Mwaka mmoja bila Magufuli: Jimbo Kuu Katoliki Mwanza kuongoza Misa ya maombezi yake

Mwaka mmoja bila Magufuli: Jimbo Kuu Katoliki Mwanza kuongoza Misa ya maombezi yake

Mhashamu Baba Askofu Mkuu Renatus Nkwande wa Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza anawaalika waamini na watu wote wenye mapenzi mema katika adhimisho la Misa Takatifu ya kumuombea pumziko la milele mbinguni Hayati John Pombe Joseph Magufuli.

Misa hii takatifu itafanyika Jumapili ya Machi 20 katika viwanja vya madhabahu ya Bikira Maria Malkia wa Kawekamo kuanzia saa nne kamili asubuhi.

Aidha, Mhashamu Baba Askofu Mkuu Renatus Nkwande anatukumbusha kumuenzi Hayati Magufuli kwa kuwa Wazalendo wa kweli, kudumisha amani, undugu na maendeleo ya taifa kwa ujumla.

Hayati Magufuli apumzike kwa amani mbinguni.

View attachment 2147385
Tupo pamoja nitakuwepo
 
Haha... Waliokuwa wanaishi kiwiziwizi walikuwa na hali mbaya sana kipindi cha Magufuli. Ni haki wameshindwa ku-move on... Na bado.
Wazazi wa Ben Saanane ilikuwa inaishi kiwiziwizi? Wata move on vipi mwanao hajulikani alipo?
Mke wa Lissu kila anapomuangalia mumewe yale mavyuma yaliomjaa mwili mzima na makovu yale ata move on vipi kirahisirahisi?
Je familia ya Azory Gwanda wanaweza ku move on kirahisi?
Lile li Magu lilikuwa ni shetani flani.
 
Hata wewe umefaidika
1)hospital
2)mashule na madawati
3) elimu bure
4)alitoa vehicle na stiker za nenda kwa usalama
5)machinga na mama lishe
6)mbolea bei chini
7)SGR
8)bwawa la nyerere ambalo linapigwa zengwe
9)na mengine ongezea mwenyewe

HIvyo vyote nimevipata hata kabla hajawa rais. Nimezaliwa na kukulia hapa Dar hizo huduma zote zipo tena nazipata kwa kulipia.
 
Wazazi wa Ben Saanane ilikuwa inaishi kiwiziwizi? Wata move on vipi mwanao hajulikani alipo?
Mke wa Lissu kila anapomuangalia mumewe yale mavyuma yaliomjaa mwili mzima na makovu yale ata move on vipi kirahisirahisi?
Je familia ya Azory Gwanda wanaweza ku move on kirahisi?
Lile li Magu lilikuwa ni shetani flani.
Watoto wa mwangosi wanateseka hawana baba alikufa kifo cha kinyama utumbo nje kama si binadamu ,Dr ulimboka alipata maumivu makali kung'olewa meno bila gazi,wale waliomzomea malaika wenu mbeya hawajulikani walipo.Hilo hamlioni unaona ya JPM tu acha bias naye atakuwa wapi?
 
HIvyo vyote nimevipata hata kabla hajawa rais. Nimezaliwa na kukulia hapa Dar hizo huduma zote zipo tena nazipata kwa kulipia.
Vilikuwepo kwa uchache yeye kaviongeza,miundo mbinu yote Dar ukigusa lazima ukute sahihi ya JPM kwenye mkataba karibu 90℅ sasa hapo utasemaje?.najuwa unamkubali kiani hutaki kukiri hadharani
 
Wanaenda kinafiki tu ila mioyo yao haiko hapo na believe me Mungu alie hai atadhihirisha imagine alitaka kumuua lisu kwa kumpiga risasi 36 na kama haitoshi akakataa watu wasimuombee Mungu alivyofundi akaliuwa lenyewe kabla ya lisu leo mnaliombea jitu liko motoni.
Ile takataka hata mimi ikirudi naitandika risasi

Sent from my SM-T295 using JamiiForums mobile app
 
Watoto wa mwangosi wanateseka hawana baba alikufa kifo cha kinyama utumbo nje kama si binadamu ,Dr ulimboka alipata maumivu makali kung'olewa meno bila gazi,wale waliomzomea malaika wenu mbeya hawajulikani walipo.Hilo hamlioni unaona ya JPM tu acha bias naye atakuwa wapi?
Acha kutetea kutetea ujinga, hayo pia unaweza kuyafungulia uzi na tutachangia vilevile.
Matukio yale yalikuwa ni mabaya na hayafai, yanapaswa kukemewa pia lakini hilo halisafishi ukatili na uuaji uliofanywa wakati wa utawala wa Magu.
 
