Mwaka 2023 Waziri Ummy amepigwa attacks za kimyakimya sana

Uwo mda wakufanya uchawa ungeutumia kutafta kodi ya nyumba lakin pia kutafta ada za shule za watoto izo pesa za uchawa huwa zinalaana huwez fanya nazo maendeleo ni vema ukatafta pesa zako harari
 
1. Bima ya Afya chini ya NHIF, Ummy ameshindwa kuhandle situation kabisa.
2. Utendaji mbovu wa hospitali zilizoko chini ya wizara ya afya, hali ni mbaya kwenye hospitali, utendaji mbovu, yeye kama waziri kama ameshindwa kusimamia lazima apopolewe.

Lakini mbona wakati wa JPM alikuwa mtendaji mzuri, au alikuwa akifanya kwa woga.
 
Kuna mambo mengi sana kama wizara ya afya inachemsha. Sio kila mtu ana uwezo wa kwenda hosptali za private, tegemeo la wengi ni serikalini.

Unafika hosptali unamkuta nurse yupo busy anachat na hapo kuna msururu wa wagonjwa. Ukiingia kwa daktari unaambiwa mtandao hamna na hawawezi kutibu mpaka mtandao urudi. Kila kitu cha serikali ni kimeo. Lakini afya ni kimeo zaidi maana hapo ndipo uhai wetu unapochezewa
 
Je yansyoibuliwa ni uongo?
 
nikujibu kwamba anaonewa sababu hayo anayosemwa nayo sio ya level ya Waziri, mathalani mtumishi amefanya malpractice Waziri anahusikaje?
Hapa ndipo tunapofeli ngozi nyeusi. Eti siyo level ya waziri. Mbona kwa wenzetu huko hakuna haya ya kuteteana katika maovu? Polisi anaua raia huko, waziri wa mambo ya ndani anawajibika. Mzazi anafariki kizembe wakati wa kujifungua, waziri wa afya anawajibika.

The buck stops with the one on top. Ndiyo maana kuna uwajibikaji na kutofanya mambo hovyo hovyo maana hata watu wa chini wanakuwa wanajua madhara watakayoyasababisha kwa uzembe wao. Kwamba yanaweza kuwaathiri si wao tu bali hata mkuu wao wa juu kabisa.

Sisi bado! 🚮🚮🚮
 
Kazi ipo!!!

Nchi yetu ina watu wengi sana, serikali yetu haina uwezo wa kuwahudumia watu wake kwa hali itakayoweza kumridhisha kila mtu.

Watumishi wa kada ya afya ni wachache sana kulinganisha na wingi wa wateja, na hapo hapo wengi wao sio waaminifu katika utendaji wa kazi zao

Vifaa navyo inaweza kuwa ni tatizo au watumishi ndio matatizo katika kutoa huduma.

Wizarani kuna maofisa kibao kuanzia Katibu Mkuu,, wasaidizi wake na wakuu wa vitengo, je hawa nao wameshindwa kumsaidia waziri?



Huko mikoani kuna RMO's wilayani kuna DMO's bado kuna wasimamizi wa vituo hivyo vya afya. Je hawa wameshindwa kutekeleza wajibu wao?


Ni kipimo gani tunaweza kukitumia kumpima waziri huyu?
 
Hospital za serikal huduma mbovu mno hazijawsh kuwa nzuri hata siku moja vitanda hakuna ,watoto wanapoteza maisha na mama zao halaf mnataka wasisemwe hebu amkeni
Tokea lini watz wakaamka?ndo kwanza wajinga wanazidi kuongezeka na umaskini ndo unawameza kuwa machawa wa mambo ya kijinga?Tukubali tupo nchi isiyojielewa tuishi nayo saizi waziri analipa watu kuficha udhaifu wake[emoji20]
 
Ma-fisi-em ndiyo yalivyo, tujadili nini? Yanawaza madaraka tu wakati uwajibikaji hayawezi.
 
Hakuna anayemchafua wakati yeye mwenyewe ndio mchafu.

Ummy alitakiwa kama ambavyo hana idea na masuala ya afya atumie watalaam wa afya kujibu issue za afya.

