Mwaka 2025 umeisha tunaingia 2026, Utamkumbuka Samia kwa lipi?

Mwaka 2025 umeisha tunaingia 2026, Utamkumbuka Samia kwa lipi?

Na yeye ajiandae kunyea debe The Hague.

Principle of force ni ile ile huwa haibadiliki.

For every action, there's an equal and opposite reaction.

Yangekuwa mauaji ya kimbari, mfano SSH ameua watu wa kabila fulani la Tanzania ingekuwa ni noma kwani hiyo huwa genocide (kimbari) lakini ni kesi ya mauaji ya binadamu (crime against humanity) kuundwa tume kwa kawaida kunaendana na jinai ya mauaji ya aina hiyo.

Inayosubiriwa ni tume itakayotoka aidha AU au huko EU ije ifanye kazi pamoja na tume hii ya SSH.

Kimbari ni balaa. Saddam Hussein alinyongwa, wasaidizi wa Hitler walifia jela, wale wahutu kule Rwanda mpaka kesho wanaendelea kukamatwa na kushtakiwa.

Kesi kule The Hague ni Crime Against Humanity sio Genocide.
 
Wote waliohusika kuua watanzania awe rais, mtoto wake, IGP, Mafwele, RPCs, RCs, watu binafsi, siku ICC ikitoa order hawana pa kujifichia ni pingu tu.
Order ya ICC sio sawa na mtu kununua mchele sokoni kisutu.

Hayo ni masuala ya international law, mwanasheria mkuu ni mtaalam wa sheria za kimataifa.
 
Yangekuwa mauaji ya kimbari, mfano SSH ameua watu wa kabila fulani la Tanzania ingekuwa ni noma kwani hiyo huwa genocide (kimbari) lakini ni kesi ya mauaji ya binadamu (crime against humanity) kuundwa tume kwa kawaida kunaendana na jinai ya mauaji ya aina hiyo.

Inayosubiriwa ni tume itakayotoka aidha AU au huko EU ije ifanye kazi pamoja na tume hii ya SSH.

Kimbari ni balaa. Saddam Hussein alinyongwa, wasaidizi wa Hitler walifia jela, wale wahutu kule Rwanda mpaka kesho wanaendelea kukamatwa na kushtakiwa.

Kesi kule The Hague ni Crime Against Humanity sio Genocide.
Endelea kumdanganya.
 
Order ya ICC sio sawa na mtu kununua mchele sokoni kisutu.

Hayo ni masuala ya international law, mwanasheria mkuu ni mtaalam wa sheria za kimataifa.
Nakukumbusha ukamkumbushe kuwa....

 
Nakukumbusha ukamkumbushe kuwa....

Crimes against humanity zinaruhusu uundwaji wa tume ya uchunguzi.

Hayo ni mauaji sawa na yale yanayotokea dunia nzima, mmoja mwenye bunduki anampiga risasi asiye na silaha.

Marekani kwa siku yanatokea mauaji ya aina hiyo 1600 huwezi kusikia Donald Trump kashtakiwa ICC.

Pale DRC ndani ya wiki mbili wameuliwa wananchi wasio na hatia zaidi ya 2000 huwezi kusikia Tshisekedi kashtakiwa.

Ni aina ya mauaji yenye kuruhusu kuundwa kwa tume na upelelezi kufanyika. Noma ni genocide ile huwa rais hachomoki.
 
Nakukumbusha ukamkumbushe kuwa....

Hayo ya kawaida sana kwa wanasheria, ndio kazi zao.
 
Nimekupa mifano ya Tshisekedi kule DRC wamekufa raia 2000 ndani ya wiki moja, nani utamshtaki nani utamuacha?.
Subiri kesi ianze ndipo utajua hujui, unaona kuua watu elfu 10 kwa siku 3 ni kitu cha kawaida, mwenyewe kajificha anajua akinachoenda kumkuta.
 
Ccm waliyataka wenyewe( bamba,) na wavimbe wapasuke( bamba) acha waisome no hee , ccm imebaki jina ,aliimba capt komba( R.I.P)
 
