Mwaka 2023 Waziri Ummy amepigwa attacks za kimyakimya sana

Tuna Hela ya kununua goli milioni 10 halafu hatuna Hela ya kupeleka dawa ma hospitalini.
 
Hivyo vyeo ni kawaida kupigwa vita kwa Afrika.

Watu mpaka wanarogana kwa uafisa tu itakuwa uwaziri?
 
We nae nilikuwa nakuheshimu kumbe mpuuzi Tu

Machawa mna KAZI Sana.

Sasa hiyo 20k unayopewa umsifu Ummy inakusaidia nini?
 
Huyu Ummy amepiga Pesa zaidi ya 1Billion unatetea upuuzi tu
 
Swadakta umesema kweli
 
Dah, hospital gani Tena kushimiana Hadi simu jamaa! Mimi sijawahi peleka familia yangu serikalini kutokana na kesi Kama hizi ninazosikia au kusoma
Temeke Hospital, Mbagala Zhakiem, Round Table na hospital yoyote ya serikali wana pokonya simu wazazi wengine waficha kiswaswadu anaongelea chooni manesi wasimuone ukiwa na shida kaongee na nesi anapigia ndugu aisee vile hospital nilimfata Dr wangu niliapa sirudi hio clinic nayo majanga matupu labda uonge nesi 2000-3000 utahudumiwa vizuri kwanza hawana muda uhoji maswali hio foleni sasa ya maabara hapana jamani niliapa sitorudi nikazaa Private raha sana unabebembelezwa unanyeyekewa.
 
Waziri Ummy ni genius katika kusimamia wizara za nchi hii. Changamoto anakwamishwa na siasa za hovyo za nchi yetu. Watumishi sasa wananyanyasika sana na bima ya afya
 
Huo ufawidhi vituoni ni kazi ya kujitolea tu, Kama unaona hawafai wekeni wanaofaa
 
Chanjo ya COVID nadhani tumetia fora kwa KUPIKA DATA ili kufurahisha Donors 🇹🇿🇹🇿🇹🇿
 
Ummy kwenyr masuala yote ya kupata maokoto ili aneemeke yuko vizuri. Marehemu magufuli alikuja kumshtukia baadae sana kama ni msanii. Alijiweka na watu wa karibu na marehemu magu akijua sifa zake zitamgikia magu and that had worked well for her.

Hizi pesa za uviko zimeliwa haswa na yeye zikiwa chini yake. Hata wakati huu wa SS. Kajiweka na watu wa karibu na dini na network ili mama amkubali.

Lakini yapo mazuri ameyafanya haswa donor funded proposals ila nadhani afya inahitaji kichwa kinhine ili nacho kisukume mbele gurudumu.

NB. Deal ndogo to kwa waziri yeyote ni si chini ya million 500. Si ajabu hawa watu kusomesha watoto wao Braeburn, ISM, IST, Feza, Agha Khan Mombasa moja ya shule la kibepari ukanda huu wa east africa.
 
Sukuma gang kazini
 
Chuki binasfi na wivu uliopitiliza dhidi ya huyu mama. Madaktari wanakosea huko na kusababisha madhara kwa wananchi tuhuma analetewa ummy as if yeye ndio yupo Kituoni. Kwenye Hospitali kuna timu za uendeshaji huduma za afya kuanzia mganga mkuu wa wilaya, mkoa, kuna mabaraza ya kitaaluma kuna Idara za Wizarani then ndio aje kuamua yeye wa Mwisho au ORTAMISEMI. Kuna makosa mengine kweli tunaona kabisa hapa kuna udhaifu kwenye mifumo na Mhe. Ummy kweli tunaona amekuwa mstari wa mbele kukemea utendaji mbovu katika Sekta ya Afya. Sasa Watanzania tunataka tupewe sijui Waziri gani aje afit hapo. Kwa Dunia ya sasa hatukupaswa kufanya hivi vitendo vya kumdhoofisha morari Waziri Ummy Mwalimu anachapa kazi nzuri na sisi tunaona. Tuache mambo ya Wivu usiokuwa na tija.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…