Nimeondokewa na ndugu zangu wengi sijawahi kuota kama wataondoka huyu mwamba niliota ameondoka
niliamka nikahuzunika sana lakin nikasema hii haitakuwa kwel na kumuomba Mungu isiwe kweli hiyo ni siku chache
tu baada ya kifo cha kijazi kabla ya rumours za twitter.
Usiku wa trh 17 mtu amabye nilikuwa nampasha habari za Magufuli ambaye ni jirani yangu akanifuata nyumbani kuniambia
Magufuli ameondoka ndipo nilpoikumbuka ile ndoto na nikasema jina la bwana lihimidiwe amina.
Licha ya kufiwa na wapendwa wengi ikiwemo ndugu wa karibu wenye mchango wa moja kwa moja kwenye furaha yangu ni kiri
kwamba Magufuri ameniuma kuliko mtu mwingine yeyote.
Huwa nakumbuka kauli yake moja akisema yeye ni yohana mbatizaji amekuja kuandaa njia yupo anaekuja naamini punde aliyetabiriwa na Magufuri
atakuja tena kutuoa utumwani na kutupeleka kanani.
Hakika wengi tuliumizwa na kifo cha Magufuli.
 
Wazazi wa Ben Saanane ilikuwa inaishi kiwiziwizi? Wata move on vipi mwanao hajulikani alipo?
Mke wa Lissu kila anapomuangalia mumewe yale mavyuma yaliomjaa mwili mzima na makovu yale ata move on vipi kirahisirahisi?
Je familia ya Azory Gwanda wanaweza ku move on kirahisi?
Lile li Magu lilikuwa ni shetani flani.
Tukiwaambia mtupe uthibitisho kuwa Magufuli alimuua Ben Saanane, alimpiga risasi Tundu Lissu na alimpoteza/kumuua Azory Gwanda mnaingia mitini. Hebu tuthibitishie hizi tuhuma.
 
Vilikuwepo kwa uchache yeye kaviongeza,miundo mbinu yote Dar ukigusa lazima ukute sahihi ya JPM kwenye mkataba karibu 90℅ sasa hapo utasemaje?.najuwa unamkubali kiani hutaki kukiri hadharani

Dar hapa miundombinu ilikuwepo kwa uchache miaka 6 iliyopita? Labda hujui unaongea nini Boss
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Wewe kila siku unalia na wizi wa kula!

Sikia mkuu pamoja na kwamba hayupo ila hata 2025 utakuja na ngonjera hii hii ya wizi wa kura!

Sent from my SM-T295 using JamiiForums mobile app

Kwa hiyo nikilia hiyo 2025 itafuta huu wizi wake?
 
Tukiwaambia mtupe uthibitisho kuwa Magufuli alimuua Ben Saanane, alimpiga risasi Tundu Lissu na alimpoteza/kumuua Azory Gwanda mnaingia mitini. Hebu tuthibitishie hizi tuhuma.

Udhibitishiwe ww kama nani? Huyo ndio ukweli na hakuna chombo cha kukubali kudhibitisha hilo hapa nchini. Lakini kikija chombo huru toka nje, ndani ya nusu ushahidi wote utakaa hadharani.
 
Udhibitishiwe ww kama nani? Huyo ndio ukweli na hakuna chombo cha kukubali kudhibitisha hilo hapa nchini. Lakini kikija chombo huru toka nje, ndani ya nusu ushahidi wote utakaa hadharani.
Hamna uthibitisho kwa kuwa ni stori za kutunga za mafisadi, mabeberu na vibaraka wao.
 
Hamna uthibitisho kwa kuwa ni stori za kutunga za mafisadi, mabeberu na vibaraka wao.

Udhibitisho upelekwe wapi wakati mamlaka za kudhibitisha zina hofu na hayo madaraka. Au unadhani ukisema tulete ushahidi ndio inaondoa ukweli? We kesha hapa, shinda hapa huo ndio ukweli ambao huwezi kuubadili kwa mahaba yako kwake.
 
Back
Top Bottom