Happy Nyerere day Tanzania 🇹🇿
Leo ikiwa ni kumbukumbu ya kifo cha muasisi wa taifa hili, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyezaliwa tarehe 13 Aprili 1922 na kufariki tarehe 14 Oktoba 1999, ni vyema tukajikumbusha historia yake na mchango wake katika taifa hili.
Nyerere wakati anafariki wengine ndiyo tunazaliwa au ni wadogo lakini historia yake inaishi na itaendelea kuishi kutoka kizazi hadi kizazi
Nyerere anakumbukwa kama mpigania uhuru aliyeshirikiana na wazalendo wengine wa taifa hili kupigania uhuru wa Tanganyika kutoka kwa wakoloni bila kumwaga damu
Mwaka 1954, alishiriki kuasisi chama cha TANU (Tanganyika African National Union), kilichokuwa mstari wa mbele katika harakati za kudai uhuru
Hatimaye, Tanganyika ilipata uhuru tarehe 9 Desemba 1961, na Nyerere akawa Waziri Mkuu wa kwanza
Mwaka 1962 akawa Rais wa kwanza wa Tanganyika, na mwaka 1964 akawa Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (Hapa kwenye muungano hapa🤔)
Tujikumbushe baadhi ya mambo aliyoyafanya enzi za uhai wake:
1. Kupigania uhuru: Aliongoza harakati za kisiasa zilizosaidia Tanganyika kupata uhuru mwaka 1961
2. Kuimarisha umoja wa kitaifa: Alihimiza umoja wa Watanzania bila kujali makabila yao na alikuza matumizi ya Kiswahili kama lugha ya taifa
Mf: Akikataza kuulizana maswali ya ukabila akilenga kuliunga taifa
3. Kuunganisha Tanganyika na Zanzibar: Alishiriki katika kuasisiwa kwa Muungano wa mwaka 1964.(Muungano🤔)
4. Ujamaa na Kujitegemea: Mwaka 1967, alitangaza Azimio la Arusha lililosisitiza usawa, kujitegemea na umiliki wa pamoja wa baadhi ya rasilimali za uzalishaji
5. Kupanua elimu na huduma za jamii: Serikali yake iliendeleza juhudi za kupanua upatikanaji wa elimu na huduma za afya kwa wananchi
6. Kusaidia ukombozi wa Afrika: Aliunga mkono harakati za ukombozi wa nchi nyingine za Afrika zilizokuwa bado chini ya ukoloni au tawala za kibaguzi.
7. Kuachia madaraka kwa hiari: Mwaka 1985, alistaafu urais na kumwachia madaraka Ali Hassan Mwinyi Mzee wa Rukusa
Lakini pamoja na yote hayo, kuna maswali ambayo tunapaswa kujiuliza kama taifa
Je, Nyerere alikuwa mtakatifu?
Je, kwa sababu alikuwa Baba wa Taifa, tunapaswa kuona kila alichofanya kuwa sahihi bila kukikosoa?
Unadhani Nyerere na wenzake walijenga misingi bora ya taifa hili, au kuna mapengo makubwa yaliyoachwa ambayo hadi leo yanaendelea kuliathiri taifa letu?
Tukiangalia misingi ya demokrasia, uchumi, elimu na haki za wananchi, je, tunaweza kusema kwamba kila uamuzi uliofanywa wakati wa uongozi wake ulikuwa sahihi?
Na kuhusu chama cha TANU alichoshiriki kukiasisi mwaka 1954, je, kuanzishwa kwake na mfumo wa kisiasa uliofuata vilikuwa sahihi kwa mazingira ya wakati huo?
Na Je kuanzishwa kwa TANU inaweza kua ni chanzo cha kufika hapa tulipo kwenye maswala ya siasa?
Tafadharini wana jukwaa hili chonde chonde lengo si kumdharau Nyerere wala kubeza mchango wake katika taifa sote tunajua nafasi yake na ndio maana leo tupo hapa kuzungumzia na kujadili pamoja
Lengo ni kujiuliza maswali kuchambua historia yetu kwa upana na kutofautisha kati ya heshima kwa viongozi wetu na uwezo wa kuhoji maamuzi yao
Historia haipaswi kuwa sehemu ya kusifia pekee inapaswa pia kuwa nafasi ya kujifunza kutafakari na kujenga taifa bora zaidi.
Karibu kupongeza
Karibu kukosoa
Karibu kujenga hoja
karibu kutoa maoni yako
Tujadili hapa ni kitu gani hasa ambacho Nyerere alifanya ungetamani kiendelezwe au Ni kitu gani ungependa kipitiwe upya
Karibuni Great Thinkers. 🫡🇹🇿
ShesRise_1 ✋️
Hongera mkuu kwa maada murua kabisa.
Kwa mawazo yangu na ingekua amri yangu bhasi ningetafuta baba wa Taifa mpya. Simvunjii heshima Nyerere lakini huo ndio ukweli na utabaki kuwa ukweli daima. Nasema hivyo kwasababu zifuatazo-
Mosi
- Nyerere alitengenezwa na hao wenye maslahi na hii nchi ili tupate uhuru wa bendera. Nyakati za ukoloni zilikua zimeshakwisha kwasababu watu walikua wanazidi kufunguka kiakili na kutafuta mbinu mbadala za kupambana na ukoloni, hivyo wakoloni walikuja na mbinu mbadala ambayo ndio ukoloni mamboleo.
