Barbiedoll
JF-Expert Member
- Apr 7, 2023
- 772
- 2,150
Bata uwe na ela mkuuTupe story za city pub na mbeya pazuri na ueleze bata hua likoje anzia uyole, mbalizi, iyunga pale breakpoint, mafiati pale carnival, sae pub, au tueleze hata viwanja vipya vya mama john, sisi hapa ni story tu hatuna maneno na mtu
Nimeshangaa sana kijana alitaka kupotosha eti show ya Michael Jackson
tumsamehe bureeeeee, hajui tupo watoto wa mnazi mmoja humu. Muulize Pat Shange alikuja lini pale Taifa.
Ku -invest kwa Watoto kunasaidiA...Nilikutana na mmiliki wa Silent Inn, sukari imemchosha, na ameshakuwa mchungaji, anaishi kwa mwanaye ambaye ni daktari Nairobi.
Ruaha Galaxy pale Kimara Korogwe miaka ya 90 mwanzoni ulitamba sana. Shoo za wasanii wa enzi hio zimepigwa sana paleYawezekana anamfananisha Mj wa USA na yule wa Ruaha Galaxy enzi zile teh teh
Basi MJ wa Bongo alikuwa ananing`inia kwenye visigino kumuigiza MJ original, basi ilikuwa hatari tupu.Ruaha Galaxy pale Kimara Korogwe miaka ya 90 mwanzoni ulitamba sana. Shoo za wasanii wa enzi zimepigwa sana pale
Kule Kimara mwisho kulikuwa na ukumbi wa washua ulikuwa unaitwa Kimara Motel umejificha mazingira tulivu sana sasa hivi umefanywa shule ya Midlands
Naelewa kuwa dala ilikuwa ni shilingi tano,Kuhusu ''dala dala''. Magari yaliitwa daladala kwa sababu yalikuwa yanachaji sh. 5 ambayo ilikuwa ni ile sarafu ya pembe iliyokuwa inaitwa dala. Miaka hiyo senti 20 ilikuwa inaitwa ''mbuni'' sh 1 ikiitwa ''mwenge'' sh 5 ndiyo iliitwa ''dala''. Kuna magari yaliyokuwa yanajiibia kubeba abiria wakifika kituoni wanasema ''dala dala, dala dala''', yaani sh tano, sh tano sh tano
Mimi nimesoma mnazi mmoja primary headteacher akiitwa Chalila baadae akaja Mtolela,namkumbzka mwalimu mtengatumsamehe bureeeeee, hajui tupo watoto wa mnazi mmoja humu. Muulize Pat Shange alikuja lini pale Taifa.
Ahaa mzee wako alitisha,mzee Ruksa hatutamsahauPesa ilikuwepo kipindi hicho. Mzee wangu alisafiri mwaka 1994 dar hadi malawi kwenda tamasha la mnyama lucky dube.
Yule jamaa alijizolea umaarufu sana ila alimuwezea sana MJ mwenyewe. Hivi aliishia wapi?Basi MJ wa Bongo alikuwa ananing`inia kwenye visigino kumuigiza MJ original, basi ilikuwa hatari tupu.
Na mimi hili nimelisikia sana japo huwa naamini kuna uwezekano sababu ikawa nyingine, au ilipewa tu hilo jina na watoto wa mjini tu kwa sababu kila sarafu au noti ilikuwa na jina lisilo rasmi.Naelewa kuwa dala ilikuwa ni shilingi tano,
Nilikuwa najaribu kuelezea kwa nini ile sarafu ya sh 5 iliitwa dala!!
One dollar ilikaa muda mrefu sana ilikwa na thamani ya sh 5 , ile sarafu ilipotoka ikaitwa one dollar , waswahili tukaibatiza dala
Itoshe kusema wewe ni born town uliyetembea hapa nchini .Basi nilikulia manerumango, au nilikulia bwejuu, au nilikulia lituhi , au nilikulia soni lushoto, au nilikulia nyambui musoma, au nilikulia utete ya ikwiriri, au nilikulia kaparamsenga ya kigoma au nilikulia malamba ya tanga, au nilikulia laela ya sumbawanga, au nilikulia malya ya kwimba, au nilikulia kitangari ya mtwara, au nilikulia mgudenj ya mlimba moro huko au nilikulia kifanya ya njombe au nilikulia igurusi au ihanda ya tunduma, au nilikua majimoto ya mpanda, au tufanye kisarawe kisha nikahamia chanika baadae nikahamia kiwalani ya airport au tufanye tandale uzuri, au tufanye nilikulia kiponzelo iringa huko au nilikulia ruangwa na ikuti huko tukuyu au nilikulia mondo huko kondoa, au nilikulia lugoba, au nilikulia majita huko musoma, au nilikulia njoro same huko au tufanye nilikulia ndungu milimani, au chagua wewe then mimi nitakubali
Hata sijui, sijui alirudi kwao usukumani au ndo basi yupo mitaaniYule jamaa alijizolea umaarufu sana ila alimuwezea sana MJ mwenyewe. Hivi aliishia wapi?
Wazee wengi wajanja walijenga kipindi cha Mwinyi. Nyumba nyingi Sinza, Kinondoni zimejengwa kipindi cha MwinyiMimi nimesoma mnazi mmoja primary headteacher akiitwa Chalila baadae akaja Mtolela,namkumbzka mwalimu mtenga
Ahaa mzee wako alitisha,mzee Ruksa hatutamsahau
Daaah! Kila la heri kwake kwa burudani alizotupatiaHata sijui, sijui alirudi kwao usukumani au ndo basi yupo mitaani
Kweli kabisa huo msemo ulitamba sana hasa kipindi cha MkapaKulikuwa na msemo kuwa kama hukujenga kipindi cha mwinyi hujengi tena
Wapi papa Musofe ? Je kizaizai ila sitamsahau wala kumsamehe Mzamiru KatunziMatajiri wengi wakubwa Tanzania waliibuka kwa Mzee Mwinyi, wengine wakaja kupata pesa kwa kikwete utawala wa marais wengine pesa haikuepo, enzi za Mwinyi ndio watu walikula bata Mtu akitoa mzigo zanzibar akifika Dar anakuta watu hadi wazimbabwe wanasubiri, dili za magendo zikazaliwa kipindi hicho lakini utawala wa mwinyi ndio ulizaa hadi matapeli wakubwa hadi strong room na wazee wa bandari ilikua kwa mwinyi na mkapa kidogo,
Siku watembelee pale Hyatt Regency level 8 wajionee watu wanaotumia pesa hapa mjiniNimekupa mfano hapo juu , ukienda beach kidimbwi leo huo mshahara wako wa miezi mitatu mfululizo mtu anamaliza ndani ya masaa tu, na kidimbwi sio popular kwa watu wanaotumia pesa mjini hapa infact kumekaa kihuni,, zipo sehemu access tu ya kuhudumiwa watu wanaangalia umepark gari gani
Dah....laki enzi za mzee Ruksa ilikuwa pesa ndogo sana....unaipata bila jasho 🤣 🤣🤣🤣🤣Laki moja mwaka 1988?
hao waliofurika wameacha urithi gani kwa wajukuu zao mpaka sasa?
maana laki 1 ya '88 kwa sasa ni kama milioni 1. Bei ya viwanja kumi jijini Dar kwa enzi hizo