Mvua Kubwa inanyesha Dar tangu usiku wa manane

Mvua Kubwa inanyesha Dar tangu usiku wa manane

Fanyeni kazi ndo kumuenzi Mwalimu, acheni kulialia.
 
Wabongo ni shida! Tena mi naomba siku ya Uchaguzi Vua la Jana lishuke,na NEC hakuna kuhairisha Uchaguzi, mwenye uwezo wa kupiga Kura aendee akapige Kura,nakura zitakozopigwa ndiyo hizohizo zitakazo hesabiwa! Angalia Mziki hata Kura 50 hazitafika!! Alafu eti kuna watu Wanataka kinuke, wakati small Gridlock inawatowa jasho!!

Kura 50 kwani itanyesha nchi nzima? Kumbuka kuna zile kura za mapema.
 




Mvua Kubwa inanyesha Dar tangu usiku wa manane.

Hii mvua itasaidia kupunguza vumbi kwa muda mrefu Jiji hili halikua na mvua.


Basiyaya ni jipu. Napajua vizuri sana, naishukuru mvua kuna jamaa alitaka niuzia kiwanja kipindi fulani, sio kipindi cha mvua ila wiki iliyofuata ghafla Mungu akashusha bonge la mvua ya ghafla! Nikamwambia jamaa naenda cheki kiwanja, Nikaenda, nikakuta nyumba ziko baharini yani mabati ndio yanaonekana. Nikamshukuru Mungu na kuwaonea huruma wakazi wa maeneo hayo kisha nikasepa! Jamaa Hajanitafuta tena..
 
Pole sana mkuu lakini siku nyingine unatakiwa kujiongeza sio kukomaa na Gari. Ungeamua kwenda hapo airport ukapaki na kuondoka na boda kwenda home. Leo ungeenda asubuhi kuchukua gari. Ungelipishwa shs 2000 kwa saa. Ambayo si kubwa ukilinganisha na adha iliyopita barabarani.
Ila airport kituko eti lisaa la kwanza ukipark sh 2000, baada ya hapo ndo buku lisaa

Sasa ndo nini[emoji849][emoji849]
 
Serikli iache ujinga! Waache kujenga madaraja yasiyo na tija kama salenda, jana chanzo kikuu cha foleni ni
1. barabara kuu mbili kufungwa, jangwani na mkwajuni! Yanatakiwa madaraja marefu haya maeneo waache ujinga wa madaraja yasiyo na tija! Maana kwa foleni ya jana hata daraja la salenda lisingesaidia kitu...
2. Traffic kukimbia mvua na magari kuanza kujiongoza. Kila mtu ana haraka matokeo yake barabara za kwenda watu wanakuja na za kuja watu wanaenda...

Jana hadi CDF kakwama kwenye foleni ya bagamoyo road dadeki...piga king'ora weeee hamna gari inampisha ndio kwana zimezimwa utadhani zimepaki...wakajimix wakaingia kati kati, shughuli ikaisha hapo...cdf jana pale moroko fao kasimama karibu saa na zaidi. Tena ana bahati ndio foleni zilikua zinaanza kuachia kwa muda ule
Jana mitrafiki ilikimbia asee[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Wabongo ni shida! Tena mi naomba siku ya Uchaguzi Vua la Jana lishuke,na NEC hakuna kuhairisha Uchaguzi, mwenye uwezo wa kupiga Kura aendee akapige Kura,nakura zitakozopigwa ndiyo hizohizo zitakazo hesabiwa! Angalia Mziki hata Kura 50 hazitafika!! Alafu eti kuna watu Wanataka kinuke, wakati small Gridlock inawatowa jasho!!
Khaaa yaan we na hili neno[emoji849][emoji849][emoji849]

' Gridlock this

' Gridlock that

[emoji848][emoji848][emoji849][emoji849]
 
Hii ya foleni ya Banana majumba sita ni ya hovyo kiwahi kutokea.Naona serikali imeamua kutuachia wenyewe tupambane na hali zetu.Yaan toka saa kumi bado hata mataa ya majumba sita sikafika.wala hakuna dalili kama tutatoka hapa
Duh
Mkuu ulifika saa ngapi?[emoji134]
 
Mkuu wazo lako zuri. Lakini msururu ule wa magari wote tungepata wazo hilo Airport pasingetosha
Ni kweli pasingetosha lakini imagine anagalu baadhi wangekuwa na wazo la kupaki “somewhere” adha ya jana ingepungua “somehow” kwa baadhi ya watu. Kuna dogo jana ameniambia yuko posta kwa masaa 4 kutoka Wizara ya Ardhi mpka mnara wa askari. Nikamshauri atafute ofisi hapo mjini apaki amtoe mlinzi Msimbazi achukue boda aende Home. Alifanya hivyo na ik amsaidie kuwahi home kwake.
 
Na kweli asee

Na by the way,

Ukishaona mtu anakuja kwenye uzi kama huu ambapo watu wanajadili mafuriko na adha za usafiri jijini Dar, yeye anaanza kukuambia eti hata Joberg, sijui London nako hua kuna mafuriko, so what? Kwahiyo kama huko kuna mafuriko maanake sisi hatuwezi ku improve huku kwetu? Kwahiyo watu waliofika majumbani saa 10 alfajiri wasilalamike kisa Joberg nako kuliwahi kutokea mafuriko?

Ndio maana nasema kutembea nchi mbalimbali na kujidai kwamba una exposure hakumuondolei mtu kale ka ushamba ka asili ambako alitoka nako kijijini na lazima kataonekana tu hawezi kukaficha!
 
Back
Top Bottom