Mwalimu Nyerere: Mafanikio, mapungufu na misingi ya taifa letu.

Mwalimu Nyerere: Mafanikio, mapungufu na misingi ya taifa letu.

ShesRise_1

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2025
Posts
22,235
Reaction score
51,111
Happy Nyerere day Tanzania 🇹🇿

Leo ikiwa ni kumbukumbu ya kifo cha muasisi wa taifa hili, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyezaliwa tarehe 13 Aprili 1922 na kufariki tarehe 14 Oktoba 1999, ni vyema tukajikumbusha historia yake na mchango wake katika taifa hili.

Nyerere wakati anafariki wengine ndiyo tunazaliwa au ni wadogo lakini historia yake inaishi na itaendelea kuishi kutoka kizazi hadi kizazi

Nyerere anakumbukwa kama mpigania uhuru aliyeshirikiana na wazalendo wengine wa taifa hili kupigania uhuru wa Tanganyika kutoka kwa wakoloni bila kumwaga damu

Mwaka 1954, alishiriki kuasisi chama cha TANU (Tanganyika African National Union), kilichokuwa mstari wa mbele katika harakati za kudai uhuru
Hatimaye, Tanganyika ilipata uhuru tarehe 9 Desemba 1961, na Nyerere akawa Waziri Mkuu wa kwanza

Mwaka 1962 akawa Rais wa kwanza wa Tanganyika, na mwaka 1964 akawa Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (Hapa kwenye muungano hapa🤔)

Tujikumbushe baadhi ya mambo aliyoyafanya enzi za uhai wake:

1. Kupigania uhuru: Aliongoza harakati za kisiasa zilizosaidia Tanganyika kupata uhuru mwaka 1961
2. Kuimarisha umoja wa kitaifa: Alihimiza umoja wa Watanzania bila kujali makabila yao na alikuza matumizi ya Kiswahili kama lugha ya taifa
Mf: Akikataza kuulizana maswali ya ukabila akilenga kuliunga taifa

3. Kuunganisha Tanganyika na Zanzibar: Alishiriki katika kuasisiwa kwa Muungano wa mwaka 1964.(Muungano🤔)

4. Ujamaa na Kujitegemea: Mwaka 1967, alitangaza Azimio la Arusha lililosisitiza usawa, kujitegemea na umiliki wa pamoja wa baadhi ya rasilimali za uzalishaji

5. Kupanua elimu na huduma za jamii: Serikali yake iliendeleza juhudi za kupanua upatikanaji wa elimu na huduma za afya kwa wananchi

6. Kusaidia ukombozi wa Afrika: Aliunga mkono harakati za ukombozi wa nchi nyingine za Afrika zilizokuwa bado chini ya ukoloni au tawala za kibaguzi.

7. Kuachia madaraka kwa hiari: Mwaka 1985, alistaafu urais na kumwachia madaraka Ali Hassan Mwinyi Mzee wa Rukusa

Lakini pamoja na yote hayo, kuna maswali ambayo tunapaswa kujiuliza kama taifa

Je, Nyerere alikuwa mtakatifu?

Je, kwa sababu alikuwa Baba wa Taifa, tunapaswa kuona kila alichofanya kuwa sahihi bila kukikosoa?

Unadhani Nyerere na wenzake walijenga misingi bora ya taifa hili, au kuna mapengo makubwa yaliyoachwa ambayo hadi leo yanaendelea kuliathiri taifa letu?

Tukiangalia misingi ya demokrasia, uchumi, elimu na haki za wananchi, je, tunaweza kusema kwamba kila uamuzi uliofanywa wakati wa uongozi wake ulikuwa sahihi?

Na kuhusu chama cha TANU alichoshiriki kukiasisi mwaka 1954, je, kuanzishwa kwake na mfumo wa kisiasa uliofuata vilikuwa sahihi kwa mazingira ya wakati huo?

Na Je kuanzishwa kwa TANU inaweza kua ni chanzo cha kufika hapa tulipo kwenye maswala ya siasa?

Tafadharini wana jukwaa hili chonde chonde lengo si kumdharau Nyerere wala kubeza mchango wake katika taifa sote tunajua nafasi yake na ndio maana leo tupo hapa kuzungumzia na kujadili pamoja

Lengo ni kujiuliza maswali kuchambua historia yetu kwa upana na kutofautisha kati ya heshima kwa viongozi wetu na uwezo wa kuhoji maamuzi yao

Historia haipaswi kuwa sehemu ya kusifia pekee inapaswa pia kuwa nafasi ya kujifunza kutafakari na kujenga taifa bora zaidi.

Karibu kupongeza
Karibu kukosoa
Karibu kujenga hoja
karibu kutoa maoni yako

Tujadili hapa ni kitu gani hasa ambacho Nyerere alifanya ungetamani kiendelezwe au Ni kitu gani ungependa kipitiwe upya

Karibuni Great Thinkers. 🫡🇹🇿

ShesRise_1 ✋️
 
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Baba wa Taifa 🇹🇿
 
Attachments

  • 2026_10_14_09.30.09.jpg
    2026_10_14_09.30.09.jpg
    54.4 KB · Views: 9
Mimi ni mfuasi wa Mwalimu Nyerere. Kwa mara ya kwanza nilihudhuria mkutano wake wa hadhara Mang'ula Kilombero mwaka 1991! Nakumbuka nilitokea hadi kwenye mkanda wa video uliorekodiwa siku ile.

Ana mazuri yake mengi kwenye suala zima la uzalendo kwa nchi, mapambano dhidi ya haki na usawa, kuhamasisha umoja na mshikamano, nk.

