Pre GE2025 MwanaHalisi: Siri yavuja, Watatu Wajipanga Kugombea Urais 2025 kupitia CCM, Katiba ya Chama chao yawaruhusu

Pre GE2025 MwanaHalisi: Siri yavuja, Watatu Wajipanga Kugombea Urais 2025 kupitia CCM, Katiba ya Chama chao yawaruhusu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
JPM aliujuwa huu mtandao alikuwa anataka kuwamaliza kabisa hawa lakini kuna watu waliomba msamaha yaishe ndio Nape akaenda kutoa siri zote ikulu ndio kusamehewa, Mama akaja akasema tuanze upya akawasamehe shughuli yake akaiona, kaambiwa Mama hawa watakumaliza, lazima mjuwe CCM kuna ujasusi wa hali ya juu huwezi kufanya jambo lisijulikane. Tofauti tu JPM alikuwa hana mswalie mtume Mama akaona niwe mpole ila ameshaambiwa hawa hawafai kawapiga chini, Mnaona kimyaa chao kina Nape na Makamba, sio bure wanajuwa wako chini ya Radar na wameambiwa kaa kimyaa au utapotea kisiasa. Sasa mwakani ndio utaona watu wana roho mbaya likija suala la siasa ndani ya CCM na fitna, hakuna huruma.
 
Vyama vyote Tanzania hili hawalitaki ila ngoja niongelee vyama hivi viwili kwanza. CCM, hawa katiba haikatazi ila wamejiwekea tamaduni tu ndani ya chama na ukithubutu ku challenge hilo basi jiandae kweli maana unaweza ukawa ndio mwisho wako kisiasa mnakumbuka yule aliyechukuwa form wakati wa Kikwete? japo CCM tamaduni hizi ni awamu 2 tu miaka kumi mwenyekiti mpya anakuja.

Chadema, hawa ukitia nia yakutaka kum challenge mwenyekiti chamoto utakiona utahama mwenyewe na utaanzisha chama chako yalimkuta Zitto. Hawa hatujui ni tamaduni au katiba ila ukijitosa tu ujue ndio mwisho wako umefika.

TFF, huko ukitaka tu basi utaletewe zengwe la kesi na utafungiwa maisha kushiriki kwenye soka...
Katika hizo zote taasisi tatu ulizozitaja, hakuna hata moja ambayo katiba yake inazuia wengine kugombea
 
JPM aliujuwa huu mtandao alikuwa anataka kuwamaliza kabisa hawa lakini kuna watu waliomba msamaha yaishe ndio Nape akaenda kutoa siri zote ikulu ndio kusamehewa, Mama akaja akasema tuanze upya akawasamehe shughuli yake akaiona, kaambiwa Mama hawa watakumaliza, lazima mjuwe CCM kuna ujasusi wa hali ya juu huwezi kufanya jambo lisijulikane. Tofauti tu JPM alikuwa hana mswalie mtume Mama akaona niwe mpole ila ameshaambiwa hawa hawafai kawapiga chini, Mnaona kimyaa chao kina Nape na Makamba, sio bure wanajuwa wako chini ya Radar na wameambiwa kaa kimyaa au utapotea kisiasa. Sasa mwakani ndio utaona watu wana roho mbaya likija suala la siasa ndani ya CCM na fitna, hakuna huruma.
Ngoja tuone !
 
Hakuna watu wanaogopa madaraka ya rais kama wanaccm. Wote salama yao ni mbeleko ya vyombo vya dola kupitia madaraka ya rais. Hakuna mwanaccm anathubutu kushindana nje ya ccm, kwani huko ndio kuna mbeleko ya vyombo vya dola.
Umemaliza ! 👍
 
Katika hizo zote taasisi tatu ulizozitaja, hakuna hata moja ambayo katiba yake inazuia wengine kugombea
Najuwa ila nimesema hizi taasisi zote hakuna wa kumyoshea kidole mwenzake japo CCM wana nafuu wao wamesema wazi sisi hizi ni tamaduni zetu kumpa mwenyekiti nafasi mara 2 akimaliza basi lakini wengine huko hakuna tamaduni wala limit
 
CHADEMA mnahangaika sana na kuteseka kama wagonjwa .Mnamuogopa Sana Rais Samia maana mnajuwa kuwa hamna ubavu wala uwezo wa kushindana naye katika sanduku la kura hapo mwakani.

Fomu ya Urais ndani ya CCM ni moja tu kwa ajili ya Mama yetu Mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan.View attachment 3139486
Kati ya Chadema na CCM anaemuogopa mwenzie ni nani hapo? Mtu kalipa machawa nchi nzima, maaskofu na mashehe wanahongwa fedha na magari akitafuta kuungwa mkono.
 
Yaani wewe ni mpuuzi kweli kweli,watanganyika 60 million hakuna wa kumwondoa mzanzibar!.

Hivi kuna mtanganyika anaweza kuongoza Zanzibar?.

Punguza ujinga wako.
Sawa mkuu,subiri uone,hutosadiki macho na masikio Yako,huyo mzanzibar tunaye hadi 2030,ikiwezekana Hadi 2035
 
Nyakati hizi usiamini sana waganga wa kienyeji, wale waganga na wachawi kweli wachache wapo busy na full booked kwa sababu ya jamu inayosababishwa na kuelekea 2025. Epuka kutapeliwa.
 
CHADEMA mnahangaika sana na kuteseka kama wagonjwa .Mnamuogopa Sana Rais Samia maana mnajuwa kuwa hamna ubavu wala uwezo wa kushindana naye katika sanduku la kura hapo mwakani.

Fomu ya Urais ndani ya CCM ni moja tu kwa ajili ya Mama yetu Mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan.View attachment 3139486
Sio cdm hao ni masisiemu yenyewe u
Yanachuana
 
Machawa watashangazwa dakika za mwisho. Itakuwa ni ama fomu zitolewe kwa idadi yoyote au chama kisambaratike. Salama yake itakuwa ni kufuata katiba tu. Jana na juzi, siyo leo.

Chawa wajiandae kwa vibwagizo vipya, cha fomu moja tu itaprintiwa, hakitakuwepo.
 
Yawezekana huu ndiyo ukawa uchaguzi ndani ya CCM wenye kuleta mabadiriko makubwa hadi kwenye uchaguzi mkuu.

So tukae kwa kutulia, nafaham wengi wetu hadi CCM kindakindaki kwa nje tunashangilia na kusema 5tena hadi 2030 ila kwenye uhalisia in your mind unasema bora atoke tu!.
In their mind wapo wanaotaka hivyo hivyo, lakini wa kutamka hivyo HAYUPO 😅😂 !
 
Najuwa ila nimesema hizi taasisi zote hakuna wa kumyoshea kidole mwenzake japo CCM wana nafuu wao wamesema wazi sisi hizi ni tamaduni zetu kumpa mwenyekiti nafasi mara 2 akimaliza basi lakini wengine huko hakuna tamaduni wala limit
Malinzi alikaa TFF kwa vipindi vyote kikatiba hadi muda wake ukaisha? Naomba jibu
 
Back
Top Bottom