Aisee...huyo ni mtoto. Anaonesha anakupenda. Ila kwa jinsi ya maelezo yako kuwa alikukataa kwanza na sasa anataka kuolewa kwa speed hii. Nashauri kama umempenda kuwa naye ktk mahusiano huku ukimchunguza. Kwa umri wake, na kama wewe umemzidi kiasi basi ni rahisi kujua tabia yake halisi. Unadishi wake ni umri na siyo tabia. Mawazo yake ya kitoto ni mazingira take na umri wake. Anaweza kuwa anakupenda kweli Ila hajajua ni style ipi ya kuonesha huo upendo wa dhati ambao watu wa JF wanaweza kuupima na kukupa GO AHEAD YA KUMUOA.
Watu wengi humu wanatamani kuwa ktk umri wako na kuanza mahusiano ya ndoa kama hivyo sema ndo hivyo tena....
Unaweza kuta watu zaidi ya 100 hawana wa kuwaambia maneno kama hayo hata kama ya uongo au ya kitoto.
Ushauri wangu, kama hamjapishana saaana kiumri anzisha mahusiano ya dhumuni la kumuoa. Lakini usiharakishe kumuoa au kuishi naye kwa sasa. Hii itakupa muda wa kumjua vizuri tabia, mihemko, mwenendo, background etc.
Halafu umesema amempigia mama ako Mdogo? Ina maana familia zinajuana?