Mwalimu Nyerere aliona mbali madhara kuruhusu kabila kubwa kushika madaraka ya Urais

Mwalimu Nyerere aliona mbali madhara kuruhusu kabila kubwa kushika madaraka ya Urais

Makabila makubwa si tatizo ikiwa katiba inakidhi vigezo.
Katiba iliyopo inampa rais ubabe na anaweza kujaza kabila lake kwenye utawala.
Chama kina nafasi kubwa kuliko wananchi na ujinga ni zaidi kuliko werevu
Haya ndo matatizo makubwa na si makabila.

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
kweli
 
Sio kila wazo nila kuandika JF.mengine yasio na kichwa wala miiguu kama hili niya kuachana nayo tu.
 
Nadhani kwa wakati ule inawezekana ilikuwa na mantiki, ila binafsi sioni kama lina mashiko eti Rais asiwe Mnyakyusa, Mchaga, Mhehe, Mngoni au kabila lolote kubwa, hayo ni mawazo mgando
Alimaanisha makabila yenye ubinafsi kama wachaga! Wasukuma ni generous sana majority of them na wana misimamo haswaa!
 
Kabila kubwa Tanzania ni wasukuma, there is no way ukawaondoa kwenye mfumo wa uongozi wa nchi hii, wako kila mahala.

Wasuluma ni karibu robo ama theluthi ya watanzania wote maana wanakaa mikoa ya Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Mara, Tabora, Katavi, Kagera, Kigoma, Singida na kwenda hadi huko Mbeya.

Hao tu peke yao wakiamua wanaweza ku-influence siasa za nchi hii.

Sisi ambao sio wasukuma tukubali tu kwamba hakuna namna ya hao jamaa kua wengi serikalini hata kama rais asingekua Magufuli.

Wewe kwako Nyerere angesema upigwe miti ungekubali kisa kasema Nyerere, yani wewe Nyerere ni kila kitu, chochote alichokisema ni asilimia mia. Halafu hayo Nyerere aliyasema wapi?
Ndiyo wanaondoka mdogomdogo tu mwisho mtajikuta mmebakia kona ya bwiru tu
 
Ni mpumbafu tu, Unguja kuna wasukuma kama wote na wengine wamekuwa viongozi ndani ya serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakiwa wazaliwa na wahamaji.
 
Kati ya vitu ambavyo nyerere alivipinga sana ni pamoja na kabila kubwa kushika madaraka ya urais na hili alikuwa na sababu kubwa sana ambazo tumejidhihirisha katika kipindi cha awamu ya tano

Nadhani wahusika mmejifunza pia na hamta rudia tena makosa mliyo yafanya miaka mitano iliyo pita kwa sababu madhara yaliyo tokana na hilo bado yapo na yanaendelea kuitesa serikali ya awamu ya sita , nadhan wenye uelewa mzuri wameelewa.

Logout.
Shida siyo kabila shida ni mtu ambaye alipewa
 
Kati ya vitu ambavyo Hayati Nyerere alivipinga sana ni pamoja na kabila kubwa kushika madaraka ya urais na hili alikuwa na sababu kubwa sana ambazo tumejidhihirisha katika kipindi cha awamu ya tano.

Nadhani wahusika mmejifunza pia na hamtarudia tena makosa mliyoyafanya miaka mitano iliyopita kwa sababu madhara yaliyotokana na hilo bado yapo na yanaendelea kuitesa Serikali ya awamu ya sita, nadhani wenye uelewa mzuri wameelewa.

Logout.
Lete ushahidi wa kauli yako.

Una video yoyote Nyerere akiyasema haya?
 
Yule mtu alivyokuwa muongo muongo sijui kama alikuwa msukuma kweli.
 
Shida siyo kabila shida ni mtu ambaye alipewa
Hivi kwa akili yao hawa unafikiria nchi hii Msukuma asiwe kwenye uongozi wakati amepiga shule vizuri na mchapakazi! Karibia robo ya watanzania wananasaba ya usukuma na unyamwezi unaweza kuwaepuka vipi?
 
Alipewa mtu wa hovyo ndiyo maana watu wanachukia
 
Alipewa mtu wa hovyo ndiyo maana watu wanachukia
Sema wewe na wazazi wako! Usiwasemee watanzania wote! Pia nioneshe nani alishapendwa na watu wote? Hata wewe hapo hupendwi na watu wote kwa hiyo sio ajabu!
 
Kweli aisee. Kipindi cha mwendazake ghafla Wa-push wote wakawa wanaccm. Unajua nilishangaa sana.
Na wakafanikiwa kumfanya mwendazake kuwa mungu wao.

Na mpaka sasa hawaamini kadedi, wanaamini yuko bize anawaongoza malaika
 
Wasukuma tunajifahamu kwa ukarimu na upole.
Sasa niambie kama yule jamaa alikuwa msukuma.
Tulilishwa za porini!
Usikariri ndo maana mnasema hapa wachaga wezi nani alikwambia wachaga wote wezi? Au wahaya wanamisifa nani alikwambia wote wako hivo? Ulishawahi kukaa na wasukuma au unawachukulia poa kwa jinsi wanavyokandamiza wakiwa wanaongea? Kila jamii inaaina mbalimbali ya watu! By the way Magufuli alikiwa mtu mzuri tu kama unatimiza mambo yako kisawasawa!
 
Msukuma ana tabia za kiskuma, mtu asiye msukuma ana tabia zisizo za kisukuma.
Kati kati hapo jaza mwenyewe!
 
Back
Top Bottom