Mwanajeshi ajinyonga, aandika ujumbe kwa mke wake "Naomba uwatunze watoto nimejitahidi nimeshindwa"

Mwanajeshi ajinyonga, aandika ujumbe kwa mke wake "Naomba uwatunze watoto nimejitahidi nimeshindwa"

Askari wa jeshi la Wananchi la Tanzania aliyetambulika kwa jina la William Chacha Giriago mwenye umri wa miaka 40 amekutwa amefariki kwa kujinyonga.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, RPC Martin Otieno amesema mtu huyo amejinyonga kwa kutumia mkanda wa suruali yake aliyokuwa ameufunga kwenye nondo ya dirisha ya nyumba ya kulala wageni iitwayo Morning Star Lodge iliyopo Mtaa wa Hazina Jijini Dodoma.

RPC. Otieno amesema tukio hilo limetokea Septemba 6, 2022 na baada ya kupekuliwa mwili wa marehemu ulikutwa na meseji mbalimbali mmoja wapo alimuandikia "Mama yangu nisamehe sana nakuomba".

Ujumbe wa pili amemuandikia mke wake umesomeka "Kwako Mama Derick nisamehe sana kwa maamuzi haya, maisha kwangu hayana maana tena ,nisamehe sana nimejitahidi nimeshindwa naomba uwatunze Watoto."
R. I . P soldier. Mimi kwa haraka haraka nahisi atakuwa alipima akakuta ameathirika na ngoma ( HIV)
 
Pesa sio kila kitu mkuu.

Kuna watu mifuko yao imevimba hatari, na bado inawawia vigumu kukabiliana na maisha.

Kuna sababu nyingi sana zinazoweza kumfanya mtu apate matatizo ya akili hapo juu umetaja moja "stress" . Stress in moderation ni kitu kizuri. Ila stress ikizidi na hujui jinsi ya ku deal nayo inaweza kuleta matatizo zaidi.

Watu wengi ambao wanafanya kazi za defence(Police, Military, Navy etc) huwa wana struggle na PTSD ( Post Traumatic Stress Disorder).

Hatujui alikuwa anapitia nini ? Ila ni wazi binadamu mwenye akili timamu anguchukua uamuzi tofauti.
Unakuta wanamwaga damu zisizo na hatia
 
Mama Derrick kama unasoma ujumbe huu pole kwa msiba njoo PM tuwalee watoto wa poti mwenzangu.
 
Kipindi nipo jkt 822 kj . Kuna kitu nilikigundua ambacho kilipelekea wanajeshi wengi kuwa walevi na stress za kutosha katika kazi yao hiyo ya uwanajeshi .

-ilikuwa hivi , Kila mwanajeshi alikuwa anazamu ya kuingia lindo pale kikosini ambako aliweza ingia mchana na wakati mwingine usiku ( wao walipenda kusema kuingia guard ).

- Sasa basi ikitokea upo guard siku hiyo labda ukatakiwa ukae getini , afu labda kuna gari au hata bogi (kundi ) Fulani la kuluta likawa limekuja pale getini na wewe ukachelewa kufungua (labda kwasababu kuna mkubwa mwingine alikuwa amekutuma Mara moja sehemu maana kule order unayopewa kwa wakati huo ndyo hapo hapo inabidi uitekeleze ).

Kutoka na kadhia hiyo ,mkuu mwingine ambaye atakuwa anaongoza Hilo bogi la makuluta au gari lililofika getini tofauti na yule aliyekuagiza , Mara nyingi alikuwa anatoa adhabu ya kukuongezea siku za lindo bila kujali Kama ulitumwa au laa , "utasikia tu baba naliongezea 14 " na ikitokea labda unataka ujitetee utasikia baba nalipa nyingi 10 , hivyo mjeda huyu itambidi akaa lindo kwa siku 24 na adhabu hii huanza kutekelezwa hapo hapo .

Halii hii huwatesa wanajeshi wengi na kuona kazi yao chungu kwasababu wengi huonekana siyo waaminifu kwa wake zao maana wake zao huwaona hawana ratiba zinazoeleweka na niwaongo waongo kwa kigezo Cha kazi hebu fikiria Ni Jana tu ulimwambia Leo utarudi afu asubuhi unamwambia mkeo sitarudi kwa siku 24 unafikiri atakuamini kirahisi ??.

Hii Ni kwa upande wa kule jkt Sasa sijajua Kama na polisi Wana Mambo Kama hayo na Kama wanayo huenda Ni moja ya sababu iliyopelekea jamaa ajae stress na kuamua kujimaliza tu.
Polisi stress zao nasikia zipo kwenye njaa ya hela,nasikia wana njaa hao.[emoji23]
 
Ujumbe ndio uniaminishe kuwa kajinyonga mimi ntakua mtu wa mwisho mpaka pale uchunguzi wa kina utakapoleta majibu huko makazini pana mambo mengi sana...wahuni kusikia ndoa zinavunjika sana wametumia huo mwanya kumpa kesi mama mjane...
 
Ukiona mambo magumu kabla ya kujiua nenda pahala ukiwa peke yako na pasiwe na watu, ongea na Mungu kwa sauti kinachokusibu, eleza unavyojisikia na unachotaka kufanya.God is real
Upo sahihi, Mimi nimeona nguvu za Mungu kabisa ukiongea nae kama baba, na sio kumpigia kelele na kulia lia.
 
Kuna watu huwa wanaandikishwa ujumbe na wosia wa mali zao at gun point, na wanasheria njaa kama yule wa Klynn wanapewa mgao na kugonga mhuri. Nothing should be taken for granted, wachunguze hasa
Bahati mbaya kabisa hatujafikia kufanya uchunguzi wa akili kubwa kiasi hicho, very sad!
 
Askari wa jeshi la Wananchi la Tanzania aliyetambulika kwa jina la William Chacha Giriago mwenye umri wa miaka 40 amekutwa amefariki kwa kujinyonga.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, RPC Martin Otieno amesema mtu huyo amejinyonga kwa kutumia mkanda wa suruali yake aliyokuwa ameufunga kwenye nondo ya dirisha ya nyumba ya kulala wageni iitwayo Morning Star Lodge iliyopo Mtaa wa Hazina Jijini Dodoma.

RPC. Otieno amesema tukio hilo limetokea Septemba 6, 2022 na baada ya kupekuliwa mwili wa marehemu ulikutwa na meseji mbalimbali mmoja wapo alimuandikia "Mama yangu nisamehe sana nakuomba".

Ujumbe wa pili amemuandikia mke wake umesomeka "Kwako Mama Derick nisamehe sana kwa maamuzi haya, maisha kwangu hayana maana tena ,nisamehe sana nimejitahidi nimeshindwa naomba uwatunze Watoto."
Hakuna watu wanaishi kwa stress kama Hawa,Tena wale wa vyeo vya vya chini,jeshini Kuna dhuluma sana,unadhulumiwa stahiki zako,huwezi kubisha maana wakubwa wanatumia amri za kijeshi,basi unaumia ndani kwa ndani!
Huyu angeenda kuwalipua ccm kifo chake kingekuwa poa.
 
Awa watu wanalitiaga stress kubwa sana aisee uyu nae kajinyonga...wenyewe wanasema amekufa kiboya na Mizinga ya heshima hatopigiwa wala hatoagwa kijeshi
Na mbinguni Sir God ana kesi naye pia... Kiufupi kakosa bara na Pwani
 
Back
Top Bottom