Ni mengi ya kumkumbuka Rais Samia, nitataja machache, 10 tu kwa umuhimu wa mpangilio wake (1-10):
  • Ni Rais wa kwanza aliyediriki hadharani mbele ya wazee-Dar na taifa lote, kukanusha umiliki wa HATI MILIKI ya nchi hii TZ waliyojitunukia/kuipora TEC kwa miaka mingi na kuirudisha kwa WANANCHI WOTE wa makundi yote. Asante sana Mama.
  • Ni Rais wa kwanza TZ kupokea kijiti toka kwa mtangulizi wake kikatiba baada ya mtangulizi huyo kufariki.
  • Ni Rais aliyeweza kudumisha na kuendeleza amani katika kipindi kigumu cha tukio la kihistoria la kuondokewa na Amir jeshi mkuu. Moshi mwingi ulikuwa ukifukuta, lakini kwa kutumia akili nyingi, busara, elimu, uzoefu akaweza kuiunganisha nchi na utulivu ukapatikana na kutuvusha salama. Ni jambo kubwa sana!
  • Ni Rais wa kwanza aliyetoa tafsiri ya KIBIASHARA, TZ kama nchi isiyofungamana na nchi yeyote katika mwaka 2025 na kuendelea kwa kufungua milango ya kibiashara kwa dunia nzima hususan MASHARIKI YA KATI. Hapa Ma-rais wengi walishindwa, kila wakigusa, waliodhani wana hati miliki na wafuasi wao walipiga kelele sana wakitumwa na wa-magharibi na washiriki wao. Asante mama kwa kutuonyesha njia, milango imefunguliwa.
  • Kaleta amani baada ya jaribio kubwa la 29/10 - 03/11 la kuipundua nchi ya TZ. Lingefanikiwa tungekuwa na Sudan ya pili Afrika. Si hao waliosababisha tu, wala wengine wasiohusika wangekuwa salama. Asante mama.
  • Ni Rais wa kwanza aliyeongeza Pato kubwa la kodi la Taifa, iliyopata kwa miaka mitatu mfululizo. Ni rekodi ambayo hakuna Rais toka Nyerere mpaka Magufuli walioweza kufikia kiwango hicho.
  • Ni Rais aliyeongeza tija katika kilimo kwa kuweka ruzuku katika pembejeo na kutafuta masoko ya mazao ya wakulima. Hii ndio tafsiri halisi ya kumsaidia MNYONGE.
  • Ni Rais wa kwanza aliyetuzawadia miundo mbinu ya kimkakati ambayo haikuwepo TZ kama SGR, bwawa la Nyerere(umeme), vijiji vyote kufikiwa na umeme, n.k. Umeme na usafirishaji ndio viashiria namba 1 vya maendeleo ya nchi.
  • Ni Rais wa kwanza mwenye dhamira ya kweli ya kutuletea aka.. mwali- KATIBA MPYA.
  • Ni Rais wa kwanza aliyetuletea Dira ya maendeleo ya TZ ya miaka 50 nzuri na itayoitoa TZ katika umasikini. Hapa wengi hawajaisoma; pateni muda mkaisome ndio mtatambua umuhimu wa Rais Samia na jinsi anavyohitaji kuikomboa Tanzania. .....NB: kwa wale wanaouliza swali: Kuna anayefahamu, Rais Samia anatupeleka wapi? Isomeni Dira hii, mtapata majibu.
Uuuups. Wewe utakuwa unaishi kwenye Kuta na Ikulu.

Nina wasiwasi kama unaishi na sisi huku kitaani. Umeandika maneno mengi bila kujua nini unaandika.

Mfano.. unaandika Mapinduzi ya nchi ya October 29, unauhakika yalikuwa Mapinduzi ya nchi? Kwamba nchi ingetawaliwa na Kenya ama Uganda ama Burundi ama China? Unauhakika nani alitaka kuipindua nchi, Hadi sasa nani alikuwa kiongozi wa hayo Mapinduzi?.
Acheni kufungiwa akili na Viongozi waliochokwa na wananchi. Hizo zilikuwa hasira za wananchi kuuchoka uongozi, ila uongozi unatumia nguvu kuwatawala wananchi. Wewe na akili Yako unaona Mapinduzi.
 
Kipekee nitamkumbuka kuwa ndiye Rais wa kwanza Tanzania kujiapisha kwenye Barracks za kijeshi.

Ni Rais wa kwanza Tanzania kuwekwa kwenye group linalowania tuzo ya Kiongozi Jeuri wa Mwaka, Tyrant of the Year.

Ni Rais wa kwanza kumaliza siku 100 zake za kwanza akiwa amejificha.

Ndiye Rais ambaye hakuwashukuru waliomchagua baada ya uchaguzi.

Kalishukuru Jeshi la Wananchi, Jeshi la Polisi na Tume ya Uchaguzi kawaacha wananchi waliomchagua.

Ni Rais wa kwanza Tanzania kukataliwa na jumuia nyingi za kimataifa duniani.

Ni Rais aliyejitangaza anayeongoza kwa mkono wa chuma, anayechukiwa na wananchi wake walio wengi.
99.03
 
Back
Top Bottom