Mwanafunzi wa UDSM akamatwa kwa kusambaza taarifa na Takwimu za uongo za Covid-19 WhatsApp

Mwanafunzi wa UDSM akamatwa kwa kusambaza taarifa na Takwimu za uongo za Covid-19 WhatsApp

Wagonjwa wanapaswa watajwe na daktari nasio mtu Baki, serikalini Kuna mganga mkuu wa serikali huyo ndio atuambie, hao akina makonda Ni uvumi tu na sio taarifa za kitabibu
Kwa hiyo unataka kusema waziri wa afya anakosea kutoa taarifa za wagonjwa wa corona?

Huyo mganga mkuu wa serikali boss wake ni nani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hiyo unataka kusema waziri wa afya anakosea kutoa taarifa za wagonjwa wa corona?

Huyo mganga mkuu wa serikali boss wake ni nani?

Sent using Jamii Forums mobile app
Taarifa za mgonjwa hutolewa na daktari, ukienda aghakhan hospital majibu utapewa na daktari na sio imam wamsikiti wa ismailia, Ni vyema tuheshimu taaluma za watu, ndio maana taarifa za majambazi anatoa igp na sio simbachawene
 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga linamshikilia Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Mwaka wa Tatu Kitivo cha Kiswahili Mariam Jumanne Sanane (23) kwa kosa la Kuchapisha na kusambaza taarifa na takwimu za uongo kuhusu Corona kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo Whatsapp.

Akitoa taarifa kwa Vyombo vya Habari leo Jumamosi Aprili 11,2020,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba mtuhumiwa alikamatwa Aprili 9,2020 majira ya saa mbili na dakika saba(2:07) usiku eneo la Mwadui, mtaa wa Tabora, kwenye machimbo ya almasi wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga kwa kosa la kuchapisha na kusambaza taarifa za uongo kwenye mitandao ya kijamii.

“Tarehe 26/03/2020 Askari wa kikosi kazi cha mtandao kilifanikiwa kuona ujumbe kwenye whatsapp uliotumwa na mtuhumiwa unaosema ‘mpk ss Tanzania ina wagonjwa wapatao takribani 230 wa Covid 19 na waliofariki ni 04”,ameeleza Kamanda Magiligimba.

Amesema mtuhumiwa amepekuliwa na kukutwa na simu iliyotumika kutuma ujumbe huo na ameshahojiwa na atafikishwa mahakamani kwa makosa ya kuchapisha na kusambaza taarifa za uongo mtandaoni pamoja na kutoa takwimu za uongo.

Kamanda Magiligimba ametoa wito kwa wananchi kuwa makini na matumizi ya mitandao ya kijamii na kuacha kupotosha watu kwani kufanya hivyo ni kosa la jinai na hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Kwa hilo Jina lake tu la Ubini ( Ukoo ) la Sanane Kazi anayo na Mziki atauona pia.
 
Binti kawataja hao wagonjwa kwa mamlaka ya nani?kwa huyo binti ni msemaji wa wizara?

Sent using Jamii Forums mobile app
Wapi binti kaitisha press conference? Kaka Kangi alisema magroup ya WhatsApp Ni vijiwe sawa na jf Ni kijiwe tu na utani mzaha unaotolewa haina athari, hivi grupu la watoto washule Lina madhara gani kiusalama?
 
Ndiyo; kwa mtazamo wangu. Kwa nini unadhania takwimu za mtu binafsi ndizo za kweli ambapo waziri anayepewa takwimu kutoka pembe zote za nchi takwimu zake ziwe si sahihi? Simple logic.
Furthermore, hakusema kuwa taarifa za mtu binafsi ndizo za kweli... wala hakusema kuwa takwimu za waziri si sahihi

Ameuliza tu kosa lipo wapi? Maana hajaona kama zimeleta madhara takwimu za mtu huyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maswali ya kitoto hayo. Taarifa sahihi ni zile zinazotolewa na waziri mhusika. Askari wamejua kuwa taarifa za mtuhumiwa sio sahihi kwa kuwa ni tofauti na taarifa ya Waziri ambaye anaarifiwa kutoka pembe zote za nchi na baada ya kujumlisha takwimu hizo ndipo anatangaza.

