Muungano: Maalim Seif aipa tume ya jaji Warioba masharti


Saluti mkuu!
 

Nakubaliana na wewe lakini tusisahau pamoja na kuwa Watanganyika wako kimya sana na Muungano haimaanishi kuwa wanakosa maamuzi, ni kama vile mtu anawaza 'hivi nikijishughulisha na kuvunja muungano napata nini?". Wengi wana Tanganyika (kwa maoni yangu) wanaona sarakasi za Wazanzibari kwa mashangao au wakati mwingine kwa daharau ingawa wapo Wazanzibari wanawaona akina Maalim Seif kama mashujaa.

Hebu angalia hiki kichekesho; Wazanzibari wapinga Muungano mara ya kwanza walikuwa wanataka serikali tatu (hata CUF Msimamo wao ulikuwa hivyohivyo), baada ya muda wakataka Mkataba (hata kuuelezea walikuwa wanapata shida), na tena mpaka "miungu wao" wanaowaamini akina Ahmed Rajabu haya yalikuwa maoni yao. Ghafla baada ya maswali magumu kuhusu huo mkataba wanaoutaka wakakaa kimya.

Sasa hivi kinara wao Maalim Seif anataka Muungano wa "Jamhuri za Tanzania", tena kuwepo na passport zao na mambo yao ya Ulinzi na Mambo ya nje - kichekesho cha karne.

Wanajua vizuri sana kuwa hayo ni lazima wayapate nje ya Muungano, na dawa yake ni kuuvunja. Hwataki kuvunja lakini wanataka Muungano!!

Hawa ni kupe tu, na huo ukupe ndiyo unawafanya mara sitaki nataka. Na usishangae ikaja single nyingine tena!!
Mark my word: Nyerere pamoja na dosari zoote hakukosea; hawa ni wanajiona wamoja kwa sababu ya Tanganyika, nje ya Tanganyika wanachukiana vibaya sana - nawafahamu.

Lets Zanzibar go, hatutaki "Jamhuri za Tanzania"........Ondokeni kuanzia Dodoma Bungeni, Ofisi ya Makamu wa Rais na acheni fadhila zoote mnazopata............Maana naona mke mwenyewe analishwa lakini kutwa kiguu na njia kulalama.
 

Mkuu hayo yote yanatokana na tanganyika haipo,idaini kwanza tanganyika muone kama wazenj wataingia,huoni kule baraza la wakilishi mtanganyika hatii mguu?
 
Last edited by a moderator:
Mkataba wa nini?hebu niambie wewe unaona mimi kama mtanganyika nafaidika vipi na uwepo wa Zanzibar kama sehemu ya Muungano?hakuna sababu ya mkataba,daini nchi yenu na muondoke jumla.

Zanzibar washadai nchi yao je tanganyika mnadai nn?
 
Unawezaje kuwa na nchi mbili, moja ikabaki na serikali yake na nyingine ikafa.....?! Hakuna muungano kama huu dunia nzima....

Some timez unakuaga na akili!
 
Umesahau kumi na tatu; kwanini viongozi wa ki-tanganyika waoga kupita kiasi. au ndio kile tunacho kiamini kuwa wao ndio wanaonufaika na Muungano huu wa kidhalimu.

Sasa ninyi majasiri si mjiondoe kabisa, vunjeni Muungano hata mimi nitakuunga mkono. Ninyi masema tunawanyonya na tunawazibia neema zenu lakini kwa nini hamtaki kutoka na sasa hivi manataka Jamhuri za Tanzania?

Halafu usituite waoga, hivi kuna muoga gani anaweza kumdhulumu mtu jasiri?

Kwa mtazamo wako (na Wazanzibar wenzako).

1. Tunawanyonya rasilimali zenu (kama zipo)
2. Tunawazibia neema zenu
3. Tunawachagulia viongozi nk nk

Sasa hapo nani jasiri!! Anayedhulimiwa ama anayedhulumu?
 
Reactions: ral
Mkuu hayo yote yanatokana na tanganyika haipo,idaini kwanza tanganyika muone kama wazenj wataingia,huoni kule baraza la wakilishi mtanganyika hatii mguu?
Serikali tatu itakuwa "pasua kichwa" vilevile!; Kwanza gharama zitakuwa kubwa kwa nchi changa kama hizi, halafu uchangiaji wa gharama za kuendesha serikali ya muungano matatizo yatajitokeza kama vile anayechangia kikubwa katika Muungano ataka naye apate mgao au sauti kubwa, kuna suala la ardhi na mengineyo.

Kuukata mzizi wa fitina ni kuuvunja Muungano tu, kila mtu afe na chake.
 
Zanzibar washadai nchi yao je tanganyika mnadai nn?

