Mwanamke mmoja Iran aamua kuwakera Ma-Ayatollah kwa kutembea na nguo zilizopigwa marufuku mtaani

Mwanamke mmoja Iran aamua kuwakera Ma-Ayatollah kwa kutembea na nguo zilizopigwa marufuku mtaani

Shida siyo hijab,we kwa utashi wako alivyovyaa unaona ndiyo maana halisi ya uhuru? Kama Uhuru ni kuvaa uchi,basi hiyo tafsiri inatumika vibaya
Alikuwa amevaa hijabu askari wa maadili wakamkata na kuanza kumsumbua kwamba hajavaa hijabu vizuri ndipo akaamua kuivua kabisa hiyo hijabu, hapo hajavaa uchi amevaa kama ukiwa na mke wako na watoto wako beach.
 
Attachments

  • Screenshot_2024-11-04-01-16-43-354.jpg
    Screenshot_2024-11-04-01-16-43-354.jpg
    270.4 KB · Views: 1
Alikuwa amevaa hijabu akakamatwa na kusumbuliwa na polisi wa maadili kwamba hajavaa hijabu vizuri ndipo akakasirika na akaamua kuitupa kabisa hiyo hijabu, hana matatizo yoyote ya akili.
Ila hajavaa kimini. Amevua nguo za juu na kubakia na chupi na sidiria (underwear). Huo sio uhuru wa kuvaa. Nchi nyingi angeonekana kichaa na kukamatwa.
 
Ila hajavaa kimini. Amevua nguo za juu na kubakia na chupi na sidiria (underwear). Huo sio uhuru wa kuvaa. Nchi nyingi angeonekana kichaa na kukamatwa.
Hapa ni Zanzibar
 
Kupendeza au kutopendeza sio suala la msingi, unavyojisikia kuhusu mama yako, dada yako au mtoto wako anavyovaa sio suala la msingi pia. Suala la msingi ni uhuru wake wa yeye au wao kuvaa wanavyojisikia kwa uhuru bila kubughudhiwa, yani kama mke wako au mama yako amechagua kuvaa hijabu na mke au mama wa mwingine amechagua kuvaa kimini na top tu wote wawe na haki sawa.
Jinsia yako tafadhali ili tuendelee na mada
 
Alikuwa amevaa hijabu akakamatwa na kusumbuliwa na polisi wa maadili kwamba hajavaa hijabu vizuri ndipo akakasirika na akaamua kuitupa kabisa hiyo hijabu, hana matatizo yoyote ya akili.
Bosi Iran watu kibao wanatembea vichwa wazi, hiyo video yako tu kuna watu kibao wapo vichwa wazi, tatizo lenu nyie mmejaa propaganda kwenye vichwa, kuna watu kibao watalii wanachukua video za Iran, kumejaa maelfu ya video youtube watu wakionesha Iran watu wanaishi vipi, badala ya kusubiria propaganda ndo ziwe elimu yako.
 
Iran ni lazima wanawake kuvaa hijab kisheria kwenye umma, wasiovaa wanavunja sheria na inategemea siku hiyo basij militia wameamkaje.
 
Mojawapo ya mambo yanayonifanya kuendelea kusimama na Israel ni hili la uhuru, Israel ndio nchi pekee ya Mashariki ya kati unavaa vyovyote, unapata kitimoto, unakunywa chochote na unaweza kuabudu chochote bila kusumbuliwa au hofu.
Kuvaa hivyo hapa TANZANIA unaruhusiwa?
 
Back
Top Bottom