Mwaka 2023 Waziri Ummy amepigwa attacks za kimyakimya sana

Mwaka 2023 Waziri Ummy amepigwa attacks za kimyakimya sana

Mimi ni shahidi wa kuwa huyu Shangazi anajitahidi sana sana kwenye kazi zake, labda tu kuna watu wanampiga vita kwa mambo yao. Huyu Shangazi hanijui, simjui, ila mwaka jana alitusaidia sana mimi na familia yangu. Mama yangu alikuwa anashida ya figo, tukamtafuta, alihakikisha tunapata msaada wa kipekee sana. Na wala hatujui, maskini ya Mungu.

Huduma ya afya Tanzania ni pana sana kusema umbebeshe lawama Waziri. Hii Wizara inahitaji efforts za watu wengi hasa Rais mwenyewe. Huku panahitaji budget kubwa sana, ila na sisi nchi ni maskini, na bado vipaumbele vya serikali havieleweki (kwa muda mrefu hatujaweka afya kama kipaumbele). Yeye kama waziri mwenye dhamana, kazi anaifanya sana tu.
Tuna Hela ya kununua goli milioni 10 halafu hatuna Hela ya kupeleka dawa ma hospitalini.
 
Nani yupo nyuma ya huu mchakato mchafu wa kumchafua waziri wa Afya Ummy Mwalimu?

Kwa maoni yangu Waziri Ummy japo sio mhalisia katika sekta ya afya ...yaani sio mtaalamu wa afya lakini amejitahidi sana kuielewa sekta hii.ameitendea haki kwa kadri ya kipaji alichonacho.

Japo naona na napata hisia yupo mtu anayetaka atoke na mtu huyo anampiga majungu kimya kimya lakini pia kwa kuibua habari chonganishi za sekta ya afya akiwa na lengo la kuonesha Waziri hafai.Je mtu huyo ni nani?anataka nini na je anao uwezo wa kuisimamia sekta ya afya kuliko UMMY?

TUJADILI KWA HAKI!!
Hivyo vyeo ni kawaida kupigwa vita kwa Afrika.

Watu mpaka wanarogana kwa uafisa tu itakuwa uwaziri?
 
Nani yupo nyuma ya huu mchakato mchafu wa kumchafua waziri wa Afya Ummy Mwalimu?

Kwa maoni yangu Waziri Ummy japo sio mhalisia katika sekta ya afya ...yaani sio mtaalamu wa afya lakini amejitahidi sana kuielewa sekta hii.ameitendea haki kwa kadri ya kipaji alichonacho.

Japo naona na napata hisia yupo mtu anayetaka atoke na mtu huyo anampiga majungu kimya kimya lakini pia kwa kuibua habari chonganishi za sekta ya afya akiwa na lengo la kuonesha Waziri hafai.Je mtu huyo ni nani?anataka nini na je anao uwezo wa kuisimamia sekta ya afya kuliko UMMY?

TUJADILI KWA HAKI!!
We nae nilikuwa nakuheshimu kumbe mpuuzi Tu

Machawa mna KAZI Sana.

Sasa hiyo 20k unayopewa umsifu Ummy inakusaidia nini?
 
Mtu yoyote anaweza kusema haya. Huu ni uzushi, JK hakuwa na uwezo wa kuinfluence maamuzi ya JPM, kila mtu anajua hilo hata hiyo Ummy anajua kuwa hakuna kosa angefanya kama kumuomba JK amlobby JPM. Acha wivu na husda kwa mwanamke mwenzio. Ukweli hakuna Waziri amewahi kuimudu hii sekta kama Ummy, anabebwa na utendaji wake, rekodi na takwimu ndizo zinazombeba. Aliondolewa hapo wote tunajua Chanjo ya UVIKO-19 ili doda, aliporudi mpk WHO walikubali wenyewe. Huyu mama hata kama hatumpendi tumpe maua yake akiwa hai, tusitake kumtoa kwa kashfa, tumuogope Mungu.
Huyu Ummy amepiga Pesa zaidi ya 1Billion unatetea upuuzi tu
 
Embu tuletee hizo takwimu zinazompaisha huyo Ummy wako. Na sera gani alizo introduce kupata hayo mafanikio.

