Jemima Mrembo
JF-Expert Member
- Jul 19, 2021
- 2,864
- 8,328
Wanawake tuna nguvu kubwa ambayo hatuithamini na tunaipuuza na kuidharau ndio maana sisi tunaongoza kushinda kwa waganga na kwenye makanisa ya kinabii.
Nguvu hiyo kubwa tuliyonayo ni unyenyekevu. Tukiweza kuwa wanyenyekevu kwa wanaume wetu, na kuwaombea, migogoro inapungua na kutoweka kabisa.
Unyenyekevu wa mama ni faida kwake binafsi, faida kwa baba na faida kwa watoto na familia nzima.
Mwanamke mnyenyekevu ndiye mwanamke mwenye hekima ya kuishi na mume.
Ni mwanaume gani ambaye ndoto yake ni kuwa na mwanamke, jeuri, kiburi na mkaidi? Mwanamke mwenye dharau, mdomo mchafu na asiye na heshima kwa mume?
Bila kuwa mnyenyekevu hamna hofu ya Mungu moyoni mwako