Mwambieni CAG, sisi tumeridhika kwa kuwa tumezoea kuibiwa

Unaacha kwenda kushangaa baharini "SHILINGI 100" inazama, wakati "MELI YENYE MAKONTENA NA MAGARI" inaelea juu ya maji.

Marehemu alikua "MKOLONI" na aliturudisha kwenye "UTAWALA WA KIKOLONI & UTUMWA (Colonial & Slavery Erra)".
Unaujua ukoloni au unaropoka tu?
 
Sasa najiuliza ikiwa ripoti ya CAG imeonesha madudu je, ni jinsi gani sasa kama taifa tumeingiaje uchumi wa Kati? Ikiwa tumeibiwa Sana namna hii...
kumbe watu wajinga na wapumbavu mpo.

itachukua muda sana kupata maendeleo. unahalalisha kosa kwa makosa mengine
 
Kwa nini nitaje moja na yako wengi?Makampuni ya mabeberu machache in Tanzania.

👇

Bila kusahau mabeberu wakubwa kuliko wote IMF, World Bank,Makampuni ya Madini na hata Gas.
Mbona hawa wote uliowataja kuwa ni mabeberu ndio wafadhili wakubwa wa serikali yako?
 
Mimi ni mtanzania na nina haki ya kutoa mawazo yangu. Nimeridhika na wizi wa Magufuli,kwa kuwa hata kama kaiba,ila nimeona alichofanya,tena kikubwa.Wengine walishibisha matumbo yao, familia zao na kugawa bure mali za Watanzania kwa mabeberu.
Haki ikizidi ni wenda wazimu! siyo kwa sababu waliiba na wewe uibe!! mwizi ni mwizi tu hkun mwizi mzuri wala mbaya, wote mnafaa kupigwa mawe/moto!! kikubwa kipi hiyo kujenga chato yenu kiubabe?? sasa watatua popo na mbayuwayu!!

Amefanya hao wengine hawakufanya?? hiyo miaka mitano aliyo kaa hapo alikuwa anatihimisha mipango ya walio mtangulia, yake ndo yalitakiwa kuanza kuonekana awamu yake ya pili, na ya nne kwa mwingine atakae kuja!! walikudanganya tu au hukusoma vizuri!
 
Mimi ni mtanzania na nina haki ya kutoa mawazo yangu. Nimeridhika na wizi wa Magufuli,kwa kuwa hata kama kaiba,ila nimeona alichofanya,tena kikubwa.Wengine walishibisha matumbo yao, familia zao na kugawa bure mali za Watanzania kwa mabeberu.
Kwahiyo yakiyofanyika uko nyuma kabla ya jpm uyajui kwasababu ulikua hujazaliwa au?.tumia akili vizuri kuelewa sio kukariri.
 
MWAMBIENI CAG, SISI TUMERIDHIKA

1. Mwambieni CAG kwamba sisi wenyewe tumeridhika, tumezoea kuibiwa. Mwambieni tofauti ya wizi wa zamani na huu ni kwamba wizi wa sasa unafaida kwa Wananchi wala asiumize kichwa. Mwambieni sisi Wananchi hatuna tatizo na hasara au wizi uliofanyika wakati wa JPM. Sisi tumeridhika hivyohivyo kwa sababu tuna macho ya kuona!!

2. Mwambieni CAG kwamba tuliibiwa hapa kupitia EPA. Pesa bilioni 135 zikaliwa na watu wachache, wakati huo elimu bure ilikua bado kuja. Mikopo ya elimu ya juu ilikua ni songombingo kwa hiyo hatuoni hatari kuibiwa sasa huku elimu bure ikiwa imeanzishwa na mikopo ikitoka kwa wakati. Sisi tumeridhika kabisa na hasara au wizi wakati wa JPM!!

3. Mwambieni CAG kwamba tuliibiwa hapa bilioni 300 Serikali ikilipa Makampuni hewa katika kashfa ya MEREMETA. Mwambieni hapakua na tatizo lolote na wakati huo bajeti ya Dawa ilikua chini ya bilioni 30 lakini sasa na wizi wa JPM umepandisha bajeti ya DAWA zaidi ya mara tisa; yaani bilioni 270. Mwambieni kwa wizi huu Mungu atupe nini? Tumeridhika sana na wizi wakati wa JPM.

