Mwaka mmoja wa Rais Samia na RC Kafulila ukusanyaji mapato Simiyu sasa ni mara tatu zaidi, maajabu ni Itilima kukusanya TZS 1.4BL

Wanafiki wakubwa nyie, mnatutangazia makusanyo makubwa lakini kila siku mnakopa na hali ya maisha inazidi kuwa ngumu, hizo pesa zinafanya kazi gani kama siyo propaganda?
 
Haya mapato yametokana na uchimbaji dhahabu na trickle down effect zake haimaanishi mtaka alishindwa kukusanya.
 
Nyie kila kitu Mbowe, Kafulila mbona alitokea NCCR,
Kichwa kizito baada ya kuzinguana na zito akiwa naibu katibu alimzingua kafulila mchakato wa ndani wa uchaguzi akasepea nccr na akaibuka mshindi ubunge jimboni
 
Wonderful Rais Samia
 
Rais kasema kila mtu ametolewa kwa sababu kadha wa kadha ila wengine waliotolewa kwenye u RC atawatumia kwingine so nadhani Kafulira na Gabriel wanaweza pewa hata ubalozi.
 
Niko simiyu, kafulila Yuko vizuri sana , Ni mtu ambaye ni mchapa kazi , Hana majigambo Kama alivyokuwa mtangulizi wake Bwana mtaka chui aliyejificha kwenye ngozi ya Usabato.

Hongera sana kafulila, uko vizuri sana my brother from another mother!
Mtaka ni chui kvp
 
Yaani 1.4B ni maajabu kwa Halmashauri kukusanya na humo kuna ada za shule na cost sharing za hospitali? shame on them
Halmashauri zinatofautiana wigo wa mapato, kwa halmashauri kama itilima kukusanya above 1bil inastahili pongezi
 
Kazi ni nzuri sana Rais Samia, we love you,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…