Kwa mujibu wa maelezo mwalimu alitaka wanafunzi waje kusaini ofisini kwake kila siku saa moja na nusu, hii inaonesha kuwa hawa wanafunzi ni sugu kwenye utoro na uchelewaji,,,
hii ni kawaida kabisa kwa shule zenye kujielewa na zenye kufuatilia watoto kwa ukaribu.
Lengo la kufanya hili zoezi la baadhi ya wanafunzi kuja kusaini kwa mwalim ni kumfanya mtoto wako awe anatabia ya kuwahi shule na asiwe mtoro bila sababu, kwasababu kadiri wanavyo chelewa wanakosa masomo hasa vipindi vya asubuhi, na huenda ni vipindi vya asubuhi huwa ni basic mathematics au physics, wanavyo chelewa wanashusha ufaulu wa shule,
HUENDA shule hii ni private na tabia hizi za wanafunzi kama hawa wanashusha taaluma ya shule na wanavuruga image ya shule husika.
INAWEZEKANA
mwalim amefanya uchunguzi na kujiridhirisha kuwa sababu za utoro na uchelewaji ni UZEMBE WA MWANAFUNZI TENA KWA MAKUSUDI, na ukisema uwaache tu tabia hii itaota mizizi. ukiwafukuza utalaumiwa na hao hao wazazi tena utatangazwa kila kona ya dunia kuwa mwanangu kafukuzwa shule kwa kosa la kuchelewa, ukimwacha kila siku anakuja shule muda wa vipindi na jamii hii hii itasema shule haina uangalizi, wanachapwa fimbo mbili tatu ila kila siku wanarudia makosa hayo hayo tena kwa makusudi, ukifuatilia zaidi sababu za kuchelewa shule unaweza kuta ni kufuatlia movie na tamthilia hadi usiku wa manane,
MWANAFUNZI AKICHELEWA AKICHAPWA WALIMU WANALAUMIWA
WAKIACHWA ,WALIMU WATALAUMIWA SHULE HAIFATILII WANAFUNZI, SHULE HAIJIELEWI, WATOTO WANADHURURA MUDA WA MASOMO,,,,
MWALIMU AFANYAJE??????
lawama zote kwa walimu, walimu, walimu, walimu walimu
Shule za serikali wameluona hili wameamua kuwaacha watoto wenu wafanye watakavyo, walimu wanachukua mshahara saa 9 wanasepa kufuga kuku na wengine wanaenda shamba, nafikiri ya watoto wenu walio shule za serikali hali mnaiona sasa na tabia za watoto wenu,,huo ni mfano tu, subirini jamii ya kesho mtaiona tu,,,, mmewadharau walimu subiri watoto wenu wa kesho mtaona ushoga na usagaji na mauaji yatakavyo ongezeka kupitia utandawazi huu na hizi filamu, ukweli nikuwa watoto wenu muda mwingi hawapo na wazazi bali wapo na walimu ambao wamekatishwa tamaa na jamii
Shule za private sasa wameanza kubadili mfumo, sasa shule zimeanza kuajiri hadi watu wakufanya usafi shuleni,,, tunatengeneza kizazi cha broilers cha hapo mbeleni,,,
WALIMU WANALIPWA MSHAHARA LAKI 3 HADI 5 ,,, hii ndo hali ya walimu nchi hii.
Wanaweza wakakosea kwa msongo wa mawazo ila ndo wanaolea watoto wenu, warekebishwe na sio kupost mitandaoni, mnaharibu taswira ya ualimu,shule na kuwapa Vichwa wanafunzi,