4. Mwambieni CAG kwamba tulishaibiwa sisi kwenye mauzauza ya uwekezaji wa Bulyanhulu na Buzwagi na hata leo hakuna maelezo ya yanayoeleweka. Kodi hazikulipwa na pesa zikapigwa na wajanja wachache. Wakati huo wote madini na migodi YOTE ilikua ni Mali ya Wawekezaji wasiolipa kodi, Wananchi ilikua ni marufuku kukaribia migodi katika nchi yao. Kama JPM ameiba halafu wananchi wanachimba madini wenyewe kwa uhuru, ninaumia kwamba atakua ameiba kidogo sana. Wizi wenye manufaa kwa umma una maana zaidi kuliko wizi usio na manufaa. Sisi tumezoea kuibiwa, lakini kwa huu wa JPM tumeridhika.

5. Mwambieni CAG kwamba sisi tumezoea kuibiwa. Tumeshaibiwa haswa, ilikuja hapa tukaibiwa katika Mkataba wa kijinga wa DOWANS. Nchi ikalipa Bilioni 111 kwa sababu ya maslahi ya watu wachache. Wakati tunaibiwa kupitia DOWANS, Mv. Victoria ilikua inalaza watu siku mbili ziwani kwa ubovu wake. Maisha yao yalikua hatarini kila safari, leo wakati wa JPM wakiiba au akitutia hasara ya bilioni 60 huku Mv. Victoria ikiwa MPYA kuna tatizo gani? Meli mpya tele kuanzia ziwa Nyasa, Tanganyika na Bahari ya Hindi Kilwa. Tunapenda wizi wa namna hii, angeiba kabisa za kutosha akajenga nyumba nzuri kama wenzake, akamiliki magari ya mizigo meupe lukuki na sheli za kumwaga. Au akamiliki supermakert za Da'slam kama wenzake. Sisi kuibiwa tumezoea, wizi wakati wa JPM una manufaa, tumeridhika.

6. Mwambieni CAG kuwa sisi tumezoea kuibiwa asijiumize bure na ma-press ya kutangaza vi-wizi vya kitoto hivyo. Tulipigwa hapa pesa TAKATIFU katika Mkataba maarufu wa RICHMOND ulioondoka na Serikali ya mwaka 2008 hadi sasa hakuna kilichofanyika. Wakati tukipigwa pesa za Richmond daraja la Mfugale lilikua halipo, Daraja la Ubungo (Kijazi Interchange) haikuwahi kufikiriwa, Daraja la Tanzanite (Salender) lilikua katika ndoto, lile la Busisi halikufikiriwa kabisa. Kama tumeibiwa leo na mambo yote haya yamefanyika mwambieni CAG sisi roho kwatu, tumeridhika riport zake tupa kule hatusikii la mwazini wala mnadi swala. Tumefunga masikio!!

7. Mwambieni CAG sio hata siku nyingi zilichotwa BOT bilioni 306 kwa kilichoitwa kashfa ya TEGETA ESCROW. Nchi ikaibiwa tena na wajanja wachache, wakabeba pesa kwenye masandarusi na rumbesa. Wakati tukiibiana bilioni 306 za Escrow umeme vijijini ulikua unaunganishwa kwa Tsh. 454,000 ila kwa wizi wakati wa JPM umeme vijijini unaunganishwa kwa Tsh. 27,000; asilimia zaidi ya 70% umeme umefika vijijini. Wizi mzuri kiasi gani huu!? Sasa tunajenga megawati 2400 kutoka Bwawa la Nyerere ili umeme ushuke zaidi. Ingalikua uwezo ni wangu ningalimrudisha mtu huyu aendelee kuiba na kutia hasara zaidi kwa sababu wizi na hasara zake zina manufaa kwa watu. Mwambieni CAG sisi tumeridhika hivyohivyo, atuwache!!

