Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sio kazi ya serikali kusimamia Dini na ibada mashuleni Ni upotofuKama ndivyo anavyofanya hiyo mmiliki basi SMZ wapo sahihi kumpiga hiyo ban
Kipimo Cha uzuri wa shule Ni ufaulu wa wanafunzi lkn wenzetu nyie mnaangalia hijab na kiarabu. Kiarabu kitawasadia Nini?Nyinyi watanganyika hemu acheni tabia zenu za kibishi bishi mnavokuja kuweleza huku visiwani. Zanzibar tuna ustaarabu wetu kwaio mkija huku muwe mnakuja na adabu zenu
Hata hoja ya msingi hakuna sana sana ni udini tuWizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, imeifutia usajili Skuli ya Eden inayomilikiwa na Shirika la Afrika Agape Association kuanzia Januri 3 mwakani.
Hatua hiyo imefikiwa baada ya Wizara kubaini mmiliki wa Skuli hiyo kuendesha Skuli kinyume na sheria, miongozo na kanuni za Wizara.
Akizungumza na wamiliki wa Skuli hiyo huko Shakani Kaimu Mrajis wa Elimu na Katibu wa Baraza la Elimu Zuwena Mataka Hafidh, amesema kumekuwepo malalamiko mbalimbali yaliyowasilishwa na wazazi hali iliyopelekea Wizara kuchukua maamuzi hayo.
Ameyataja baadhi ya malalamiko hayo ni pamoja na Wanafunzi wa kislam kutosomeshwa somo la dini ya kislaam na kiarabu, kulazimishwa kujifunza dini ya kikiristo, kutotakiwa kufunga katika mwezi mtukufu wa Ramadhan na Wanafunzi kutoruhusiwa kuvaa hijabu.
Malalamiko mengine amesema kupandishwa ada bila ya utaratibu, kutokuwa na mashirikiano mazuri baina ya wazazi, walimu na mmiliki wa skuli na mmiliki huyo kuendesha skuli kwa hisia zake binafsi.
Aidha amebainisha kuwa malengo ya Wizara sio kuifutia leseni Skuli hiyo bali ni kuhakikisha inafuata sheria na miongozo ya Serikali katika kuendesha Skuli yao.
Kaimu Zuwena, amebainisha kuwa mmiliki wa Skuli hiyo amekuwa mgumu kufuata sheria na miongozo ya Wizara na kuendesha Skuli yake anavyotaka yeye jambo ambalo halivumiliki.
“Haiwezekani Skuli kuendeshwa bila ya kufuata miongozo ya Wizara kwani tuna skuli 590 hatutakuwa tayari kuona mmiliki yoyote wa skuli binafsi anakwenda kinyume na utaratibu na hatutasita kuchukua hatua,” amesisitiza.
Hata hivyo, amesema Skuli hiyo imekuwa ikifatiliwa mara kwa mara na kupewa maagizo ya kurekebisha kasoro hizo lakini haizingatii maagizo anayopewa na badala yake kuendelea kuendesha skuli kinyume na sheria.
Amesisitiza kuwa skuli yoyote ya binafsi inatakiwa kufuata sheria, miongozo na mambo mbalimbali yanayotolewa na wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar.
Nae Afisa Elimu Taaluma Mkoa wa Mjini Magharibi, Amosi John Henock, amesema toka skuli hiyo kusajiliwa mwaka 2010 imekuwa ikijitokeza migogoro baina ya mmiliki na jamii pamoja na kushindwa kujirekebisha baadhi ya kasoro ambazo alitakiwa kuzifanyia kazi.
Aidha amesema Skuli hiyo imeshawahi kufungiwa na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud na kutakiwa kurekebisha kasoro zilizoonekana lakini aliendelea kukaidi.
Amesisitiza kuwa Skuli hiyo haitaendelea kufundisha mpaka pale itakapokubali kwenda sambamba na maagizo ya Serikali katika kuwapatia watoto elimu.
Amesema hata katiba ya Zanzibar imeeleza wazi kwamba mtu yoyote hapaswi kufanya jambo lolote kwa lengo la ubaguzi wa moja kwa moja ama kwa taathira yake.
Kwa upande wake Sheha wa Shehia ya Shakani bi Mwanaisha Khamis Rashid amebainisha kuwa mara nyingi amekuwa akikaa na uongozi wa Skuli hiyo katika uendeshaji elimu kwa kufuata miongozo na mitaala ya Wizara lakini hakuifuata.
Nae mmiliki wa skuli hiyo bwana Youung Am Kim ameahidi kuheshimu maamuzi ya Wizara ya Elimu ya kutofungua Skuli na hiyo na kuwajuillisha wazazi juu ya suala hilo.
Aidha amesema atahakikisha anafuata sheria ya elimu ya Zanzibar na kuondoa changamoto ambazo zinalalamikiwa kupitia Skuli yake.