Lakini pia ana mapungufu yake mfano sera yake ya Ujamaa na Kujitegemea ilizalisha matatizo mengi kwenye jamii, kuiunganisha Tanganyika na Zanzibar kwenye Muungano wenye kero nyingi, kutuletea Katiba ya 1977 na pia CCM kuifanya kuwa chama dola kupitia hiyo Katiba, nk.
 
Kama naweza pata mda wa KUTOA hukumu kwa mtuhumiwa aitwae nyerere NI kunyongwa Hadi kufa kwa kosa la kulazimisha CCM iendelee kutawala wakati watanzania kwa wingi wao mwaka 95 walikataa kata kata CCM kurudi ikuru.
Haya mambo ya kung'ang'ania madaraka kumbe sio ya leo

Unadhani huo mwaka wa 95 wananchi walitaka nani ndio ashike kijiti au Ni Mrema?
 
1. Mambo ya uhuru wa nchi nyingine kama huko South Africa, Msumbiji, Zimbabwe na Angola

2. Siasa za Uganda mpaka ikapelekea vita vya 1978

3. Kuunganisha Tanganyika na Zanzibar.
Ndio kusema wema ulizidi uwezo
Wakati wa ku focus na nyumbani akaenda kutatua migogoro ya majirani?
Mf: Siasa za Uganda si ndio mkuu?

Usinichoke !
 
Mimi ni mfuasi wa Mwalimu Nyerere. Kwa mara ya kwanza nilihudhuria mkutano wake wa hadhara Mang'ula Kilombero mwaka 1991! Nakumbuka nilitokea hadi kwenye mkanda wa video uliorekodiwa siku ile.
hongera sana mkuu
Ana mazuri yake mengi kwenye suala zima la uzalendo kwa nchi, mapambano dhidi ya haki na usawa, kuhamasisha umoja na mshikamano, nk.
ni kweli kabisa
Lakini pia ana mapungufu yake mfano sera yake ya Ujamaa na Kujitegemea ilizalisha matatizo mengi kwenye jamii, kuiunganisha Tanganyika na Zanzibar kwenye Muungano wenye kero nyingi, kutuletea Katiba ya 1977 na pia CCM kuifanya kuwa chama dola kupitia hiyo Katiba, nk.
Hapa mimi naona ndio jinamizi lilipo
katiba swala la muungano💔
 
Ndio kusema wema ulizidi uwezo
Wakati wa ku focus na nyumbani akaenda kutatua migogoro ya majirani?
Mf: Siasa za Uganda si ndio mkuu?

Usinichoke !
Ni wema uliozidi uwezo, kuwa idealistic sana na pia kukosa watu wenye uwezo wa kiakili wa kutosha ku challenge mambo yake mengi. Tanzania ilitakiwa iwe na kina Oscar Kambona kama 20 hivi, bahati mbaya aliziungukwa zaidi na Waswahili.
 
Alizungukwa na watu wasio na uwezo mkubwa kiakili?
Au walimuogopa ?
 
Hii ni sawa kweli kuzidisha mahaba kwa watu baki?
Anajua kwa usahihi zaidi ni yeye huenda alikua anafanya kwa mashinikizo kutoka mashirika ya kijasusi kutoka nje maana Nyerere alisapoti mataifa mengi ya Africa kupata uhuru wakati ambao dunia ilikua kwenye Cold War na wakati huo covert operation zilikua nyingi sana.
Hivi nchii inafaa kuendeshwa kama familia ?
Wakati wa utawala wake aliruhusu mijadala kwa sehemu, aliruhusu watendaji wake kukosoana Ila waliojaribu kumkosoa yeye walikiona cha mtema kuni.
 
Nyerere katuachia shetani CCM dude linalomaliza nchi yetu limeuza KILA kitu madini bandali migodi mito na maziwa vyote vimeuzwa mtanzania ukihoji vitu hivi unatekwa na kupotezwa CCM NI lishetani
Sidhani kama ni sahihi kumlaumu Nyerere kwa haya yanayo tokea sasa hivi

Naamini lau kwamba angekuwa hai leo hii haya yasingetokea kabisa,tulimuona akiita press conference na kuzungumzia mambo mbali mbali ambayo alidhani yanapaswa kurekebishwa

Mfano alikemea vikali maswala ya rusha pale ambapo rushwa ilikuwa inaonekana wazi wazi

Na alisema wazi nchi hii inatakiwa ipate kiongozi ambaye akisema na akionekana tu kwa muonekano wake kwamba anapinga rushwa

Kwahiyo kumuhukumu mndewa Nyerere kwa makosa ya watangulizi wake sio sahihi kabisa
 
Anajua kwa usahihi zaidi ni yeye huenda alikua anafanya kwa mashinikizo kutoka mashirika ya kijasusi kutoka nje maana Nyerere alisapoti mataifa mengi ya Africa kupata uhuru wakati ambao dunia ilikua kwenye Cold War na wakati huo covert operation zilikua nyingi sana.
Ooh Shukran sana mkuu
Huwenda kulikua na shinikizo
Na ubaya hayupo tungemuuliza
Wakati wa utawala wake aliruhusu mijadala kwa sehemu, aliruhusu watendaji wake kukosoana Ila waliojaribu kumkosoa yeye walikiona cha mtema kuni.
Waliomkosoa walikiona cha mtema kuni (Ama kweli vya kurithi vinazidi)
 
Ooh Shukran sana mkuu
Huwenda kulikua na shinikizo
Na ubaya hayupo tungemuuliza

Waliomkosoa walikiona cha mtema kuni (Ama kweli vya kurithi vinazidi)
Kuna sheikh mmoja wakati wa kudai uhuru.
Oscar Kambona.
Kuna mzee mmoja huko Iringa na degree zake saba.

...wanamjua vizuri Nyerere.
 
Back
Top Bottom