Mwanajeshi, Kapteni Tesha ajitoa muhanga kuongea hatari ya Taifa linapoelekea

Mwanajeshi, Kapteni Tesha ajitoa muhanga kuongea hatari ya Taifa linapoelekea


View: https://www.youtube.com/watch?v=W05IF22nAfI

Kupitia YouTube, Kapteni Tesha anaanza kwa kusema..

"Habari za wakati huu watanzania Kwa majina naitwa K Tesha afisa kutoka jeshi la wananchi wa Tanzania katika kikosi [00:03] cha Saki kwa maana kwamba ni shule ya anga ya kijeshi Awali ya yote napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu muumba mbingu [00:13] na nchi kwa kunipa uhai na afya mpaka muda huu ambapo nazungumza nanyi Watanzania wenzangu nikiwa na maumivu makubwa sana [00:21] moyoni juu ya haya yanaendelea katika nchi yetu...""

Muhtasari.
Kapteni K. Tesha, afisa anayejitambulisha kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (Saki/Shule ya Anga ya Kijeshi), anatoa maoni yake kwa umma kuhusu hali anayoiona katika taifa.

Hoja Kuu za Kapteni Tesha:
  • Hatari ya Taifa: Anadai anaona hatari kubwa mbele ya taifa kutokana na yale yanayoendelea [00:30]. Anasema ametoa barua kwa wakubwa wake, akiwemo CDF, kuonyesha kutoridhishwa kwake na hali ya nchi [01:35].
  • Jeshi Kuchukua Nchi: Anashauri Jeshi la Ulinzi wa Wananchi (JWTZ) lichukue nchi haraka ili kuweka mambo sawa, akidai kuwa imani pekee ya Watanzania imebaki kwenye jeshi [02:34]. Anataka uchaguzi uzuiwe kwa sababu una mtego na umejaa makashfa [01:00:25].
  • Deep State: Anaelezea dhana ya "Deep State" kama kundi la watu wenye ushawishi ndani ya serikali au taasisi za dola (serikali ndani ya serikali) ambalo linaendesha maamuzi nyuma ya pazia [04:19]. Anadai kundi hili nchini linaongozwa na "CCM Mtandao" wakiwemo Mstaafu Kikwete na Rostam Aziz.
  • Uchunguzi wa Kifo cha Magufuli: Anasisitiza kuwa kifo cha Hayati Rais Dkt. John Pombe Magufuli kichunguzwe na Jeshi kwa haraka, akitaja taarifa kwamba kinaweza kuwa kimesababishwa na CCM Mtandao.
  • Ushauri kwa CDF: Anamuomba CDF (Mkuu wa Majeshi) asikubali siasa kuingizwa Jeshini kwa kuwa inaweza kugawanya umoja wa jeshi, na anashauri Kikwete na mtandao wake wakamatwe kujibu tuhuma za ufisadi na kifo cha Magufuli .

Kwanini anamuomba CDF wakati yeye aneshakuwa compromised?

Kama kutetea nchi, watetezi watatoka ngazi za chini siyo kwa CDF, IGP, au mkuu wa usalama.

Nafikiri hili kauli ni onyo kwa kwa wahuni.
 
Watu walituona wapuuzi tuliposema tunatoka 29 OCT, kiko wapi ? Jeshi lipo upande wa wananchi.
Tarehe 29 tunatoka.
Nataka kuamini kwamba huyu jamaa ana changamoto ya afya ya akili la kama si hivyo ana watu wengi sana ndani ya jeshi wako nyuma yake!
 
Huyu watamcourt marshal tu, kajitoa muhanga kwa sheria zetu mbovu za jeshi ni uasi kafanya!

Ila katoa message muhimu sana kuonyesha wanasiasa kwamba wanajeshi tena hata maofisa hawaridhiki na hali hata kama wanawalipa fweza zaidi
Unafikiri yeye hakujua yote hayo? Huyo ana watu nyuma yake hajakurupuka..!!

Sema mi ndiomana nawapenda wachaga ni wanaume na nusu..!!
 
Kwanini anamuomba CDF wakati yeye aneshakuwa compromised?

Kama kutetea nchi, watetezi watatoka ngazi za chini siyo kwa CDF, IGP, au mkuu wa usalama.

Nafikiri hili kauli ni onyo kwa kwahuni.
Ili kikitokea cha kutokea CDF asitafute wa kumlaumu alishaambiwa nini kinachoenda kutokea mapema ndio maana kamuelekezea yeye ndivyo wanavyofundishwa wakiwa kambini unapowasilisha jambo kwa mkubwa afanyie maamuzi yeye mkubwa wake ni CDF sio huyo mkubwa wako wewe ulietaka amtajetaje kwenye video sio tofauti na hapo
 
Kwanini anamuomba CDF wakati yeye aneshakuwa compromised?

Kama kutetea nchi, watetezi watatoka ngazi za chini siyo kwa CDF, IGP, au mkuu wa usalama.

Nafikiri hili kauli ni onyo kwa kwahuni.
Sasa CDF ni nani kama wanajeshi wa chini hawamsikilizi? huyu anazungumza kwa sababu nyuma ana backup kubwa tena sana, na amejiridhisha vya kutosha hadi kufikia hatua hio..

Polepole pia kukataa ubalozi ilikuwa si bure, ana back up ya kutosha, alishasema waandishi na vyombo vya usalama watunze kumbukumbu za wahalifu na watekaji kwani siku inakuja lazima hao watekaji wawajibishwe.

Na huyo kapteni kasema wazi wanajeshi wengi wapo upande wa wananchi.

Soma alama za nyakati, wanajeshi waliobaki upande wa Samia ni wanufaika,CDF mwenyewe ni chawa kindakindaki.
 
Hatimaye nimefanikiwa kuimaliza interview yote

Haya ngoja nika shee na wana kwenye flash nianze na ile liblary ya mtaani yenye maspika makubwa yule mjinga ukimpa hata buku anaweza ku play hadi X kwa sauti ya juu.

1759581006010.png
 
Back
Top Bottom