Tunataka tija ya uchumi iongezeke hata angekuwa ni mhindi anakuja kumiliki hiyo bandari kwetu ni sawa tu.
Tunataka kuondoka na foleni za kuingiza meli ambazo zina uhusiano wa moja kwa moja na bei za bidhaa huku mitaani.
Tunataka kuharakisha utoaji wa mizigo katika eneo lile la bandari, hali inayoleta ujenzi wa ICDs nyingi katika maeneo yale ambazo zinamilikiwa na wenye uhusiano wa karibu na wanasiasa wenye vyeo vikubwa serikalini.
Tumetambua na tulishatambua faida za DPW muda mrefu sana uliopita na tupo na Rais SSH na serikali yake, mahali ambapo TRA inaweza kupata trilioni 27 kwa mwaka na wakati kwa sasa inapata trilioni 7 tu, tupo na mipango yote ya serikali ya sasa.
Hawa kina Mwabukusi, Lissu na Dr Slaa wanatumiwa na wote wenye kufaidika na haya magumashi yanayoendelea kuwatajirisha wachache pale TPA, lakini mwisho wake umekaribia.