Mwaka 1988 Chakachaka alipiga show Makondeko Kibamba kiingilio kilikuwa 100,000

Mwaka 1988 Chakachaka alipiga show Makondeko Kibamba kiingilio kilikuwa 100,000

Nini usichoamini broo ,
Watu waliingia makondeko kwa laki mwaka 1990, sio kwa kuambiwa bali nilishuhudia kabisa
Kanda bongoman alipokuja Tqnzania , hakuna sehemu alitumbuza chini ya kiingilio cha laki.
Soda mtaani ilikuwa ina uzwa sh 20 hadi 25, ila siku ile pale iliuzwa karibu na sh 100.

For the records, nauli ya basi mjini kote na uda ilijuwa kwa basi la uda sh 5, ndo sababu ikaitwa dala dala (dollar dollar ) , inasemekana ila:sina uhakika kuwa dola ilikaa muda mrefu ikiwa na thamani ya shilingi tano za kitanzania , ilipotoka tharafu ya shilingi tano , wajanja walikuwa wanaita 1 dollar waswahilib tukageuza dala.
Kutoka hapo makondeko kwenda kariakoo enzi hizo nauli ilukuwa sh 12 , na ndo ilikuwa ni nauli kubwa kwa outskirts suburbs na dar, ifuatiwa na tegeta., Mkuranga kisemvule , mvuti, mwanambaya , kwa miaka hiyo yakiwa ni makazi ya simba na binadamu wachache wabishi.
Usipoteze calories kuelewesha wanaotaka kuwa against after all huyu anakipaji cha kupinga kutaka aonekane anaelewa.
 
Ndugu yangu uzi ukikuzidi umri we tumia fursa ya kujifunza,kanda bongo man alitimuliwa jenya,kuna ndoa zilivunjika huko,hii ni kweli sio chai
Upo right mkuu, tatizo la dot. Com kabla ya kutulia na kujifunza ,wao wanajifanya wanajua kila kitu wakati ni wapumbavu, na pia wameshazoeshwa kutafuniwa kila kitu, na pia waeleweshe kuwa wimbo uliopigwa na Mbilia Bel (nakei nairobi)ndio uliomfanya president Moi awafungulie tena hawa Congolese musicians
 
Alipiga pale Kilimanjaro, Simba Grill. Mmiliki wa Mahepe ndo alimleta nchini kupitia Roy West import and Export ikiwa na makao yake pale Mansfield (uhamiaji zamani).
Thanks na salute mkuu, kipindi nchi Ina heshima na adabu, tulikua hatuchezewi ovyo Tanzania, Africa nzima ilikuwa inasubiria tamko kutoka Dar es Salaam ndio na wao watoe tamko lao
 
Legend
hata mie nilikuwa nashangaa hiyo show Michel jackson alipiga wapi. Nakumbuka kulikuwa na uvumi kuwa aliposhuka airport alifunika pua yake kuashiria kuwa Dar inanuka na akaishia sinza kwa watoto yatima.
Huyu jamaa ni muongo yet amekuwa akiwashutumu wenzake kuwa ndio waongo.
Huyu mmnapa airtime kujibishana nae huyu ni mshamba alietukuka.

Poleni sana.
 
Upo right mkuu, tatizo la dot. Com kabla ya kutulia na kujifunza ,wao wanajifanya wanajua kila kitu wakati ni wapumbavu, na pia wameshazoeshwa kutafuniwa kila kitu, na pia waeleweshe kuwa wimbo uliopigwa na Mbilia Bel (nakei nairobi)ndio uliomfanya president Moi awafungulie tena hawa Congolese musicians
Dotcom hudhani kila kitu kipo google,hapo ameshagoogle akaambulia patupu,ila hajui ubongo wa binadamu unatunza kumbukumbu sana
 
Imepita miaka 35,
Nimekumbuka kitu kimoja
mwaka 1988 enzi hizo Ivon Chakachaka akiwa kwenye peak,kulikuwa na mmakonde mmoja akiitwa Dk Khalid Alex mbunge wa Mtama by then,sina uhakika na jimbo ila ni huko kusini
,alikuwa na ukumbi kule kibamba Luguruni maarufu kama Makondeko,

