ShesRise_1
JF-Expert Member
- Aug 21, 2025
- 22,235
- 51,111
- Thread starter
- #61
Aisee nomaaNyerere alikua muhuni tu kama wahuni wengine alipenda CCM kuzidi nchi
Aisee nomaaNyerere alikua muhuni tu kama wahuni wengine alipenda CCM kuzidi nchi
Hatimae umeunga mkono hojaHapa nakubaliana na wewe mkuu,hata yeye mwenyewe alishawahi kulizungumzia hili na kusema hii katika siku akija kushika madaraka mtu ambaye ni dikteta basi itakuwa ni balaa sana
Kwahiyo moja ya jambo kubwa ambalo huyu mzee anafaa kulaumiwa ni kutunga au kuilinda katiba ambayo ndio msingi wa mambo mengi ya hovyo yanayotokea sasa hivi
ShesRise_1 hapa Sasa lawama zote ziende kwa Nyerere popote pale alipo awe mzima au amekufa
TuwaacheHawana adabu 😃
Ni huzuni sanaNI yeye haswaa Mzee wa kilalacha
SawaKitu kingine ambacho utawala wake ulifanikiwa ni kuwa na Sera ya Non alignment
Kipindi kile cha vita baridi /cold War kati ya wabwana wakubwa wale
Sisi kama nchi hatukuwa na Sera za kuwa na upande wowote ule hatukuwa upande wa ukomunist au ubepari
Sasa hii ilitusaidia sana kuendelea na mambo yetu kama nchi bila kuathiriwa na ushabiki wa kuwa upande huu au ule,lau tungekuwa na ushabiki basi ingetuapasa kama ni Upande wa Russia basi ni huo huo na kama ni ubebapari basi ni huo huo,hii ingetufunga na kushindwa kuwa uhuru na kufanya mambo mengine kama nchi
Ndio kusema alituachia kizazaa😢Alikubali kuua demokrasia na kuacha katiba mbovu kupindukia.
Sana tu!😅😅 kwahiyo tumwagilie maji
Ndio kusema alituachia kizazaa😢
Hoja nimeelewa vizur sana hapa,labda huenda nyie ndio hamtaki kukubali kwamba sio kila kosa ni la NyerereWewe sijui hujaelewa hoja
Yanayotokea leo ndio kwa namna moja au nyingine anapokea lawama
Kwa sababu wao ndio walikosea mfumo bora tangu mwanzo
Mf: katiba na muungano
Kosa lake kubwa ni kutokuacha Tanganyika ipatikane mwaka 1994 au kuto kuiunganisha Zanzibar kuwa nchi moja mwaka 1984 alipomtoa Jumbe madarakani.Nyerere ana mengi mazuri ila hakuwa mchumi mzuri na pia alijuhusisha na mambo mengi sana ambayo hayakuwa na faida kwa Tanganyika kama nchi. Alikuwa idealist sana pia.
Nilijua ukija na hii unakua na akili nyingi 😅 kumbe wewe ni yule yule jana na leoSana tu!
Aiseee 😢Nyerere hakua fisadi tu ila kwenye demokrasia alivurunda 100% sasa kwa katiba hii waliomfuatia wamevuruga demokrasia na wamekua mafisadi wa kutupwa.
Hebu ona hapa.View attachment 3690463
Kwani Nyerere kalaumiwa kwa kila kitu mkuu?Hoja nimeelewa vizur sana hapa,labda huenda nyie ndio hamtaki kukubali kwamba sio kila kosa ni la Nyerere
Kuna mambo ya moja kwa moja unaweza kumlaumu Nyerere kama katiba au swala la Muungano,lakini sio kila jambo anapaswa kupewa lawama
Kuna mengine watangalizi wake wangepaswa kuyabadilisha,ndio maana hata yeye alisema Kuna mambo ya kijinga alifanya lakini kibaya zaidi bado watangulizi wake wanayaiga, je hapa wajinga ni yeye au watangulizi wake?
Hapa nawahitaji wafuatao... Kiranga (pundit) Mkandara @udadisi Susuviri Nyani Ngabu Jasusi if you know what I meanHappy Nyerere day Tanzania 🇹🇿
Leo ikiwa ni kumbukumbu ya kifo cha muasisi wa taifa hili, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyezaliwa tarehe 13 Aprili 1922 na kufariki tarehe 14 Oktoba 1999, ni vyema tukajikumbusha historia yake na mchango wake katika taifa hili.
