mamamzungu
JF-Expert Member
- Nov 17, 2019
- 2,554
- 4,271
Usisikilize ramli chonganishi, mara nyingine mama zetu hawana vifua, unamshirikisha Jambo na yeye chap anashirikisha marafiki zake, wajomba, majirani huko ndio anaatract negative energy bila yeye kujua.
Mimi nikimshirikisha Jambo langu mama namwambia kabisa usiwaambie wengine, wasije kuleta husda tukafeli.
Halafu wakati mwingine na wewe Jikaze, usimwambie yoyote Jambo lako, hata mama, Kama Una pesa kidogo mpe huku ukitia nia Ile pesa unayompa ilete baraka kwako.
Umesema ukweli wamama hawana siri mpk unaogopa kumwambia yaani mimi siwezi kumueleza jambo langu la msingi ambalo sitaki wengine walifahamu mpk pale litakapo kamilika
Nimewahi kumdokeza tu kuna mtu nimempata ila sina uhakika nae akaenda kuwaambia ndugu zake ndugu zake Nao wakasambaza nikaanza kupigiwa simu za kuulizwa mpk nikaona aibu namuuliza kwanini ulisema ananikazia et kwani kuna ubaya gani
Na mchumba nikakosa