LGE2024 Mwamposa: Watu wangu nenda mjiandikishe mkapigie kura CCM

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Mkuu umemaliza kila kitu, siongezi chochote. Ukiona mtu anatumia nguvu za shetani kupata ushindi halafu anajitokeza kutaja jina la Mungu ujue huyo ni shetani mbaya hata kuliko Lucifer mwenyewe. Nape amewahi kusema kuwa wao wanapindua matokeo halafu wanamuomba Mungu awasamehe. Je, huyu ni Mungu wa kweli au ni Mungu wa namna gani? Huyu bila shaka sio Mungu bali ni shetani wanayejaribu kumpaka rangi ya Mungu.

Adhabu kwa mtu anayempamba shetani kwa jina la Mungu ni kali kuliko adhabu kwa mtu asiyemjua Mungu na ambaye ameamua kukaa upande wa shetani moja kwa moja bila unafiki. CCM na serikali yake siku zote wanahusika kuiba kura na kushinda uchaguzi kimagumashi lakini utawaona walivyo wanafiki wakishafika bungeni wanaapishana kwa kutumia Quran na Biblia. Watu wa aina hii ni wabaya hata kuliko shetani. Hukumu yao kwa Mungu itakuwa maradufu.
 
Huyo ni mfanyabiashara anatafuta kiki ili aendelee kubaki kawe na ccm wameishamhonga eneo kubwa la kujenga duka lake la kuuzia maji, mafuta na keki za upako huko mzee beach
 
Askofu shoo na kitime mbona wako wazi kabisa kubusu upande wanashabikia ?mbona hampigi kelele?
 
Fungua na wewe kanisa lako utakuwa na waumini kisha wahimize wakahaiikishe wanaipigia chadema ,hakuna haja ya kuona wivu kwa mwamposa
Kwa hiyo unakubali kuwa kanisa la Mwamposa ni tawi la CCM au unataka kusema nini mkuu? Je, Mwamposa anayo haki ya kusimama madhabahuni na kuhubiri siasa za CCM? Mwambie avue majoho avae magwanda ya CCM kama alivyofanya Askofu Gwajima ili tujue moja. Vinginevyo, kuwapigia kampeni CCM madhabahuni ni kumkufuru Mungu. Je, wewe una imani kwamba wafuasi wote wa Mwamposa ni makada wa CCM? Acha kutetea ujinga mkuu.
 
Askofu shoo na kitime mbona wako wazi kabisa kubusu upande wanashabikia ?mbona hampigi kelele?
Askofu Shoo na Kitima hawajawahi kusimama madhabahuni na kuwahimiza waumini wao wawapigie kura chama fulani. Kama hiyo clip unayo naomba uiweke hapa kila mtu aisikilize. Vinginevyo, ukae kimya na uache kutetea upumbavu mkuu.
 
Weka video kuthibitisha haya
 

Muhuni tu huyo. Anataka kuwafurahisha Wahuni wenzake.
 
Nchi huru hii acha Mwamposa afanye jambo jema kwake na kwa utajiri wake
 
Askofu Shoo na Kitima hawajawahi kusimama madhabahuni na kuwahimiza waumini wao wawapigie kura chama fulani. Kama hiyo clip unayo naomba uiweke hapa kila mtu aisikilize. Vinginevyo, ukae kimya na uache kutetea upumbavu mkuu.
Acha ujaha lugha wanazotumia kufikisha ujumbe ni kuipinga serikali na kuipinga serikali maana yake ni nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…