Mimi maoni yangu ni kwamba mwanamke hawezi fanya hayo uliyo yaeleza hapo juu japo umesema baadhi, ungesema mabinti ningekubali maana huwa tunawaona huku vyuoni hata mtaani
Vibinti vya chuo wengi wao japo sio wote huwa wanapenda show-off za hivyo huwa wanaishi kwa kutambiana leo huyu kaweka nywele za100k mwenzake mwenye tamaa akiona nae atafanya kila kitu nae aweke hata zaidi ya hiyo na kama hana hela na ana boyfriend basi ujue huyo boyfriend ataenda kusumbuliwa mpaka atoe hela binti akasuke au avae amzidi mwenzake
Na hii hata kwa wavulana huko vyuoni baadhi nao hufanya vitu kama hivyo, wanavaa kuimpress wasichana au kushindana na wavulana wenzao na hao nao wakisha kuwa wakubwa na kuwa wanaume huwa wanaacha hizo show-off.