Acha kutupia lawama upande mmoja
Mwanamke kuwa jeuri haina maana umtelekeze mtoto wako ateseke,, na kwa taarifa yako humkomoi mwanamke una mkomoa mtoto wako
Maana mwanamke yakimshinda kulea mtoto anatelekeza kwa ndugu yeye anaenda mjini kula raha,, sasa kwa hiyo picha nani amekomolewa kama sio mtoto wenu
Haijalishi umegombana na mwanamke tafuta namna ya kutunza hicho kiumbe chako kama mama mtu anagoma ushirikiano kwa sasa lazimisha hivyohivyo mwisho wa siku atalegeza
Shida yenu ninyi wanaume mnafanyaga vitu mkizani mtawakomoa wanawake kumbe mnajikoMoa kizazi Chénu
Kwahiyo unachotaka kusema ni kuwa mwanamke kutelekeza mtoto na kwenda kula raha ni sawa ila mwanaume kushindwa kulea mtoto na mwanamke asiye na utimamu wa kiakili wala msingi wa maadili tatizo anakuwa ni mwanaume?
Why unakwepa kuwajibisha mwanamke kwa nguvu sawa na ile unayotumia kumuwajibisha mwanaume?
Nadhani ifike hatua tuanze kuzingatia kuwa wanawake nao ni binadamu wenye utashi na maamuzi.
Mambo ya kuwapa "Free Benefit of a doubt card" hayatafanikiwa katika kizazi hiki cha wanaume wenye macho mbele ya uso,kisogoni,utosini,chini ya kidevu na pande mbili zote za kichwa. Tunatazama uwajibikaji kwa jicho la 360.
Hakuna kusema mwanamke hapa amekosea sababu mwanaume kasababisha yeye wakati anafanya uzembe alikuwa hatambui madhara,why sasa akwepe kuwajibika?
Hawa masingle mother wengi wao kuteseka ni kitu wamejitakia,ukiwauliza hakuna watu responsible waliwakataa sababu walikuwa ni watu wamenyooka utaona sura zao namna zinapatwa na aibu. Kila single mother,katika story yake ya maisha yake ya kuteswa na wanaume,kuna story ya wanaume aliyewatesa yeye na kuwakataa hatoiweka wazi au kuihadithia huku nafsi yake ikijua wazi kuwa hawa wanaume walikuwa ni sahihi kwake na wangempa maisha mazuri na anajutia kutowaheshimu au kukubalia mojawapo awe mume wake.
Atahadithia tu namna wanaume aliowataka na kuwafuata yeye kwa utashi wake wa udangaji na umalaya,kisha wakamnyoosha.
Wengi wamelala na wanaume kwasababu walikuwa wanajaribisha,au kutest mahusiano huku wakiachia miili yao itumike kama wake halali. Mimba ikiingia lawama kwa mwanaume ambaye alishampa angalizo kuwa hatalea mimba wala mtoto kama mwanamke akiruhusu ujauzito uingie,kwann hawasemi kama hautajihusisha na mtoto basi hapa ndipo tunaishia, kwann huwa wanaendelea kulala nao na kujibebesha ujauzito halafu wanasema "nitalea mtoto wangu mwenyewe"?