Matatizo ya afya ni complicated hata huyo Gwajima utegemei ata ya maliza kwa miaka mitano, walau anauelewa mpana wa medical practice, policy/regulations and management kuanzia kwenye zahanati mpaka hospitali za rufaa.

Shida kubwa ya afya ni working culture ya kutofuata miongozo ya afya na Dorothy alikuwa ana expose hayo mambo alipokuwa TAMISEMI kila siku na hata muda mchache alipokuwa waziri. Anahitajika mtu wa kupambana kuona taratibu za practice zinaheshimika na hiyo sio kazi ndogo kuwabadili watu tabia.

Let me tell what Dorothy Gwajima angefanya kama angekuwa waziri kwenye hili sakata la mimba. Badala ya kuzunguka na kwenda vituo ambavyo havina shida na kufanya propaganda huku akificha tatizo. Yeye angewaibukia kituo chenye tatizo na kuanza kuwapiga audit ajiridhishe kama number of staffs wanaotakiwa kuwa shift wote wapo nurses, wakunga, kama wanazidiwa na wajawazito angeomba barua yao iliyoandikwa wizarani kuomba kuongezewa wakunga, angekagua kama wajawazito wanapewa pre-natal care sahihi and so forth; kwa kifupi pangechimbika.

Sina shaka kuna uzembe huko wa ndani based on bad working culture na Dorothy kaonyesha mara kadha kila alipokuwa akiamua kuwapiga audit ya papo kwa hapo iwe inventory control au process za mahabara.

Usicheze na Dorothy kuna siku walitaka kumuongopea dawa hakuna akawaambia subirini mnanisikia tu hamnijui aliwaanzia kwenye order ya dawa na kuanza kupiga audit hadi kwenye remaining stock halafu akawauliza mbona receipts za MSD, issues na inventory hazi match dawa mlizopewa zimeenda wapi. Mwisho anawaambia ‘now you see now you don’t ebu nielezeni dawa ziko wapi hiki sio kitendawili cha Schrödinger’s equation’ tells you she is deeper in quantum physics too (to appreciate her sarcasm you need to understand particles behaviour).

Dorothy Gwajima is something else to appreciate her inabidi uwe na abc za health management.

Kuna siku tena akakuta wagonjwa wanacheleweshewa vipimo wakataka kumuongopea, haya subirini twende kazi akawapiga process audit hadi maabara wenye wakaomba msamaha.

Unataka kumfananisha Dorothy na Ummy; akili zako sio sawa. Ndio afya awamtaki Dorothy kwa sababu awawezi muongopea.
Swadakta umesema kweli
 
Dah, hospital gani Tena kushimiana Hadi simu jamaa! Mimi sijawahi peleka familia yangu serikalini kutokana na kesi Kama hizi ninazosikia au kusoma
Temeke Hospital, Mbagala Zhakiem, Round Table na hospital yoyote ya serikali wana pokonya simu wazazi wengine waficha kiswaswadu anaongelea chooni manesi wasimuone ukiwa na shida kaongee na nesi anapigia ndugu aisee vile hospital nilimfata Dr wangu niliapa sirudi hio clinic nayo majanga matupu labda uonge nesi 2000-3000 utahudumiwa vizuri kwanza hawana muda uhoji maswali hio foleni sasa ya maabara hapana jamani niliapa sitorudi nikazaa Private raha sana unabebembelezwa unanyeyekewa.
 
