi yetu na sheria zote za nchi.>>> Ibara ya 13 ya Katiba inaeleza usawa mbele ya sheria kwa kila mwananchi na Ibara ya 4 inazungumzia mihimili mitatu ya Serikali na jinsi zinavyotakiwa kushirikiana, kila taasisi kwa uhuru wake.Athari kwenye maisha ya kila siku: Kuna watu wanaopenda kusema demokrasia siyo chakula. Ukweli ni kwamba haki za mfumo wetu wa utawala, zinajulikana kama haki za siasa, hazionekani wazi kwenye maisha ya kila siku kama ilivyo kwa haki nyingine kama za kuishi na kupata chakula.Tunaporuhusu baadhi ya watu kuwa nje ya sheria ambazo sisi wote tunazifuata, tunatengeneza mazingira tatanishi ya kutegemea utashi mtu moja au watu wachache. Wao ndio wataamua utamu na ugumu wa maisha yetu bila sisi kuwa na mchango wowote.Mamlaka ya viongozi wetu wote yanatoka kwa wananchi na kila hatua inayotupeleka mbali na hilo, inazidi kupunguza uwezo wetu wa kuamua mwelekeo ya maisha zetu.
3. Kifungu cha 7(b)(2) na 7(b)(3) na 18A na 65A of Written Laws (Miscellaneous Amendments) (No.3) 2020Haya mabadiliko ya sheria yanawapa kundi la watu Mamlaka juu ya sheria na yanapunguza uwezo wa baadhi ya watu kudai haki nchini. Kwa sababu Mahakama ni sehemu ya mwisho kupeleka kilio chako ukinyimwa haki, hii ni sawa na kutomruhusu mtoto kulia unapompiga.Tunahitaji kutoa dukuduku letu na kuamini kwamba tunapokanyagwa na mtu yoyote, tutafidiwa. Utawala wa sheria unategemea imani yetu katika mifumo ya sheria. Mifumo yetu ya sheria ikianza kuleta ubaguzi kuanzia kwenye sheria zenyewe ndio tunaelekea kuuua mfumo yenyewe.>>> Ibara 26 ya Katiba inampa kila raia jukumu na uhuru wa kuilinda Katiba yetu kupitia Mahakama ya nchiAthari kwenye maisha ya kila siku: Tunapofunga milango ya mfumo wa haki nchini ndio walalahoi wanakosa njia muhimu ya kufidiwa. Watu maarufu na wenye mahusiano na vigogo na wanasiasa wanaweza kuwa na njia tofauti lakini wananchi wa kawaida wanategemea mfumo wa Mahakama wanapodai haki zao. Wapi tupeleke kilio chetu haki zetu zikikiukwa?
Je, una maoni gani kuhusu muswada huu unaotarajiwa kupitishwa Bungeni hivi karibuni?
Pia, unaweza kusoma: Muswada wa Rais, Spika, Waziri Mkuu kutoshitakiwa unapangiwa siku mbili Juni 5&6 tena kwa hati ya dharura
Kusoma zaidi uchambuzi wa Vifungu vinavyokiuka Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tafadhali tembelea PDF hii
Kina ndiyoooooooo mna matatizo sana.Mtoa maada unamulaumu nani CCM,RAIS,MAGUFULI, WANANCHI,SELIKALI,. Unalalamika nini, kitu gani mswaada gani. Sikuelewe. Muache rais wetu nani aliyemchagua, .awe mfalme ivi mfalme anachaguliwa kura za wananchi, acha ku mambo yako
Kutegemea maombi ni kukwepa uwajibikaji. Wananchi wana wajibu wa kuikataa serikali kandamiziKwakweli taifa hili linahitaji maombi.
Tanzania inaongozwa na watu wa, ajabu sana,wanaogopa nini kama wao ni wasafi ,kunadhambi kubwa inaenda kufanyika,eti spika awe juu ya katiba
Una uhakika gani kama atakubali kuachia kiti hio 2026 ?Jiwe hata afanyeje 2026 lazima ashighulikiwe kwa maovu yote aliyofanya hata Kama rais mpya atatoka ccm
We jamaa hivi unachochangia kinaendana na mada? Unalazimisha kutetea hata kama hauna points?Je ni sahihi ku lockdown wasitoke nje nchi kitropical za joto?. Kwanini uige njia zinazotumiwa na taifa baridi US na Ulaya zenye baridi. Unafungia watu tena bila chakula,.wew unajifungi na wademu na vyakula. Lakn Rais wetu mpendwa hakufanya ivi,ndio maana rais shujaa wa haki na demokrasia
hawezi kuzidisha hata siku tatu muda wake ukiisha ccm kuna walevi wa madaraka watamgeuzia kibao hata yeye hatoamini na hilo analitambua fikaUna uhakika gani kama atakubali kuachia kiti hio 2026 ?
So we decided to be caward??Unataka ukatwe jina? Just pray
Walevi wa madaraka hawana uwezo wa kumfanya chochote rais aliye madarakani labda waingie msituni kutumia mbinu mbadalahawezi kuzidisha hata siku tatu muda wake ukiisha ccm kuna walevi wa madaraka watamgeuzia kibao hata yeye hatoamini na hilo analitambua fika