Mwamposa: Mimi siyo Freemasons na sijui kwanini naandamwa na kusingiziwa vingi

Mambo ya watumishi wa Mungu iwe masheikh au makaasisi waachie wenyewe maana wanajua nani wanamtumikia
Wanapoingilia yale yasiyo kwenye uwezo wao, lazima tuwajulishe. Mimi siyo Mwislamu, lakini niseme ukweli, sijasikia au kuona Sheikh au Mhubiri wa Kiislamu akidai kuponya, kuleta au kuongeza utajiri, wala hawana vitabu vya utajirisho. Lakini dini ya Kikristo umeingiliwa na kujaa matapeli wengi mno. Kazi yao kudanganya watu kwa kutumia jina la Mungu kujitajirisha. Hii ndiyo sababu utaona ugomvi mwingi kwenye hayo makanisa. Wengine hutumiaa umaarufu wao wa kidini kujiingiza panono zaidi, kama vile kwenye siasa (Rwakatare/Gwajima). Wote hao siyo wacha Mungu bali matapeli. Ndiyo maana nyumba zao za igada hata kama zimejengwa na waumini lakini ni mali binafsi za hao manabii wa uongo.
 
Ila maaskofu wa katoliki kuvaa micheni mikubwa ya msalaba na Pete ya dhahabu ya Ki Askofu ni sawa tu? Shida ni Kwa Mwamposa tu?

Padre wa parokia tu wa kanisa katoliki gari ya thamani ya chini anayotumia ni Prado.
Kuna makanisa au madhehebu kazi zao za kiroho na kibinadamu zinaonekana. Makanisa katoliki yana huduma nyingi za jamii zinazojulikana. Unamlinganisha nabii wako ambaye pesa yote anayokusanya anakula na mke wake na watoto wake. Mali zote za madhahabu ni mali yake, pesa anaweka account ya binafi. Hao maaskofu Katoliki unaowasema wana mahospitali, kliniki, nchi nzima. Hivi unajuwa hospitali ya Bugando imejengwa na inaendeshwa na Kanisa katoliki. Na ile ile ya Moshi (KCMC) pia ni kanisa la Kianglikana au Kilutheri. Wewe kaa na matapeli wako wanaokudanganya wanawaponyama wasiyotembea kumbe uongo.
 
Yesu ambaye ndiye Neno la Mungu alishasema walio wake watatambua kazi zao wanaoijiita watimishi wake....
 
Mungu alikuponya na siyo padri. Padri hana uwezo huo. Alikuombea na Mungu akasikiliza sala zake na zako. Hata hivyo, pumu huwa inafikia mahali inapona yenyewe. Mimi watoto wangu wawili wamekuwa na pumu tena kali saana mpaka katika umri wa miaka 18 ikawa imeisha. Sasa hawa watoto wako kwenye 40s na hawajawi kupata attack ya pumu.
 
[emoji38][emoji38][emoji38]
 
😂😂😂 izi imani hizi
 
Kupona pumu tu kwan kina mwamposa hawajawai kuwaponya watu magonjwa mengine acheni wivu na husda ,,mwamposa chapa Kaz watu elfu 20 kwa ibada moja lazma utapigwa majungu

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Maswali ya msingi sana haya.

Sijawahi kufuatilia kumbe ndivyo inavyokuwa?
 
Watu wa Mungu naowaamini ukiacha dhehebu langu la RC ni mwakasege na mchungaji FJ Katunzi(huyu mchungaji ntamheshimu mpaka kesho kwa sababu aliniponya pumu mwaka 2004)
Mungu ndiye mponyaji siku zote zingatia hili..............huyo mchungaji alitumika tu na Mungu kupitisha uponyaji wako.
 
Mganga wa kienyeji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…