8. Mwambieni CAG sisi tumewahi kuibiwa Twiga mzima akabebwa na shingo yake akaondoka zake. Hii nchi tunaibiana na Wanyama yeye anahangaika na vipesa vidogo vidogo vya matengenezo ya ATCL. Mwambieni wakati tukiibiana TWIGA upatikanaji wa maji Vijijini ulikua ni asilimia 47% na sasa kwa wizi na hasara wakati wa JPM upatikanaji wa Maji vijijini umefikia asilimia 70.1% huku mijini upatikanaji ukitoka asilimia 74% hadi 84%. Ni mtu mjinga pekee anaweza kuchukizwa na wizi wakati wa JPM, mwambieni CAG sisi tumeridhika tunatamani angekuwepo aibe tena. Hatutakagi ujinga!!

9. Mwambieni CAG kuwa tumeibiwa sana nchi hii. Wakati wote tuliibiwa huku Nchi ikiwa haina Ndege hai HATA MOJA. Mwambieni leo tuna Ndege 11 za kwetu wenyewe. Hizo hasara za ATCL zisimuumize kichwa, hakuna biashara isiyo na hasara, JPM keshawawekea mtaji na heshima ni wajibu wao kutafuta akili za kupata faida sio KUUA MTAJI. Mwambieni CAG, sisi tunampenda mwizi anayeiba halafu akanunua Ndege kwa ajili ya Nchi nzima, akajenga Reli ya kasi, Stendi kibao za kisasa, Masoko kwa ajili ya biashara nk. Kwakweli sisi tumeridhika sana na wizi huu!! Mungu amlaze mahala pema JPM, ametutoa tongotongo!!

10. Mwambieni CAG asipoteze nguvu zake bure kwa sababu hata hao wezi huwa hawafanywi kitu. Mwambieni tumezoea na zaidi tumeridhika na wizi au hasara wakati wa JPM. Mwambieni CAG nchi hii imeongozwa na wezi wengi lakini huyu alikua ni mwizi wa heshima. Tunampenda, tutammiss hivyohivyo na yeyote mwenye kumchafua atachafuka kwanza yeye. Tutakua Taifa la kijinga sana kuacha ALAMA za mtu huyu zifutwe na watu Wajinga, Wavivu wasio na lolote walioachiwa Nchi wasiongoze wakihangaika na umbea, udaku na ushambenga.

Kwa taarifa yenu #SISI TUMERIDHIKA HATA ANGEIBA NCHI YOTE AIUZE!! Tuna macho ya kuona.

TutakukumbukaDaima JPM

MenukaJr,
Da'slam-Tanzania.
 
Someni na Ripoti ya CAG 2014
Screenshot_2021-04-14-16-48-00-1.jpg
 
Mbona humshukuru aliyeandika ujumbe huu? Namba bado hazijasomeka. Mtaomba poo MATAGA. Sasa tuko MATHA= Make Tanzania Happy Again
 
Tunamshukuru JPM, hutaki hutak bwashe😂😠!
 
Nikumbushe namba 7,Mradi wa umeme vijijini yaani REA ulianza wakati wa JK,na Bei ilikuwa ni Tsh 27,000 sio zaidi ya hapo.
 
Imfikie CAG na waliomtuma
Alisema ukweli kabisa. Alileta na yale ambayo Assad aliyaandika yakamchoma dikteta akaamua kumuachisha kazi CAG mbobevu.

Mungu ni fundi MKUBWA mno tunamshukuru kwa ufundi wake mahiri
 
Kama watu wakifanya wizi mkubwa ndio flyover, Reli, mabwawa , madaraja, hospitali, ndege na mabarabara yanapatikana, naomba serikali iongeze kasi ya kuiba pesa, waibeee tena waibe zaidi...!!!
 
Wanaolalama ni wale waliokua wazoea kufaidi wenyewe

Huu utaratibu wameamua kuuita wizi sababu tuu hawajafaidi pesa ila wanasahau wote tunafaidi miundombinu na huduma za kijamii

Wanatengeneza mazingira ya kuingia wafanye yale ya zama zile ila haiwezekani
 
mama D Tunajua lengo lao walipiga billions of money na hawakufanya chochote cha maana JPM kashatuonyesha njia tutatembelea mule mule
 
Back
Top Bottom