Kuna vitu vikikaliwa kimya hasa vikiwahusisha Wanawake vinazidi kuwaharibu Wanawake, mfano wa haya ni huu uzi wako.
Kuna jambo unatakiwa kulijua, kuna mambo huwa hayapitwi na wakati na wala hayapaswi kuathiriwa na wakati, utu,silika na nafasi ya mwanaume na mwanamke katika kujenga jamii. Hivi vitu hata mabadiliko yawe yatakavyo kuwa wakati unatakiwa kufata vitu hivyo, yaani utu, silika na nafasi ya mwanamke na mwanamke hii ndiyo asili, ukiviacha vitu hivi madhara yake ni haya tunayo yaona hapa.
Nukta hii umeilezea kwa kumili upande mmoja, Mwanamke ni kweli hapaswi kuburuzwa na sisi Wanaume hatutakiwi tuwe watemi kwa wake zetu kwani utemi si katika mapenzi bali ni uharibifu.
Lakini, je ni kweli wanawake wa leo wanaelewa vipi tamko kuburuzwa ? Tamko hili wanalielewa vibaya bali wanawake wa leo wametengenezwa kuwa na hofu na kutuona sisi Waume zao kuwa ndiyo maadui zao wakubwa na tunawakwamisha, na kila uchwao wanapambana kushindana na sisi.
Bali hakuna zama ambazo Wanawake wamekuwa wajinga kuzidi zama hizi, mwanamke amekuwa kama Mshumaa tu na amezidi ujinga mno.
Demokrasia si mfumo sahihi kuanzia kwenye afya ya akili mpaka utendaji, ungekuwa mfumo sahihi ungetumika tangu na tangu.
Hapa kuna tatizo mahali. Unakaaje na mwanamke asiye kuheshimu ?
Umbile la mwanaume linamtaka mwanamke awe chini yetu. Na hii ndiyo furaha yetu sisi Wanaume bsli mpaka wao wsnapenda kuwa chini yetu, ila tu kuna wajinga wamewawahi.
Hili siyo lazima, ila hapa pa Mwanamke kutoka kazini, hivi wanaume wenzangu huwa mnawaza nini au mnawezaje kuandika jambo kwamba "Mwanamke ametoka kazini" na wewe Mwanaume upo ?
Mimi mmoja wapo nataka watoto zangu wa kike wakae majunbani mwao sababu huko ndiyo salama yao ilipo, sababu mama zao mama wa nyumbani.
Nani alikudanganya ya kuwa Mwanamke akiwa nyumbani hatimizi ndoto zake ? Wapo wanawake wengi wako majumbani na wametimiza ndoto zao kuliko hata hao ambao wanapambana kuutafuta ugali.
Ndoto zao na wapo Wanawake wengi zaidi waliopo maofisini na wanatafuta ugali hawajitimiza ndoto zao.
Nyinyi ndiyo mnazidi kuwafanya wanawake wazidi kuwa wajinga na wawe wavivu wa kufikiria na mwisho wa siku wanakuwa bidhaa na wao wanao sawa kwamba wamekombolewa
Hivi kuna haja gani ya Mwanamke kutoka kwenda kazini hali ya kuwa wewe unaleta nyumbani ?
Dunia imebadikika ila uhalisia haujabadilika na silika zetu hazijabadilika. Tuishi kwenye asili huko ndiko usalama ulipo.