Nyerere aliiuza Tanganyika kwa Malkia, rejea historia ya safari yake Uingereza. Pia katika mapinduzi 9 ambayo yalijaribu kumtoa Nyerere madarakani, mapinduzi yote hayo yalizimwa kwa usaidizi wa Uingereza.
Pia Uingereza ndio mmiliki wa kisiwa Cha Zanzibar, rejea historia ya vita fupi kabisa duniani ilikua ni kati ya Uingereza na Zanzibar. Je! ulishawahi kujiuliza kwanini Zanzibar alipigana na Uingereza? Je! baada ya hayo mapigano ni Nini kilitokea/kiliendelea?
Baada ya vita fupi kabisa duniani, Zanzibar ilibakia kuwa koloni la Uingereza pia.
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni kusudio la Uingereza kuunganisha makoloni yake ili uwepo wepesi wa kufanya ukoloni mamboleo. Hivyo Nyerere anapopewa credit ya muungano nafikiri tunashindwa kuelewa alifanya hivyo kwa maslahi ya nani???
Leo tunauona muungano wetu ulivyo wa hovyo, tena afadhali huyo mkoloni yeye muungano wake na Ireland, Scotland na Wales Kuna uhuru kidogo.
Nyerere ndiye aliruhusu Uingereza iwe inaandika/kuipitisha mitaala ya elimu yetu. Sio ajabu elimu yetu ni mboooovu na haizalishi wasomi wenye tija kwa Taifa letu.
2. Nyerere aliua mifumo yetu ya asili(Uchief) ya uongozi akaleta mfumo wa kitaifa. Nyerere aliingia mikataba ya kuua mifumo ya kichifu na kuleta mfumo wa serikali ili kujipa yeye madaraka makubwa. Madhara yake tumeyaona tulipopata Marais vichaa wanaua mpaka wananchi wao.
Mimi binafsi sikuona umuhimu wowote wa kuleta mfumo wa serikali kuu, Bali tungebaki na mifumo ya asili lakini yangekua yanatambulika kama majimbo.
Leo Kuna takataka zinaitwa wabunge zinakula Kodi zetu Kwa kigezo Cha uwakilishi wa wananchi na kuisimamia serikali. Kwakweli kazi ya hao wabunge hata sizioni naona ni watu waliopo kwaajili ya maslahi yao.
3. Nyerere alileta mfumo wa kijamaa na aliposhindwa kuusimamia alitumia kigezo Cha kung'atuka lakini huku nyuma aliacha mashimo makubwa sana yailyoharibu uchumi wa nchi yetu kabisa.
Hata hivyo kabla yakung'atuka ni vyema angetangaza kuufuta rasmi mfumo wa kijamaa. Lakini aliishia kumtwika mzigo mzito Mhe.Mwinyi huku akimshauri Mwinyi akakope world bank na IMF wakati yeye aliwapinga.
4. Nyerere alituachia katiba mbovu sana, Katiba yetu ilitungwa mwaka77 na CCM ilianzishwa mwaka 77 baada ya TANU kuungana na A.S.P, Katiba hii ilitungwa ili kukipa madaraka chama Cha CCM na ilitungwa na hao niliowasema hapo juu kwamba Nyerere alikua kibaraka wao.
Nyerere alijua anachokifanya na ndio maana aliishia kuongea tuu kwamba tunakatiba mbovu ila hajawahi kutaka mabadiliko yake.
5. Nyerere alifanya madudu mengi lakini pia alikua na mazuri yake.
Kwa heshima na tahadhima napenda kumpongeza Nyerere kwa kulielimisha hili Taifa. Nyerere aliipokea hii nchi ikiwa na wasomi wasiozidi 100. Baada ya kuchukua madaraka alianzisha elimu ya watu wazima MEMKWA.
Alijitahidi sana katika hili, alifanya bidiii sana mpaka watu wakajua kusoma, kuandika na kuhesabu. Yes! Yes! Yes! Elimu Yao waliita K,K,K,K Yaani Kujua Kusoma,Kuandika na Kuhesabu.
Babu yangu alijua kusoma na kuandika hivyo walimchagua pia awe mwalimu kwa jamii yake.
Mwisho niseme hii nchi itapata ukombozi siku ukweli utakapowekwa wazi.
Uingereza inatikiswa na CCM inatikisika😂😂😂, pale Uingereza kiti Cha waziri mkuu hakikaliki🤣🤣🤣, Brexit imesimama, Ireland, Scotland na Wales wanasubiri kula za maoni.
Ukisoma historia ya Nigeria na yule jamaa yao wa kuitwa BABANGIDA ndio yaliyopo Tz na CCM.
Nb: Maelezo ya ziada ni ndio njia tunaweza kupita ili kumpata baba wa Taifa mpya nje ya hapo tuendelee kuimba Iyena Iyena.
Ni mimi Zirlovimovic Vladimilovic Zirkov a man from the past and the future.