Mwalimu Nyerere: Mafanikio, mapungufu na misingi ya taifa letu.

Sidhani kama ni sahihi kumlaumu Nyerere kwa haya yanayo tokea sasa hivi

Naamini lau kwamba angekuwa hai leo hii haya yasingetokea kabisa,tulimuona akiita press conference na kuzungumzia mambo mbali mbali ambayo alidhani yanapaswa kurekebishwa

Mfano alikemea vikali maswala ya rusha pale ambapo rushwa ilikuwa inaonekana wazi wazi

Na alisema wazi nchi hii inatakiwa ipate kiongozi ambaye akisema na akionekana tu kwa muonekano wake kwamba anapinga rushwa

Kwahiyo kumuhukumu mndewa Nyerere kwa makosa ya watangulizi wake sio sahihi kabisa
Nyerere hawezi kukwepa lawama licha kua ana mengi mazuri !
 
Kwa upande wangu huyu mndewa kama binadamu au viongozi wengine popote pale duniani ana mazuri yake na mabaya yake,kwahiyo hakuwa mtakatifu

Na kizuri zaidi kabla hajafa alikiri kwamba kuna mambo mabaya aliyafanya kwenye uongozi wake,na alijoke kwamba badala ya watu kuiga mazuri yake na kuyafanyia kazi kinyume chake wanaiga hata mabaya yake

Sasa kwa upande wangu kuna mazuri kadhaa ambayo huyu mndewa ameyafanya na anahitaji pongezi kwa hilo

Mosi,azimia la Arusha,pamoja na mambo mengine hapa ndio maadili ya viongozi yalipewa uzito mkubwa sana,ikiwemo kiongozi asijihusishe na mambo mengine nje ya siasa,ikiwemo kumiliki mali au kuwa mfanya biashara

Hapa kiongozi hakuwa na tamaa ya kujilimbikizia mali,uongozi ulikuwa kwa ajili ya kuwahudumia watu,wote tunajua baada ya kuanzishwa azimia la Zanzibar basi rushwa sasa na kujilimbikizia mali na ufisadi umekuwa sehemu ya maisha yetu ya kila siku

Viongozi wamejawa na tamaa ya kuhodhi mali na kujinufaisha wao binafsi

Lingine ambalo ni zuri ni kujenga umoja wa kitaifa,leo hii tupo proud hapa Tanzania kwamba wote ni wamoja,hakuna kuangaliana huyu ni kabila gani au anatoka wapi, tunatambuana kwa utanzani wetu kupitiia lugha yetu adhimu kabisa Kiswahili,kwahiyo katika eneo hili napo kafanikiwa sana
 
Nyerere katuachia shetani CCM dude linalomaliza nchi yetu limeuza KILA kitu madini bandali migodi mito na maziwa vyote vimeuzwa mtanzania ukihoji vitu hivi unatekwa na kupotezwa CCM NI lishetani
Ukiondoa madini ni kitu gani hapo mtanzania anaweza kukitumia kununua gari au bunduki ujerumani? Mito? Maziwa? Bandari?

Bandari ni kama stendi ya meli mkuu zikiingia landcruiser kutoka ujerumani zilizo agizwa na mchimba madini wa chunya tunazikatia kodi hapo. Na dhahabu ya huyu bwana wa chunya inaenda ujerumani (utajiri una flow from Chunya to ujerumani).

UChumi hauhitaji hasira mkuu.

Nionyeshe bidhaa zinazotoka Tanzania kwenda ujerumani (made in Tanzania) nikuonyeshe marcesdez benz kitoka ujerumani hapa chunya

Ukiisha elewa ndio utajua kwanini ulipewa uhuru bila kumwaga damu

Na ukae ukijua CHADEMA wakishika nchi kodi zipo pale pale, polisi wapo pale pale na jeshi ni lile lile na pesa za kujenga bara bara utatoa wewe na sio wao kwa sababu wao wanakutegemea wewe utoe kodi ndio wajenge

Suluhisho ni viwanda, viwanda, viwanda, viwanda
 
Kwa upande wangu huyu mndewa kama binadamu au viongozi wengine popote pale duniani ana mazuri yake na mabaya yake,kwahiyo hakuwa mtakatifu

Na kizuri zaidi kabla hajafa alikiri kwamba kuna mambo mabaya aliyafanya kwenye uongozi wake,na alijoke kwamba badala ya watu kuiga mazuri yake na kuyafanyia kazi kinyume chake wanaiga hata mabaya yake

Sasa kwa upande wangu kuna mazuri kadhaa ambayo huyu mndewa ameyafanya na anahitaji pongezi kwa hilo

Mosi,azimia la Arusha,pamoja na mambo mengine hapa ndio maadili ya viongozi yalipewa uzito mkubwa sana,ikiwemo kiongozi asijihusishe na mambo mengine nje ya siasa,ikiwemo kumiliki mali au kuwa mfanya biashara

Hapa kiongozi hakuwa na tamaa ya kujilimbikizia mali,uongozi ulikuwa kwa ajili ya kuwahudumia watu,wote tunajua baada ya kuanzishwa azimia la Zanzibar basi rushwa sasa na kujilimbikizia mali na ufisadi umekuwa sehemu ya maisha yetu ya kila siku

Viongozi wamejawa na tamaa ya kuhodhi mali na kujinufaisha wao binafsi

Lingine ambalo ni zuri ni kujenga umoja wa kitaifa,leo hii tupo proud hapa Tanzania kwamba wote ni wamoja,hakuna kuangaliana huyu ni kabila gani au anatoka wapi, tunatambuana kwa utanzani wetu kupitiia lugha yetu adhimu kabisa Kiswahili,kwahiyo katika eneo hili napo kafanikiwa sana
Tunabuguana kwa vyama zaidi
 
Happy Nyerere day Tanzania 🇹🇿

Leo ikiwa ni kumbukumbu ya kifo cha muasisi wa taifa hili, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyezaliwa tarehe 13 Aprili 1922 na kufariki tarehe 14 Oktoba 1999, ni vyema tukajikumbusha historia yake na mchango wake katika taifa hili.

Nyerere wakati anafariki wengine ndiyo tunazaliwa au ni wadogo lakini historia yake inaishi na itaendelea kuishi kutoka kizazi hadi kizazi

Nyerere anakumbukwa kama mpigania uhuru aliyeshirikiana na wazalendo wengine wa taifa hili kupigania uhuru wa Tanganyika kutoka kwa wakoloni bila kumwaga damu

Mwaka 1954, alishiriki kuasisi chama cha TANU (Tanganyika African National Union), kilichokuwa mstari wa mbele katika harakati za kudai uhuru
Hatimaye, Tanganyika ilipata uhuru tarehe 9 Desemba 1961, na Nyerere akawa Waziri Mkuu wa kwanza

Mwaka 1962 akawa Rais wa kwanza wa Tanganyika, na mwaka 1964 akawa Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (Hapa kwenye muungano hapa🤔)

Tujikumbushe baadhi ya mambo aliyoyafanya enzi za uhai wake:

1. Kupigania uhuru: Aliongoza harakati za kisiasa zilizosaidia Tanganyika kupata uhuru mwaka 1961
2. Kuimarisha umoja wa kitaifa: Alihimiza umoja wa Watanzania bila kujali makabila yao na alikuza matumizi ya Kiswahili kama lugha ya taifa
Mf: Akikataza kuulizana maswali ya ukabila akilenga kuliunga taifa

3. Kuunganisha Tanganyika na Zanzibar: Alishiriki katika kuasisiwa kwa Muungano wa mwaka 1964.(Muungano🤔)

4. Ujamaa na Kujitegemea: Mwaka 1967, alitangaza Azimio la Arusha lililosisitiza usawa, kujitegemea na umiliki wa pamoja wa baadhi ya rasilimali za uzalishaji

5. Kupanua elimu na huduma za jamii: Serikali yake iliendeleza juhudi za kupanua upatikanaji wa elimu na huduma za afya kwa wananchi

6. Kusaidia ukombozi wa Afrika: Aliunga mkono harakati za ukombozi wa nchi nyingine za Afrika zilizokuwa bado chini ya ukoloni au tawala za kibaguzi.

7. Kuachia madaraka kwa hiari: Mwaka 1985, alistaafu urais na kumwachia madaraka Ali Hassan Mwinyi Mzee wa Rukusa

Lakini pamoja na yote hayo, kuna maswali ambayo tunapaswa kujiuliza kama taifa

Je, Nyerere alikuwa mtakatifu?

Je, kwa sababu alikuwa Baba wa Taifa, tunapaswa kuona kila alichofanya kuwa sahihi bila kukikosoa?

Unadhani Nyerere na wenzake walijenga misingi bora ya taifa hili, au kuna mapengo makubwa yaliyoachwa ambayo hadi leo yanaendelea kuliathiri taifa letu?

Tukiangalia misingi ya demokrasia, uchumi, elimu na haki za wananchi, je, tunaweza kusema kwamba kila uamuzi uliofanywa wakati wa uongozi wake ulikuwa sahihi?

Na kuhusu chama cha TANU alichoshiriki kukiasisi mwaka 1954, je, kuanzishwa kwake na mfumo wa kisiasa uliofuata vilikuwa sahihi kwa mazingira ya wakati huo?

Na Je kuanzishwa kwa TANU inaweza kua ni chanzo cha kufika hapa tulipo kwenye maswala ya siasa?

Tafadharini wana jukwaa hili chonde chonde lengo si kumdharau Nyerere wala kubeza mchango wake katika taifa sote tunajua nafasi yake na ndio maana leo tupo hapa kuzungumzia na kujadili pamoja

Lengo ni kujiuliza maswali kuchambua historia yetu kwa upana na kutofautisha kati ya heshima kwa viongozi wetu na uwezo wa kuhoji maamuzi yao

Historia haipaswi kuwa sehemu ya kusifia pekee inapaswa pia kuwa nafasi ya kujifunza kutafakari na kujenga taifa bora zaidi.

Karibu kupongeza
Karibu kukosoa
Karibu kujenga hoja
karibu kutoa maoni yako

Tujadili hapa ni kitu gani hasa ambacho Nyerere alifanya ungetamani kiendelezwe au Ni kitu gani ungependa kipitiwe upya

Karibuni Great Thinkers. 🫡🇹🇿

ShesRise_1 ✋️

Wapwa walivyo hawana aibu watasema na hii umeandikiwa 😂.

Big brain madam🫡
 
Kwa upande wangu huyu mndewa kama binadamu au viongozi wengine popote pale duniani ana mazuri yake na mabaya yake,kwahiyo hakuwa mtakatifu
Ni sawa
Na kizuri zaidi kabla hajafa alikiri kwamba kuna mambo mabaya aliyafanya kwenye uongozi wake,na alijoke kwamba badala ya watu kuiga mazuri yake na kuyafanyia kazi kinyume chake wanaiga hata mabaya yake
Kumbe hata yeye alikiri ila unasema watu wasijadili kwa kumkosoa?
Sasa kwa upande wangu kuna mazuri kadhaa ambayo huyu mndewa ameyafanya na anahitaji pongezi kwa hilo

Mosi,azimia la Arusha,pamoja na mambo mengine hapa ndio maadili ya viongozi yalipewa uzito mkubwa sana,ikiwemo kiongozi asijihusishe na mambo mengine nje ya siasa,ikiwemo kumiliki mali au kuwa mfanya biashara

Hapa kiongozi hakuwa na tamaa ya kujilimbikizia mali,uongozi ulikuwa kwa ajili ya kuwahudumia watu,wote tunajua baada ya kuanzishwa azimia la Zanzibar basi rushwa sasa na kujilimbikizia mali na ufisadi umekuwa sehemu ya maisha yetu ya kila siku

Viongozi wamejawa na tamaa ya kuhodhi mali na kujinufaisha wao binafsi

Lingine ambalo ni zuri ni kujenga umoja wa kitaifa,leo hii tupo proud hapa Tanzania kwamba wote ni wamoja,hakuna kuangaliana huyu ni kabila gani au anatoka wapi, tunatambuana kwa utanzani wetu kupitiia lugha yetu adhimu kabisa Kiswahili,kwahiyo katika eneo hili napo kafanikiwa sana
Shukran sana alifanya kwa nafasi yake tunampongeza 👏
 
Nyerere ana mengi mazuri ila hakuwa mchumi mzuri na pia alijuhusisha na mambo mengi sana ambayo hayakuwa na faida kwa Tanganyika kama nchi. Alikuwa idealist sana pia.
Alikuwa mchumi mzuri sana ila alichofeli kukizingatia ni kwamba binadamu kiasili ni wabinafsi ukiwaambia walime mahindi kwenye shamba la kijiji tegemea kulala njaa
 
Ukiondoa madini ni kitu gani hapo mtanzania anaweza kukitumia kununua gari au bunduki ujerumani? Mito? Maziwa? Bandari?