Akizungumza kwa niaba ya walimu wenzake Mwalimu Ummy Aga amesema wameweka jitihada binafsi kwa wanafunzi wao kuona wanafanya vizuri katika mitihani yao na kujipima katika ufundishaji lakini kufutwa kwa Skuli hiyo imeondosha ndoto yao kwa Wanafunzi wao.
Mimi naona ifike mahali muachiwe mjitegemee wenyewe. Tumechoka makelele yenuIli iwe nchi Inatakiwa iweje
Zanzibar ina
Ardhi
Watu (citizens)
Baraza la mawaziri
Bunge-Baraza la wawakilishi
Mipaka ya kijiografia
Mahakama
Bendera ya Taifa
Wimbo wa Taifa
Huku Tanganyika
Hakuna
Bunge
Rais
Baraza la mawaziri
Shida ya watanganyika wanajitoa ufahamu wakija zanzibar. Katiba iko wazi mtanganyika huku ni mgeni kama wageni wengineWanaosema ni udini nawauliza je munaijua mikataba yao ya uwekezaji hadi waislamu wakaenda shule hiyo?Watanganyika acheni mambo yenu ya ajabu kama mumeshindwa kufuata utaratibu wa uwekezaji na ushauri wa wizara ya elimu na Amal zanzibar hamisheni shule mukaiweke bukoba ,musoma,iringa na kwa wanyamwezi wenzenu musituhangaishe!Shule zanzibar sio hiyo tu zipo nyingi za manaswara lakini zinafuata utaratibu.Ubishi wenu musituletee huku visiwani!
Tumuulize huyu Amosi John HenockKwani wanajitungia wao mtihani wa taifa? Na hao Waislmu wamekosa shule zao mpka waende kwa wanaowaita makqwafir au ndo baniani mbya kiatu chake daawah,
ila watajuana wenyewe
Wapi umeona shule za kiislam zikilazimisha mtu asiekuwa muislam kwenda kusali?mhhh mbona kama issue ya kidini inataka kushika hatamu hapa.
Wale walosoma shule za seminari najua wanajua utaratibu wa shule za namna hiyo, yan pale ni sala asubuhi sala usiku, yan kilamtu lazima ajue BABA YETU sasa huku nako vipiiiii, na wale waosoma shule za kiisilamu lazima wato wafunge ijabu, waingie msikitini kila ijumaa sasa hao vipi kwani?
Kwanini msiwaripoti wanapovunja sheria?Huku ni sheria ngapi wanazivunja na bado hatuwafukuzi?
Hamjachoka bado, mana bado mnaing'anga'niaMimi naona ifike mahali muachiwe mjitegemee wenyewe. Tumechoka makelele yenu
Maneno yenu yanakufarahisheni nafsi zenu huku yanakufanyeni kuonekana wajinga 😀Kinachosumbua hapo ni udini
Sekta ya elimu inatakiwa kuwa huru mfano Tanzania bara ni hiari ya shule kufundisha masomo ya Dini au kuyaacha kabisa.
Za private ziko Muslim schools na Christian schools.
Mtu alienda Muslim schools anakutana na ya kiislamu kibao kuanzia kuvaa hizo hijabu nk akienda Christian schools atasali kikristo nk Na wazazi huridhika
Zanzibar hicho kinafanyika ni kutaka kulazimisha mwenye Shule ageuze shule kwa lazima iwe Muslim school
Zanzibar mbona Muslim schools ziko kibao wazazi wapeleke watoto wao huko huo ni ukorofi usio na sababu mtu kafungua Christian school yake kwa Nini umkomalie kuwa lazima iwe Muslim school.
Hii ichukuliwe kama kero ya muungano.Ichukuliwe wazi kabisa kuwa huyo mwenye shule ananyanyaswa kidini
Raisi Mwinyi aingilie kati Hilo swala haraka
Sio kweli, kuanzia kidato cha nne ndio mitihani inatoka NECTAMitihani yote ya msingy na secondary wanafanya ya NECTA
Hata siye umetuchosha hivyohivyo usifikiri tunaupenda.Tulisema koti likikubana unalivua mkakataa tusilivue!Hawa wanzibar tumewadekeza sana, huu muungano uko one sided ....haiwezekani na haikubaliki
Kuna mengi sana ya kusema juu ya madhira ya huu muungano
Naomba niishie hapa!
Hapo Kama umesikiliza vizuri wenye shule ndio wanaotaka kuleta udini utamlazimishaje kumfundisha mtu masomo ya dini isiyokuwa yake hiyo ni shule ya wanafunzi mchanganyiko mmiliki wa shule aache ubaguziudini tuuuu huo unawasumbua,
Skuli ndio nini?Zanzibar ni sehem nyengine babaa badilikeni zanzibar tuna sheria zetu na taratibu zetu maiforce tanganyika iwe kama zanzibar
Wamiliki wa shule ndio wadini ndio maana wameambiwa wafuate sheriaudini tuuuu huo unawasumbua,