Huyu mtu binafsi amepata wapi takwimu zake? Swali la mwisho kwamba taarifa ya mtuhumiwa imeleta madhara gani ni la kipuuzi mno na halihitaji hata kujibiwa.
Umejibu vizuri sana mkuu 100%[emoji1241]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Furthermore, hakusema kuwa taarifa za mtu binafsi ndizo za kweli... wala hakusema kuwa takwimu za waziri si sahihi

Ameuliza tu kosa lipo wapi? Maana hajaona kama zimeleta madhara takwimu za mtu huyo

Sent using Jamii Forums mobile app
Hizo taarifa zake zikienea zinaleta taaruki kubwa kwa Jamii Hilo ndio kosa.
 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga linamshikilia Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Mwaka wa Tatu Kitivo cha Kiswahili Mariam Jumanne Sanane (23) kwa kosa la Kuchapisha na kusambaza taarifa na takwimu za uongo kuhusu Corona kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo Whatsapp.

Akitoa taarifa kwa Vyombo vya Habari leo Jumamosi Aprili 11,2020,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba mtuhumiwa alikamatwa Aprili 9,2020 majira ya saa mbili na dakika saba(2:07) usiku eneo la Mwadui, mtaa wa Tabora, kwenye machimbo ya almasi wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga kwa kosa la kuchapisha na kusambaza taarifa za uongo kwenye mitandao ya kijamii.

“Tarehe 26/03/2020 Askari wa kikosi kazi cha mtandao kilifanikiwa kuona ujumbe kwenye whatsapp uliotumwa na mtuhumiwa unaosema ‘mpk ss Tanzania ina wagonjwa wapatao takribani 230 wa Covid 19 na waliofariki ni 04”,ameeleza Kamanda Magiligimba.

Amesema mtuhumiwa amepekuliwa na kukutwa na simu iliyotumika kutuma ujumbe huo na ameshahojiwa na atafikishwa mahakamani kwa makosa ya kuchapisha na kusambaza taarifa za uongo mtandaoni pamoja na kutoa takwimu za uongo.

Kamanda Magiligimba ametoa wito kwa wananchi kuwa makini na matumizi ya mitandao ya kijamii na kuacha kupotosha watu kwani kufanya hivyo ni kosa la jinai na hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
How if it was a typing error 032 but typing 320..sijui ila yote tujali kanuni za afya.
Nawa mikono na dawa,oga kwa sabuni ya dawa, kula matunda na mboga za majani,sali sana epuka msongamano..acha mazoea ya kusalimiana au kushika ovyo kingo za kushukia ngazi.. Ukijisikia vibaya fika kituo cha afya kwa uchunguzi wa hiari..

Maandalizi mema ya Easter..
Jesus Christo our savior..
 
Your right, chamsingi tujikinge, idadi za wagonjwa na Nani kataja hazina tija, wewe nawa usipige chafya kaa mbali na magenge, Basi
 
Hicho kikosi kazi kingekuwa active hivi hata kwa cases za utapeli,ingependeza sana.
 
Wanafunzi wasome waache haya mambo. Why Tanzania?, Vitu vidogo vidogo tuviache. Haileti sifa kwenye jamii.
 
Wanafunzi wasome waache haya mambo. Why Tanzania?, Vitu vidogo vidogo tuviache. Haileti sifa kwenye jamii.
Kwani chuo kilivyofungwa walipewa course work? Binti kajifungia ndani kukwepa korona mumechoropoa akifa na korona mtatukoma
 
Kutaja idadi wa wagonjwa kwenye hospital fulani ni siri pia na mpaka kawataja ina maana anajua majina yao na kama hawajui kwa majina basi hana taarifa sahihi au za ukweli na sheria itafuata mkondo wake

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwani kuna hospital kaitaja hapo kuwa ina wagonjwa 230 ?

Kwani kutaja kuwa hospitali x ina wagonjwa 230 ni siri za wagonjwa ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa msomi wa mwaka wa tatu kukosa kujua mipaka ya kuchapisha habari kwenye mtandao ni kitu kibaya Sana. Ila si ajabu Kama hawahawa wasomi ndiyo daily tunaona video zao za utupu mtandaoni maana yake hilo ni tatizo la kutokujitambua Kama wasomi.
Ukimuuliza mtu kwanini ukubali kurekodiwa video ya utupu anakwambia, it was my boyfriend who did it, I didn't know if he could be that stupid kuiweka mtandaoni. Nyoookoo stupid yeye au wewe uliyerekodiwa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom