Mvutano mkali kati ya Trump na Zelensky watokea katika Ikulu ya White House

Mvutano mkali kati ya Trump na Zelensky watokea katika Ikulu ya White House

Daaah unyonge ni mbaya sana, rais anadhalilishwa kiasi hiki kwa vile walafi wanataka madini tu?
 
Akina Tundu Lissu ndio hawa akina Zelensky....kulialia kwa WAJOMBA....Mh.Rais Trump hataki wapwa......
 
Ujinga wao ukraine walikubaluana ukraine kamwe isijiunge nato...kierehere Chao kwa ujeuri wa misaada kamdindia kaka mkubwa....kikwapi sasa...kaka kamega kiwanja na kisago juu
...kiburi si maungwana.....kiko wapi sasa....mikoa 5 imeondoka....deal la madini "graphite ,Lithium ,Titanium" anaingia na Marekani atake asitake....mwisho kabisa mshindi ni Putin na Trump....
 
Ujinga wao ukraine walikubaluana ukraine kamwe isijiunge nato...kierehere Chao kwa ujeuri wa misaada kamdindia kaka mkubwa....kikwapi sasa...kaka kamega kiwanja na kisago juu
Katika vita haina mshindi.
Urusi kuhidumia vita zaidi ya miaka 3 hili sio jambo zuri na hakuna ushindi wowote;
Ameharibu uchumi kuhudumia vita
AMepiteza wanajeshi kibao
Silaha nyingi zimeteketezwa.

Hakuna mshindi katika vita hii
 
Aisee bora kasimamia anachoamini ingekuwa kiongozi wa kiafrika ungekuta mkataba wa kipuuzi ushasainiwa zamani
Zele kaonyesha kuwa haijalisha una nguvu ndogo kiasi gani, haijalishi shida ulizokuwa nazo ni bora kuwa na msimamo.
Trump alifikiri angepata kitonga
Upo uwezekano Zelensky kaagizwa na nchi za EU kukataa matakwa ya Trump...nina uhakika kwa asilimia 100% kuwa EU NDIYO WAMEMPA MWONGOZO ZELENSKY WA KUFANYA HIVYO.
 
Kajitutumua, si kazi rahisi kuitetea nchi yako.
Zelensky yupo sahihi kabisa kuhusiana na msimamo wake kwa maslahi mapana ya nchi yake na Watu wake.
Ni Bora kufa huku ukitetea Nchi yako kuliko kuendelea kubaki hai huku umeisaliti Nchi yako na kuitoa sadaka kwa mumiani.
 
Upo uwezekano Zelensky kaagizwa na nchi za EU kukataa matakwa ya Trump...nina uhakika kwa asilimia 100% kuwa EU NDIYO WAMEMPA MWONGOZO ZELENSKY WA KUFANYA HIVYO.
Usalama wa Ukraine ndio Usalama wa bara lote la Ulaya, hususani Ulaya Magharibi.

Ukraine ikishindwa Vita maana yake ni kwamba Ulaya yote kabisa itakuwa imetekwa na Urusi. Hili litakuwa jambo baya sana tena ni jambo la hatari kubwa sana kupita kiasi kwa Watu wote kabisa wa bara la Ulaya.
Kwa hali kama hiyo, ni Bora Watu wa Ulaya waingie katika Vita ya Tatu ya dunia kuliko kuruhusu Urusi ishinde Vita hiyo.
Kwanza kabisa, lengo Kuu mojawapo la kuanzishwa kwa NATO ilikuwa ni kupambana na Udikteta wa Watawala wababe wa Urusi.

Urusi ikishinda Vita hii, bado ataendelea kuteka maeneo mengine zaidi na zaidi hadi Ulaya yote kabisa iwe chini ya Utawala wa Urusi, Putin hataishia kuiteka Ukraine peke yake.
 
Ona hapa alivyosimangwa na kuwekwa mtu kati huko White house. Kwa mtindo huu kila nchi itataka kujidhatiti kivita. Pengine tutashuhidia hata wamiliki wa silaha za nyuklia wakiongezeka.

View: https://youtu.be/Ch0q31cfEIQ?si=osbqYAW03TSSMj40

Trump hana adabu hata kidogo, haya mazungumzo siyo ya WATU wenye hadhi ya Urais, bali ni watu hasa Wanawake wanaosutana huko mitaa ya uswahilini kama vile Tandale kwa Mtogole!

Trump ameinajisi Ikulu ya Marekani
 
Back
Top Bottom