Kule mtandao wa X anamtumia yule dogo Eric Benard ndio chawa wake anatafuta team ya kupiga PR watu wanalipwa 20k kumtetea Ummy badala ya kusimamia facts tukio la majuzi la ile hospital Mwanza huyo dogo ameokoteza picha kutetea watu hawalazwi chini na kupokonywa simu mwisho wa siku wakawa wamejipiga "own goal " picha zilikua za kituo tofauti na utetezi na ni za miezi 6 nyuma.

Huyu dogo ndio inahisiwa pia ndio admin wa page ya wizara ya afya kule X.

Ummy ameonyesha uwezo mdogo ndio maana amekuja na mkakati huo na kila sentensi lazima aseme tunamshukuru mama .
 
Tanzania yetu hii yani watu kuelezea changamoto zilizopo kwenye sekta ya Afya ni kumchafua waziri wa afya na sio Katibu Mkuu, Naibu waziri au Naibu Katibu mkuu

Nafikiri watu wanashida na sekta ya afya sio waziri wa afya sababu serikali yote ni ileile hata awekwe nani
 
Kuna ukweli ambao kila mtu anatakiwa aukubali. i.e. mfumo wa uongozi na muundo wake haufai kwa nchi yetu. Nchi yetu ni kubwa na haiwezi kuongozwa kutoka Dodoma.
 
Namuona mrembo Ummy hana baya na mtu halafu anatekeleza majukumu yake kiweledi sana(muono wangu) ila wapo watu wanamtafutia baya kila siku iendayo kwa mola.AU MIMI NDIO SIJUI YA NYUMA YA PAZIA??
Kumbe ni "fantasy" zako kwa kupenda wanawake wenye rangi kama ya Ummy ndio kilichofanya useme anashambuliwa?

Hii tabia alikua nayo Magufuli aliwahi kumsifia mwanamke aliyemteua kuwa yeye kama msukuma anapenda wanawake weupe ili kusudi tu akimuangalia anapata furaha.

Hizo fantasy mbaki nazo huko sawa mjinga wao?

Tunataka waziri mwenye uwezo kiutendaji huo urembo yapo majukwaa kama ya Miss Tanzania mpeleke Ummy huko.
 
Kwamba ummy elimu ndogo? unajua level yake ya elimu? Sasa kama ummy ni elimu ndogo vipi boss wake? Kwanza wewe kweli ni mtaalamu wa afya mbona mwandiko wa kiswahili na majungu. Ummy ni kweli anaweza kuwa ni kiongozi dhaifu kwenye serikali dhaifu lakini usizidishe chumvi mpaka hoja yako ikaonekana ni majungu
 
Kwa ile habari iliyowahi kutokea Tanga. Yule dada aliyefariki wakati anajifungua mbele ya mamake mzazi. Nadhani president alitoa ubani kama sikosei. Ummi alitakiwa kuwa ni a long gone minister.

Kwa sababu kwenye situation kama hizi hana agenda. Ama kwa lugha nyepesi hana plan madhubuti za kukabiliana na hali hiyo.
 
Kiuhalisia ummy ana bahati tu ya kupendwa na watu ila kwenye utendaji wa kazi ni hamna kitu hospital nyingi za serikali huruma ni mbovu na dawa hata antibiotics hakuna.

Ila kuna siku ndo nilimuona ummy muigizaji maana walifanya maadhimisho ya siku ya malaria duniani kwenye kiwanda flani pale kibaha ( Cha viua wadudu) kama sijakosea wakati kile kiwanda kilikua hakifanyi kazi miaka 2 nyuma kilikua tayari kishafungwa na waliokota vijana mtaani wakapewa 5000 na t-shirt wavae kama wafanyakazi wa kile kiwanda.
 
Unatetea ujinga kwa mifano raisi kabisa hebu zungumzia na swala la vifo vya wazazi mahospitalini hebu zungumzia ukosefu wa vifaa na madawa hospitali hebu zungumzia hali za hospitali zetu mkuu usiwe mtoto
 
Tuanze kwanza kujadili kwa haki kabisa nani alipost picha za chongolo hata akatolewa kwenye kiti tena muda mfupi bada ya makonda kuteuliwa???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…