Waziri Ummy ni genius katika kusimamia wizara za nchi hii. Changamoto anakwamishwa na siasa za hovyo za nchi yetu. Watumishi sasa wananyanyasika sana na bima ya afya
 
Sikatai changamoto zipo ila sio za Ummy. Hao wafawidhi na viongozi wa huko na madaktari wanachukua hatua gani? Umesema hapo juu wanafanya upasuaji vibaya ili warudie wapate hela japo sina hakika, sasa hapa analaumiwaje Ummy na sio hao madaktari ndio wakuchukuliwa hatua?
Huo ufawidhi vituoni ni kazi ya kujitolea tu, Kama unaona hawafai wekeni wanaofaa
 
Ok Ummy amestructure muundo wa Wizara sina haja ya kukufafanulia in details. Unakumbuka alipokua Gwajima alipotuingiza kwenye nyungu, takwimu za afua za UVIKO-19 zilipokwama, Ummy ndie aliyekuja na mikakati ya kuziinua mpk Tanzania tukashika namba 2 Afrika kwa kufanya vizuri. We tukana kwa hasira tu lkn namba mnazisoma.
Chanjo ya COVID nadhani tumetia fora kwa KUPIKA DATA ili kufurahisha Donors 🇹🇿🇹🇿🇹🇿
 
Ummy kwenyr masuala yote ya kupata maokoto ili aneemeke yuko vizuri. Marehemu magufuli alikuja kumshtukia baadae sana kama ni msanii. Alijiweka na watu wa karibu na marehemu magu akijua sifa zake zitamgikia magu and that had worked well for her.

Hizi pesa za uviko zimeliwa haswa na yeye zikiwa chini yake. Hata wakati huu wa SS. Kajiweka na watu wa karibu na dini na network ili mama amkubali.

Lakini yapo mazuri ameyafanya haswa donor funded proposals ila nadhani afya inahitaji kichwa kinhine ili nacho kisukume mbele gurudumu.

NB. Deal ndogo to kwa waziri yeyote ni si chini ya million 500. Si ajabu hawa watu kusomesha watoto wao Braeburn, ISM, IST, Feza, Agha Khan Mombasa moja ya shule la kibepari ukanda huu wa east africa.
 
Nani yupo nyuma ya huu mchakato mchafu wa kumchafua waziri wa Afya Ummy Mwalimu?

Kwa maoni yangu Waziri Ummy japo sio mhalisia katika sekta ya afya ...yaani sio mtaalamu wa afya lakini amejitahidi sana kuielewa sekta hii.ameitendea haki kwa kadri ya kipaji alichonacho.

Japo naona na napata hisia yupo mtu anayetaka atoke na mtu huyo anampiga majungu kimya kimya lakini pia kwa kuibua habari chonganishi za sekta ya afya akiwa na lengo la kuonesha Waziri hafai.Je mtu huyo ni nani?anataka nini na je anao uwezo wa kuisimamia sekta ya afya kuliko UMMY?

TUJADILI KWA HAKI!!
Sukuma gang kazini
 
Chuki binasfi na wivu uliopitiliza dhidi ya huyu mama. Madaktari wanakosea huko na kusababisha madhara kwa wananchi tuhuma analetewa ummy as if yeye ndio yupo Kituoni. Kwenye Hospitali kuna timu za uendeshaji huduma za afya kuanzia mganga mkuu wa wilaya, mkoa, kuna mabaraza ya kitaaluma kuna Idara za Wizarani then ndio aje kuamua yeye wa Mwisho au ORTAMISEMI. Kuna makosa mengine kweli tunaona kabisa hapa kuna udhaifu kwenye mifumo na Mhe. Ummy kweli tunaona amekuwa mstari wa mbele kukemea utendaji mbovu katika Sekta ya Afya. Sasa Watanzania tunataka tupewe sijui Waziri gani aje afit hapo. Kwa Dunia ya sasa hatukupaswa kufanya hivi vitendo vya kumdhoofisha morari Waziri Ummy Mwalimu anachapa kazi nzuri na sisi tunaona. Tuache mambo ya Wivu usiokuwa na tija.
 
Back
Top Bottom