Ule ukumbi ukienda leo hakuna hata mabaki ya tofali hata moja ulikuwa ukumbi wa kisasa kwa miaka ile,kumbuka ulikuwa utawalawa Mzee Ruksa,

Chakachaka akiwika na nyimbo zake kama Sangoma,Umkhomboti,Thank you Mr Dj,am in love with DJ,alikuwa wa moto kwelikweli ila huyu tycoon wa enzi hizo bwana Alex akafanikiwa kumleta nchini,kiingilio kilikuwa shilingi laki moja,lakini ukumbi ulifurika aswaa japo uko nje ya mji,ni miaka 35 imepita ila laki moja !!!
Mluu
Tutemdee haki basi

Japo kapicha ka ukumbi ili sisi tuliozaliwa miaka ya tisaini tuone
 
Yeah LA Prima ukumbi uliokua umetulia vema na restaurant yao ile iliyoitwa Pieces!hivi Mzee Lyimo angali hai(owner),huyu mzee alipenda sana hospitality business, kuna anayekumbuka pale Bushtrekker restaurant opposite Serena Hotel?,source ya Maboi ngangari Dar nzima
 
Ndugu yangu uzi ukikuzidi umri we tumia fursa ya kujifunza,kanda bongo man alitimuliwa jenya,kuna ndoa zilivunjika huko,hii ni kweli sio chai
Unaonekana ulikuwa mtoto
hii ilikuwa mwaka 1990 Ezekia Oyuki
Moja ya watu walikuwa na nguvu sana chini ya utawala wa Moi
Alikuwa na harusi ya mwanae na aliyekuwa amealikwa kuja kutumbuiza alikuwa ni Kandabongoman
Na bongomani alipojua kuwa harusi inafanyikia Kisumu akaghairi kwenda badala yake akaenda Nairobi kwenye show ya Tshala Muana
Basi Ezekia kusikia Bongomani hajaja na Yuko Nairobi alichukia na akatoa masaa 24 bongomani atoweke nchini Kenya huo ndiyo ukweli na bongomani amekuja kurudi Kenya mwaka 2003 na Kama hujui Ezekia Oyuki ndiye alikuwa mtuhumiwa wa mauaji ya Robert Ouko
Ezekia alifariki 1992 Kifo kilichojaa utata
 
Huwa sielewi mpaka wa kibamba na mbezi,kile chuo cha St Joseph inadaiwa kipo kibamba,Luguluni ni mtaa ndani ya kibamba,sina uhakika lakini
Mpaka wa mbezi na kibamba ulikuwa mbele kidogo ya magari saba , enzi hizo kulikuwa na bar maarufu ya mbezi inn, enzi hizo ikimilikiwa na bwana mmoja kuitwa mzee mbwana .
Ile magari saba uluguruni mpaka ulikuwa na kibamba hospitali , uluguruni na magari saba lilikuwa ni eneo moja likijulikana kama mailli 15, jina la.magarinsaba lilikuja baadaye sana baada ya kutokea ajali ya lori la mafuta, yakaungua magari saba moja likiwa na maiti ndani.
Chuo cha saint joseph kipo luguruni
 
Shukrani mkuu kwa ufafanuzi mujarab
 
Basi kuna kitu (wivu wa kimaendeleo) ulisababisha hayo yote
Sio wivu bali zilikuwa plan mbaya za Dr, Alex khalid mutawalla
Ukumbi ulitumia pesa nyingi za mikopo na haukukaa muda ukaanza kufifia kabla hata pesa haijarudi, umauti ulipomkuta Dr pale pakawa ni mali ya benki na brokers wake , bomoa bomoa ya kwanza scanphill colas wakiwa wanajenga ubungo mlandizi road mwaka 98 ikapaathiri sana , ilivyokuja bomoa bomoa ya mzee baba ndo pakaisha kabisa
 
Back
Top Bottom