Mwanafunzi wa IFM adhalilishwa na Walinzi wa Ikulu kisa kupiga picha maeneo ya ikulu

Eheee nikiwa bado mgeni wa jiji nikapita yale maeneo naelekea agakani hospital mara paap Boda Boda nami nikaita kwa sauti oya bodaaaa simamaa!!! Mh sitaki kumaliza kilichotokea ngoja sitasahau
 
Unafikiri kwanini Wanatuita manyani ya dark continent....!??
Africa tuna shida nyingi..viongozi wetu ni Miungu watu, Mfano USA raia wake wanapewa fursa ya kutembelea ikulu yao (white house) hata raia wa kigeni..kuna bustani maalam ambapo raia wanaruhusiwa kutembelea ikulu, ila kwetu Tanzania,ukishamchagua rais wako,ni taboo (mwiko) kupita hata karibu na ukuta wa ikulu
 
Hats hao waliokupa like hapa nawashangaa pia!
 
Hakuna sheria ya inayomruhusi Askari kumpiga raia ikiwa hajanisha lolote.

Hiyo yote ni sifa tu za hao maaskari ili kumfurahisha Mkuu na kujipendekeza hakuna kingine.
 
Busara kwa wana usalama wetu ni sifuri. Hizo picha zingefutwa akaonywa kwa maneno. Watu tumewachagua wenyewe sasa wanatuona kama ng'ombe!
 
Nchi hii ujinga kila mahali


Ni kutokana na kukosa akili za kufikiria mambo ya maana yenye tija, sehemu nyingine raia wanauhuru wa kupiga picha mahali popote na endapo hairuhusiwi basi kunawekwa vibao maalumu kuzuia upigaji picha, ila hapa kwetu wanayafanya hayo ili kuonyesha wanafanya kazi kumbe ni ujinga mtupu
 
👉
Mwanafunzi wa IFM adhalilishwa na Walinzi wa Ikulu kisa kupiga picha maeneo ya ikulu

Usiahangae kwa akili zao wakaanza kukutafuta mleta mada hapa
 
Upuuzi tu.
Apo haparusiwi kupiga picha hata eneo la maji kuanzia soko la samaki na ukipita hakuna kusimama
Eneo lile limeongezewa ulinzi tofauti na tulivyozoea tatizo sisi wabongo wagumu kupokea na kuelewa vitu vipya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…