MwanaFA azomewa na wananchi baada ya kuanza kusifia Awamu ya 6 kwenye Tamasha la miaka 30 ya Bongo Fleva

Hatari wanaiona sana ndio maana wanatapatapa kutafuta namna za kujinusuru na hiyo hatari

Bahati mbaya ukiwa mwovu unachokiogopa ndicho kitakachokukuta!
 
Hivi mwana FA huwa hasomi upepo wa kisiasa unavyovuma nchini? kuna mambo si ya kutamka na kusema kukiwa na mvumo mbaya wa kisiasa mpaka upepo huo upite. Angalia ni wapi pa kusifia, uko na makundi gani kuweza kutoa sifa
Alitakiwa akatae uteuzi. Kitendo cha kukubali kuteuliwa kajitia kitanzi. Amekuwa si mtu huru tena kifikra na kimaamuzi.
 
CCM ni sikio la kufa hawasikii, hawashauriki, hawaelewi wala hawasomi alama za nyakati. Waache siasa kwenye mambo yanayowaunganisha na kuwaleta pamoja wanatanzania hata ni kwa nusu saa tu.
 
Wawe wanaandaa matamasha yao ya kusifu siasa zao, wanabuni tu tamasha kama la bodaboda, tamasha ngoma za kienyeji, tamasha la muziki wa dansi, mama lishe, wamachinga, tamasha la wavuvi, tamasha la singeli, taarabu nk. Haya watakuwa wameyaandaa wao, huko watamwaga sifa zote, hakutakuwa na vagi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…