Bandari ni kama stendi ya meli mkuu zikiingia landcruiser kutoka ujerumani zilizo agizwa na mchimba madini wa chunya tunazikatia kodi hapo. Na dhahabu ya huyu bwana wa chunya inaenda ujerumani (utajiri una flow from Chunya to ujerumani).

UChumi hauhitaji hasira mkuu.

Nionyeshe bidhaa zinazotoka Tanzania kwenda ujerumani (made in Tanzania) nikuonyeshe marcesdez benz kitoka ujerumani hapa chunya

Ukiisha elewa ndio utajua kwanini ulipewa uhuru bila kumwaga damu

Na ukae ukijua CHADEMA wakishika nchi kodi zipo pale pale, polisi wapo pale pale na jeshi ni lile lile na pesa za kujenga bara bara utatoa wewe na sio wao kwa sababu wao wanakutegemea wewe utoe kodi ndio wajenge

Suluhisho ni viwanda, viwanda, viwanda, viwanda
Nani kasema kua suluhisho la nchii ni Chadema ?
Kila siku tunasema hii nchi hata wakipewa chadema bila kuboresha kabitiba ni sawa na kazi bure

Hii nchi tatizo sio CCM
Tatizo ni misingi na muundo wenyewe ndio maana leo tunajadili kuhusu wa asisi wa taifa Nyerere akiwa kiongozi wao hao wazee laiti kama wangesimika misingi imara tusingekua hapa

Pengine tungekua na matatizo ila nadhani sio kwa ukubwa huu
 
Tunabuguana kwa vyama zaidi
Sijui kama ni sahihi kusema ushindani wa kisiasa ni kubaguana,hapana sio sahihi,vyama vyote duniani msingi au kazi yao namba moja kutaka kushika dola,kwahiyo lazima watakuwa na maono na Sera mbali mbali katika kufikia malengo yao

Kwahiyo kutofautiana kupo kwa Sera zao na maono yao,na hamuwezi kuwa na vyama vya siasa ambavyo vyote vitakuwa na mtazamo mmoja au malengo yanayoo fanana,kwahiyo kutofautiana kisiasa kupo lakini si sahihi kusema huku ni kubaguana
 
Kuuana, kupotezana na kufungana kwa sababu ya siasa sio ushindani, ni ubaguzi wa kisiasa.
 
Lawama haziwezi kukosekana hata kidogo ,lakini sio katika mambo ambayo yeye moja kwa moja hahusiki,mlaumuni kwa yale ambayo yeye binafsi amehusika nayo lakini kwa yale ambayo hakushiriki moja kwa moja basi asishirikishwe
Ni lawama gani ambazo hahusiki nazo ambazo amebebeshwa hapa?
Zitaje
 
Kumbe hata yeye alikiri ila unasema watu wasijadili kwa kumkosoa?
Sijasema asikosolowe ila je anakosolewa kwa jambo amehusika moja kwa moja au kwa makosa ya wengine?

Hivi leo hii umkosoe Nyerere kwa yanayotokea CCM leo ni sahihi kweli?
 
Alikuwa mchumi mzuri sana ila alichofeli kukizingatia ni kwamba binadamu kiasili ni wabinafsi ukiwaambia walime mahindi kwenye shamba la kijiji tegemea kulala njaa
Nyerere kwenye mambo ya kiuchumi hakua vizuri, hapo umezungumzia kilimo tu lakini angalia sekta zingine kama madini, usafiri, viwanda & utalii hakuzitendea haki.
 
Wapwa walivyo hawana aibu watasema na hii umeandikiwa 😂.

Big brain madam🫡
Nitaandikiwa thread ngapi mkuu na kusaidiwa kujibu comment 😅😅

Kwanini watu wahawaamini kama mwanamke anaweza kujenga hoja?

Basi wapitie hata mabandiko yangu mengine wataona tu ni mimi mwenyewe wala sihitaji script kutoka kwa mtu au akili mnemba

Waje Tujadili kwa hoja hivyo tu
 
Baba wa Taifa ana mazuri na mapungufu yake.

Kamwe hakuwapenda watu waliomzufi uwezo kama akina Tuntemeke sana na Oscar Kambona, vivyo hivyo, viongozi wa Leo wa Taifa letu hawapendelei kuona watu waliowazidi uwezo wakiishi kwa uhuru. Kwa ufupi yeye ndiye aliyepanda hii mbegu...
 
Back
Top Bottom