Mwanajeshi ajinyonga, aandika ujumbe kwa mke wake "Naomba uwatunze watoto nimejitahidi nimeshindwa"

Mwanajeshi ajinyonga, aandika ujumbe kwa mke wake "Naomba uwatunze watoto nimejitahidi nimeshindwa"

Hapo kitu cha kwanza ni kuangalia kama mwandiko ni wake au lah. Cha pili ni kufuatilia simu yake na tatu kumchukua maelezo mkewe kuhusu tabia na mwenendo wake na alikuwa anasumbuliwa na nini
naona watu wa forensic hamko mbali
 
Kipindi nipo jkt 822 kj . Kuna kitu nilikigundua ambacho kilipelekea wanajeshi wengi kuwa walevi na stress za kutosha katika kazi yao hiyo ya uwanajeshi .

-ilikuwa hivi , Kila mwanajeshi alikuwa anazamu ya kuingia lindo pale kikosini ambako aliweza ingia mchana na wakati mwingine usiku ( wao walipenda kusema kuingia guard ).

- Sasa basi ikitokea upo guard siku hiyo labda ukatakiwa ukae getini , afu labda kuna gari au hata bogi (kundi ) Fulani la kuluta likawa limekuja pale getini na wewe ukachelewa kufungua (labda kwasababu kuna mkubwa mwingine alikuwa amekutuma Mara moja sehemu maana kule order unayopewa kwa wakati huo ndyo hapo hapo inabidi uitekeleze ).

Kutoka na kadhia hiyo ,mkuu mwingine ambaye atakuwa anaongoza Hilo bogi la makuluta au gari lililofika getini tofauti na yule aliyekuagiza , Mara nyingi alikuwa anatoa adhabu ya kukuongezea siku za lindo bila kujali Kama ulitumwa au laa , "utasikia tu baba naliongezea 14 " na ikitokea labda unataka ujitetee utasikia baba nalipa nyingi 10 , hivyo mjeda huyu itambidi akaa lindo kwa siku 24 na adhabu hii huanza kutekelezwa hapo hapo .

Halii hii huwatesa wanajeshi wengi na kuona kazi yao chungu kwasababu wengi huonekana siyo waaminifu kwa wake zao maana wake zao huwaona hawana ratiba zinazoeleweka na niwaongo waongo kwa kigezo Cha kazi hebu fikiria Ni Jana tu ulimwambia Leo utarudi afu asubuhi unamwambia mkeo sitarudi kwa siku 24 unafikiri atakuamini kirahisi ??.

Hii Ni kwa upande wa kule jkt Sasa sijajua Kama na polisi Wana Mambo Kama hayo na Kama wanayo huenda Ni moja ya sababu iliyopelekea jamaa ajae stress na kuamua kujimaliza tu.
 
Yeah!, nilitaka kusema kwamba, wamehakikisha huo mwandiko wa kwenye ujumbe ni wake? Pakuanzia ni hapo kwanza. Mauaji mengi yanasakiziwa suicide.
Kuna watu huwa wanaandikishwa ujumbe na wosia wa mali zao at gun point, na wanasheria njaa kama yule wa Klynn wanapewa mgao na kugonga mhuri. Nothing should be taken for granted, wachunguze hasa
 
Kwa hiyo suluhu ya kujitundika imekuwa sahihi?
Inaonenaka hata nilichokiandika hujakisoma...mstari wa wapili kutoka mwisho na huo wa mwisho suluhisho nimeliandika...
 
Askari wa jeshi la Wananchi la Tanzania aliyetambulika kwa jina la William Chacha Giriago mwenye umri wa miaka 40 amekutwa amefariki kwa kujinyonga.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, RPC Martin Otieno amesema mtu huyo amejinyonga kwa kutumia mkanda wa suruali yake aliyokuwa ameufunga kwenye nondo ya dirisha ya nyumba ya kulala wageni iitwayo Morning Star Lodge iliyopo Mtaa wa Hazina Jijini Dodoma.

RPC. Otieno amesema tukio hilo limetokea Septemba 6, 2022 na baada ya kupekuliwa mwili wa marehemu ulikutwa na meseji mbalimbali mmoja wapo alimuandikia "Mama yangu nisamehe sana nakuomba".

Ujumbe wa pili amemuandikia mke wake umesomeka "Kwako Mama Derick nisamehe sana kwa maamuzi haya, maisha kwangu hayana maana tena ,nisamehe sana nimejitahidi nimeshindwa naomba uwatunze Watoto."
Sawa,Hawa Askari wenu fake muwe mnawafundisha saikolojia ya kukabiliana na msongo wa mawazo..
 
Unampa nafasi shetani,anakufungafunga,inafikia mpaka mahali unashindwa kuchomoka,na kwakuwa hukuamua kumtumainia Mungu,unakata tamaa kabisa ya maisha na huoni tena maana ya kuishi.Hii ni case ya pili nilioisikia mimi ndani ya mwezi huu Septemba,mmoja ni mfanya biashara mwenye uwezo tu, amejinyonga kisa amekuwa na madeni mengi,huyu naye ni wa pili issue ni kama inafanana..
 
Inaonenaka hata nilichokiandika hujakisoma...mstari wa wapili kutoka mwisho na huo wa mwisho suluhisho nimeliandika...
Unarudi pale pale kwenye mockery.

Unashusha hadhi ya mfumo wa jeshi letu kwamba wanaishi kijima kabisa.
 
Mental health is important,so sad,waongezewe mishahara wanafanya kazi kubwa hawa!
 
Kuoa mwanamke mzuri afu hana uaminifu ni balaa !! ndiyo maana imeandikwa "Wanaume tuishi na wanawake wa AKILI" 1 Pet 3:7
Pole kamanda ila naomba tu unipe number ya Mama Derick ili nikampe pole.
 
Kaacha kiasi gani cha kuwatunza hao watoto ?

Huku ndio kuchuma janga ili ukale na wa kwenu

Ila isijekuwa watu wamepitia hapo kufanya murder na kui-pose kama kujiua !!!!
Wewe jamaa huna huruma
 
Unampa nafasi shetani,anakufungafunga,inafikia mpaka mahali unashindwa kuchomoka,na kwakuwa hukuamua kumtumainia Mungu,unakata tamaa kabisa ya maisha na huoni tena maana ya kuishi.Hii ni case ya pili nilioisikia mimi ndani ya mwezi huu Septemba,mmoja ni mfanya biashara mwenye uwezo tu, amejinyonga kisa amekuwa na madeni mengi,huyu naye ni wa pili issue ni kama inafanana..
Wewe inakuingia akilini hiyo? Uchunguzi ufanyike na hapo pia..
 
Back
Top Bottom