Sasa mnamdai nani nchi yenu?kwan hamjui procedure za kudai nchi yenu?tuwakumbushe?kazi ya baraza la wawakilishi ni nini?si muende mahakama ya katiba kudai nchi yenu?mnadai kwenye vijiwe mkuu?mtadai sana kama ndo hivo..kelele nyingi lakini kuchukua hatua hamchukui!poleni zenu,heri sie ambao hatujadai nchi yetu!
 
mchakato wa katiba mpya unaoendelea sasa unazidi kupata vikwazo vingi kiasi cha kuonekana labda wakati wake ulikuwa bado,lakini kutokana na msuguano wa kiuchumi na hali halisi ya dunia ya leo ikaonekana kwamba wakati wa kubadilisha katiba ni sasa.Kwa upande wangu sidhani kama viongozi wa serikali na wale kisiasa ndio wanawajibika kuwasilisha maoni ya watu,mwananchi ndio mwenye kutoa maoni.Viongozi hawa wakijifanya kuwasilisha maoni ya watu wataaribu kila kitu chema walichokianzisha wao wenyewe kwa manufaa ya wote,na hapo itaonesha kuwa hicho walichokianzisha hakikuwa cha watu bali chao wenyewe.Kikubwa wakuu hawa wajitahidi kuwa wavumilivu ili ile tume walioichagua na kuiamini iweze kuleta mwongozo ule wananchi wanautaka (katiba).Hii ikiwa ni pamoja na kutojihusisha na matamko au maelezo ambayo wakati mwingine tayari walikwisha wasilisha kwenye tume,kwani kufanya hivyo ni sawa na kuishinikiza/kuishurutisha tume ifuate kile ambacho wanataka wao na si vinginevyo.K
 
Ukweli ni kwamba viongozi wengi WA Tanganyika hawapendi muungano lakini hawataki historia iwaandike wao kama chanzo cha kufa muungano.Kiukweli hakuna Mtanganyika yeyote anaefaidika na muungano,especially uwepo au kutokuwepo kwa zanzibar kwenye muungano.HAKUNA!
 
ZANZIBAR ni vyema wakasikilizwa na kupewa wakitacho kwakuwa asilimia kubwa hawati muungano, muungano una magumashi makubwa sana na hata upatikanaji wake ulikuwa wa kimagumashi. Ni muungano gani ambao hata mkataba wake hauonekani?
 
Mkuu hayo yote yanatokana na tanganyika haipo,idaini kwanza tanganyika muone kama wazenj wataingia,huoni kule baraza la wakilishi mtanganyika hatii mguu?

Kama tanganyika haipo sasa nyie mwadai uhuru kutoka wapi?je waweza kudai uhuru kutoka kwenye nchi yako mwenyewe(maana ndicho mnachofanya)and its treason mnachokifanya!
 
Sijaona neno ambalo nitalipinga katika bandiko lako hili. Hawa jamaa kama nilivyosema, kigugumizi chao katika matamko na kwenye majukwaa ya kisiasa zinadhihirisha kabisa hawana hata tone la political will kujitoa kwenye muungano.

Wanajificha kwenye katiba ya nchi kama kujitoa ni kosa ya uhaini ili kuficha madhaifu yao.

Kama unavyosema, kwa sababu wao siyo wamoja, hata wale wanaotegemea maisha yao kwa kodi za Watanganyika hawawezi kukubali kuachia posho na malupu lupu wanayoyapata. Hata Wabunge, wafanyakazi waandamizi wa serikali, wafanyabiashara, n.k. Hawawezi kukubaliana na mawazo yao.

Kitu ninachokifahamu, hawa jamaa ni weakling na hawawezi kujitoa kwenye muungano lakini nchi yetu itakuwa na serikali tatu.

I can't wait to read rasimu kujua mwelekeo wa taifa letu katika maswala yanayopigiwa kelele sana ambazo zingine mpaka zinakuwa na crocodile tears.
 
Its enough to say Maalim Seif ISN'T NORMAL! Sorry
 
Unafikiri ni njia gani zinaweza kutumika kuwapata hawa viongozi waje hadharani na kuweka msimamo wao?
 

Pendekezeni (au niseme amueni) kujitegemea 100%! Na mkubali pia kulipa mnachodaiwa na Tanganyika na upande huu tuwalipe madai yenu yote yaliyopo ( kama yapo). Then Mzanzibar aliepo Tanganyika aehesabiwe kuwa ni raia wa kigeni
 
Hahahaha alhamdullah leo umekubali na umeelewa nini wanachokitaka wazanzibari ? Mungu awafungue na awangoe hawa walio baki wanaowabeza wazanzibari

Mkataba, jamuhuri zote mezani.
 
Chama sio dini wala msahafu, sio kwamba mtu hawezi kubadili kauli au kuenda kinyume na chama chake, katiba ya sio kitu chochote, kiongozi bora huangalia wafuasi nini wanakitaka, ndipo huunga mkono kwa wafuasi hao ili aweze kukubalika, alicho kifanaya maalim kuwangu mkono wazanzibari ambao wengi wanahoja, ukiangalia leo hii wazanzibari asilimia 66 wanaunga mkono kuwepo kwa mamlaka kamili ya zanzibar na muungano wa mkataba, hivi maalim kama ana stik katika katiba ya chama chake ataungwa mkono ? Ndio maana anaunga hoja ya kuwepo muungano wa mkataba.
 

Kumbe mkuu ile tume ya warioba ni kijiwe?unajiona bora kwa kuto lidai au kulilia taifa lako tanganyika lililo kupatia uhuru?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…