Mwana FA: Waziri Pekee kwenye Baraza la mawaziri asiye na Degree

Nlichogundua wasanii ni waongo sana nakumbuka zamani kwenye interview zake Ali kua anasema yeye ni form six olevel ana A ya kuswahili na Alevel ana A ya Kiswahili Ndo mana tungo zake ni konk kiasi hicho [emoji28][emoji28][emoji28]
 

Je ulikua ukitoka certificate unakwenda moja kwa moja Advance diploma na sio Ordinary diploma kwanza ?
 
Wachana na blablabla, kama kasoma IFM au IDM au IAA ni bora kuliko Havard. It is more than enough.

Sent from my SM-A127F using JamiiForums mobile app
 
Kawaida huwa hakuna diploma ya miaka mitatu; diploma huwa ni miaka miwili tu. Hicho kilichoandikwa hapo juu kama diploma si diploma plane bali ni Advanced Diploma; na hiyo ndiyo ilipelekea asome Masters degree kwa sababu kawaida Advanced Diploma huwa ni equivaent na First Degree.

Ni msomi mzuri nimempenda na ninampongeza sana kwa kuweza ku-diversify kwa namna hii kwenye qualificatons zake. Hakika mamlaka za uteuzi zilimuona kwa jicho lililo sahihi kabisa
 
Sjui atakua anasomaje ripori na kuzielewa
 
Hivi kiwango cha elimu ili mtu awe waziri ni kipi?
Waziri ni mtumishi kama walivyo watumishi wengine wa serikali ikiwa tu mtendaji wa mtaa ni lazima awe na angalao kuanzia diploma je waziri inatakiwa awe na elimu ya kiwango gani? maana waziri ni mshauri wa Rais moja kwa moja
 
Huyu pamoja na Ay na wasanii kadhaa nadhani ikiwemo ali kiba sijui walisoma chuo fulani cha IT kikijulikana kama Learn IT kiko pale lumumba kabla ya crdb ghorofani 3nzi hizo kikitoa ICDL za mambo ya IT kutoka UK nadhani walsoma kitu inatwa Internationl Diploma na kuna baadhi ya watu waliowahi waliisajili TCU ikawa inasound kama degree.

Kilikuwa na branch Oysterbay hotel area pia watoto wengi wa kipemba na kiarabu wamesoma chuo hichi.

Hichi chuo walisoma wasanii wengi sana wenhine hawakumaliza. Wakati ithibati bado inayumba ya kuthaminisha mitaala.
 
Madini kama haya ndio tunayataka Mkuu. Nimekuelewa kwa kiasi fulani
 
MwanaFA=Mediocre
 
Sifa ya waziri inatokana na sifa ya ubunge, kujua kusoma na kuandika! Na huko wanafanya kazi za kusoma na kuandika tu
 
Waziri ni mtumishi kama walivyo watumishi wengine wa serikali ikiwa tu mtendaji wa mtaa ni lazima awe na angalao kuanzia diploma je waziri inatakiwa awe na elimu ya kiwango gani? maana waziri ni mshauri wa Rais moja kwa moja
Huwezi kua Waziri bila ya kua Mbunge! Hayo mengine yote mbwembwe tu!!

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…