Mwanafunzi wa IFM adhalilishwa na Walinzi wa Ikulu kisa kupiga picha maeneo ya ikulu

Hapo pameandikwa USIPIGE PICHA, na ikulu sio Kariakoo,najua kuna watu watakuja na mipovu oh mbona White House kwa Trump watu wanapiga picha wakiwa mbali nje,sheria za Marekani na Tanzania zipo tofauti,tuache kutoa mipovu kwa sababu zisizo na maana,na swali la mwisho umejuaje kama huyo ni mwananfunzi wa IFM na anatoka mkoani ama wanafunzi wa IFM siku hizi wanavaa uniform na beji kuwaonyesha kuwa wanasoma hapo na wanatoka mikoani?
 
Wanajeshi wetu nao hawana tofauti na mbwa ,reasoning zero.

Unavuta nywele za mdada ili iweje ? roho za Kichadema hizi
Sasa atareasoning kitu gani mtu wa std seven na form 4 failure..katupwa hapo getini waliosoma wanakula kiyoyozi ndani huko.
 
Huu Ushamba wa kutoruhusu kupiga picha sehemu kadhaa sijui utakwisha lini! Hivi hawa wajeda wsnajua kweli maana Google? Kwamba mtu yuko marekani anaweza hata kuona Maliwatoni kwa Mkulu!!
 
Pole yake!

Kuna jamaa mmja namjua yalimkuta naye,alafu huyo jamaa team lumumba kindakindaki
Jamaa walimuenyesha sana....kimoyomoyo nkasema Sawa sawa acha yamkute

Ova
Umemfuatilia baada ya kudhalilishwa vile bado ni kindakindaki kijani?
 
Mtera tu huruhusiwi kupiga picha kwa sababu za kiusalama sembuse ikulu?.
.
Kuna mazingira ikulu hayapigwi picha hata kidogo kama ilivyo white house ya trump hakuna view ya juu (Ariel view) mtaenda mtapiga mbele tu tena nje ya fesi. Huruhusiwi kupiga picha sehemu nyingine zaidi ya mlango wa kuingilia.
 
Maskini pole yake madada wa mkoani nao
Alikuwa anataka kuwapostia wanaume wa Dar.

Ccm hainaga undugu wanakupiga na kura unawapigia.

Angalia ishu ya korosho watu wamepigwa biti wakapitisha sheria,kaatumbua mawaziri wa kilimo alafu wakaja ikulu kushukuru kwa kutumbuliwa,USICHEZE NA HOFU KUU
 
Huyo binti ni mjinga kabisa amestahili alicho kipata na majitakia....
 

Endelea Kuwadanganya ' Mapopoma ' wenzio na najua Wapo wengi watakuwa wamekuamini wakati hii Taarifa ' umeitunga ' tu na hapa dhumuni lako Kuu siyo huyo Dada bali ni kusema kuwa IKULU ya Tanzania hiyo ya Dar es Salaam inalindwa na Wanyarwanda ( hasa wa Kabila la Watutsi )
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…