Nyerere wakati anafariki wengine ndiyo tunazaliwa au ni wadogo lakini historia yake inaishi na itaendelea kuishi kutoka kizazi hadi kizazi
Nyerere anakumbukwa kama mpigania uhuru aliyeshirikiana na wazalendo wengine wa taifa hili kupigania uhuru wa Tanganyika kutoka kwa wakoloni bila kumwaga damu
Mwaka 1954, alishiriki kuasisi chama cha TANU (Tanganyika African National Union), kilichokuwa mstari wa mbele katika harakati za kudai uhuru
Hatimaye, Tanganyika ilipata uhuru tarehe 9 Desemba 1961, na Nyerere akawa Waziri Mkuu wa kwanza
Mwaka 1962 akawa Rais wa kwanza wa Tanganyika, na mwaka 1964 akawa Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (Hapa kwenye muungano hapa🤔)
Tujikumbushe baadhi ya mambo aliyoyafanya enzi za uhai wake:
1. Kupigania uhuru: Aliongoza harakati za kisiasa zilizosaidia Tanganyika kupata uhuru mwaka 1961
2. Kuimarisha umoja wa kitaifa: Alihimiza umoja wa Watanzania bila kujali makabila yao na alikuza matumizi ya Kiswahili kama lugha ya taifa
Mf: Akikataza kuulizana maswali ya ukabila akilenga kuliunga taifa
3. Kuunganisha Tanganyika na Zanzibar: Alishiriki katika kuasisiwa kwa Muungano wa mwaka 1964.(Muungano🤔)
4. Ujamaa na Kujitegemea: Mwaka 1967, alitangaza Azimio la Arusha lililosisitiza usawa, kujitegemea na umiliki wa pamoja wa baadhi ya rasilimali za uzalishaji
5. Kupanua elimu na huduma za jamii: Serikali yake iliendeleza juhudi za kupanua upatikanaji wa elimu na huduma za afya kwa wananchi
6. Kusaidia ukombozi wa Afrika: Aliunga mkono harakati za ukombozi wa nchi nyingine za Afrika zilizokuwa bado chini ya ukoloni au tawala za kibaguzi.
7. Kuachia madaraka kwa hiari: Mwaka 1985, alistaafu urais na kumwachia madaraka Ali Hassan Mwinyi Mzee wa Rukusa
Lakini pamoja na yote hayo, kuna maswali ambayo tunapaswa kujiuliza kama taifa
Je, Nyerere alikuwa mtakatifu?
Je, kwa sababu alikuwa Baba wa Taifa, tunapaswa kuona kila alichofanya kuwa sahihi bila kukikosoa?
Unadhani Nyerere na wenzake walijenga misingi bora ya taifa hili, au kuna mapengo makubwa yaliyoachwa ambayo hadi leo yanaendelea kuliathiri taifa letu?
Tukiangalia misingi ya demokrasia, uchumi, elimu na haki za wananchi, je, tunaweza kusema kwamba kila uamuzi uliofanywa wakati wa uongozi wake ulikuwa sahihi?
Na kuhusu chama cha TANU alichoshiriki kukiasisi mwaka 1954, je, kuanzishwa kwake na mfumo wa kisiasa uliofuata vilikuwa sahihi kwa mazingira ya wakati huo?
Na Je kuanzishwa kwa TANU inaweza kua ni chanzo cha kufika hapa tulipo kwenye maswala ya siasa?
Tafadharini wana jukwaa hili chonde chonde lengo si kumdharau Nyerere wala kubeza mchango wake katika taifa sote tunajua nafasi yake na ndio maana leo tupo hapa kuzungumzia na kujadili pamoja
Lengo ni kujiuliza maswali kuchambua historia yetu kwa upana na kutofautisha kati ya heshima kwa viongozi wetu na uwezo wa kuhoji maamuzi yao
Historia haipaswi kuwa sehemu ya kusifia pekee inapaswa pia kuwa nafasi ya kujifunza kutafakari na kujenga taifa bora zaidi.
Karibu kupongeza
Karibu kukosoa
Karibu kujenga hoja
karibu kutoa maoni yako
Tujadili hapa ni kitu gani hasa ambacho Nyerere alifanya ungetamani kiendelezwe au Ni kitu gani ungependa kipitiwe upya
Karibuni Great Thinkers. 🫡🇹🇿
ShesRise_1 ✋️
Hakika hakika alifanya kazi nzuri sanaMiongoni mwa vitu alivyofanikiwa Nyerere ni kuweza na kuikuza na kuiendeleza lugha ya kiswahili na kuifanya iwe lugha mama na inayozungumzwa na kueleweka na watu wengi na makabila mbalimbali, kujenga taifa lisilokuwa na udini na ukabila kwa kiasi kikubwa
Chama dola hapa alikosea timing aisee alituingiza chakaMapungufu yake ni kuingia haraka na bila kutafakari kwa kina kwenye siasa za ujamaa, muungano wa 1964, kutengeneza katiba ya mwaka 1977 ambayo imeifanya ccm kuwa chama dola kuliko chama Cha kisiasa..
Nyerere ni Baba wa TaifaYote kwa yote anabaki kuwa muasisi wa taifa letu regardless ya disaster aliyotengeneza either kwa kujua au kutokujua
Shukran sana mkuu 🙏🙏Mimi hua si comment humu mara kwa mara ila leo wacha ni comment. Asee huyu ShesRise_1 ni mtu mmoja mwenye akili sana. Hua napitia maada zake kmya kmya na most of mada zake ni za kujenga. Nakupongeza sana ShesRise_1 kwa kua ww ni moja kati ya Great thinker wa Jamii Forums.
Muda ukifika nitapewaModerator napendekeza huyu member apewe uplatnum member