Mvutano mkali kati ya Trump na Zelensky watokea katika Ikulu ya White House

Mvutano mkali kati ya Trump na Zelensky watokea katika Ikulu ya White House

Ona hapa alivyosimangwa na kuwekwa mtu kati huko White house. Kwa mtindo huu kila nchi itataka kujidhatiti kivita. Pengine tutashuhidia hata wamiliki wa silaha za nyuklia wakiongezeka.

View: https://youtu.be/Ch0q31cfEIQ?si=osbqYAW03TSSMj40

Afrika ijifunge kibwebwe,tuendelee kujipanga kuiba chaguzi kwani hiyo itatuokoa,tuendelee kupiga uvivu kwani hiyo itatuokoa,tuendelee kutojituma kufanya matumizi sahihi ya rasilimali zetu kwani kwetu huo ndio ujanja,hadi tutakapo kiona kilicho mnyoa kanga manyoya.
 
Usalama wa Ukraine ndio Usalama wa bara lote la Ulaya, hususani Ulaya Magharibi.

Ukraine ikishindwa Vita maana yake ni kwamba Ulaya yote kabisa itakuwa imetekwa na Urusi. Hili litakuwa jambo baya sana tena ni jambo la hatari kubwa sana kupita kiasi kwa Watu wote kabisa wa bara la Ulaya.
Kwa hali kama hiyo, ni Bora Watu wa Ulaya waingie katika Vita ya Tatu ya dunia kuliko kuruhusu Urusi ishinde Vita hiyo.
Kwanza kabisa, lengo Kuu mojawapo la kuanzishwa kwa NATO ilikuwa ni kupambana na Udikteta wa Watawala wababe wa Urusi.

Urusi ikishinda Vita hii, bado ataendelea kuteka maeneo mengine zaidi na zaidi hadi Ulaya yote kabisa iwe chini ya Utawala wa Urusi, Putin hataishia kuiteka Ukraine peke yake.
Hapa umetoa boko aisee. Putin hana haja na ardhi ya mtu. Kinachoitokea Ukraine ni kitendo chake cha kutaka kumletea Russia adui sebuleni kwake. Hayo mengine uliyoandika ni mihemuko yako tu ya kuwa pro-west.
 
Mimi siyo mtaalamu wa diplomasia.Ila hata kwa kutumia D mbili,naelewa kwamba Trump na makamu wake walikosea,walivunja mila ya kidiplomasia.

Trump na makamu wake walikuwa wanadhani wanaongea na mkuu wa wilaya waliyemteua wao mpaka Zelensky alikuwa anasikika akiwakumbusha kwamba Zelensky is a president.
 
ZELENSKY. Kumbe kajeuri😄

Bado watawala wa CCM wakienda White House sijui kama watakuwa wameotea nini watakikuta, au itakuwa surprise kwa viongozi wa CCM na vyombi vyao vya Dola kama mabalozi na usalama wa Taifa kitego cha nje kuwa na taarifa kabla ili waweze kuwa na ubavu kama wa Zelensky kutoka na weledi wa mabalozi wake ktk ujasusi wa kidiplomasia na usalama wa taifa kitengo cha intelejensia ya nje ili wasikurupushwe White House..

Ujasusi Blog
www.ujasusi.com
Intelligence insights on series of leadership changes at Tanzania's ...
1740795570402.jpeg

13 Jul 2024 — The appointment of Selemani Mombo as the new TISS Director General could have significant impacts on Tanzania's security and intelligence


Waziri wa Mambo ya Nje Mahmoud Kombo, wakurugenzi wizarani, mabalozi uwezo wa kukusanya taarifa za maoteo ili Tanzania isijikute inapata surprise kubwa kutoka kwa washirika wake


View: https://m.youtube.com/watch?v=ZJJtJslaC_4
 
ZELENSKY. Kumbe kajeuri😄
🤣🤣🤣 kawekwa mtu kati na wafadhili wake but still analeta ubishi ,

Mbona wame mdhalilisha hivi lakini na kuleak maongezi yao dahh zele ana mwisho mbaya aisee
 
At least anajitahidi hata ikiashindikana amejaribu, na wazungu ndio michezo yao. Wanesubiri ashachakazwa na mental state yake might not be at its best ndio wanataka kumpa masharti ya kuingia makubaliano ya kijambazi.
🤣🤣🤣
 
Zele yuko sawa iweje anyanganywe ardhi hapo asirudi nyuma kama wanapewa madini ardhi yake irudi vinginevyo aendelee kukiwasha au itawaliwe na us na Mrusi kinguvu. Warusi nao washenzi tu ila wanaunafuu kuliko mayahudi
Atakiwasha vipi sasa endapo mfadhili wake mkuu ataamua kumnyima misaada ujue comments zenu kuna wakati zina chekesha sana 🤣🤣🤣
 
Katika vita haina mshindi.
Urusi kuhidumia vita zaidi ya miaka 3 hili sio jambo zuri na hakuna ushindi wowote;
Ameharibu uchumi kuhudumia vita
AMepiteza wanajeshi kibao
Silaha nyingi zimeteketezwa.

Hakuna mshindi katika vita hii
Unajitekenya huku unacheka mwenyewe ?? 🤣🤣
 
Upo uwezekano Zelensky kaagizwa na nchi za EU kukataa matakwa ya Trump...nina uhakika kwa asilimia 100% kuwa EU NDIYO WAMEMPA MWONGOZO ZELENSKY WA KUFANYA HIVYO.
Watamponza mwenzao wakati akiwa anauliwa wao watakuwa ktk sebule zao wanakunywa cofee
 
Upo uwezekano Zelensky kaagizwa na nchi za EU kukataa matakwa ya Trump...nina uhakika kwa asilimia 100% kuwa EU NDIYO WAMEMPA MWONGOZO ZELENSKY WA KUFANYA HIVYO.
Uko sahihi 100%
 
Back
Top Bottom